Tanga ni kama haina serikali kabisa, matapeli wa viwanja wanafanya wanavyotaka kwa kujitapa kuwa hakuna wa kuwatia nguvuni

je parle

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2018
Posts
2,022
Reaction score
3,919
Nina andika kwa masikitiko makubwa huu mji wa tanga umekuwa wa hovyo mno .As if if hakuna serikali inayofanya kazi zake kwa weledi. Hii mata ya changani kuna huyu mwenyekiti anaitwa masumbuko sijui aliwezeje kukalia kiti cha kuwa mwenyekiti. Yan hana weledi alafu ni tapeli na nusu wao pamoja na baraza lote la kata. Huyu mwenye kiti wanapita na vijana wake. MTAJA, NA KIJANA MWENGINE ANAITWA SEMINDU. Hawa kazi yao kubwa ni kuangalia sehemu gani kuna kiwanja hakija jengwa.

Wakishaona hivyo wanaleta mteja kuja kununua ki siri siri ,watu wengi wameshalizwa kwa style hii. Alafu mzigo wanagawana na mwenyekiti, na siku ukija kugundua kiwanja chako kimeuzwa mara mbili ndio hapo mwenyekiti anaanza kukupiga danadana hadi ukate tamaa. Na katika madai wakishakuona utawazidi nguvu wanakupa kiwanja kingine cha mtu mwingine ambae hajajenga na yeye akija kugundua kesi inakuwa tena kupelekeshana hivyo hivyo.

Rushwa ni kubwa sana inafanyika hapa kichangani. Serikali ya jamhuri imeshindwa kuwafunga hawa watu watatu mwenyekiti masumbuko, mjata,na semindu. Kwanza hawa wanahatibu sifa ya watu wa tanga ya ukarimu na kupendana. Nina wasiwasi hawa jamaa watatu sio raia wa Tanzania.

Tunaomba uhamiaji pia kuwafuatilia kujua uraia wao. Huyu mmoja semindu alishawai kuuza kiwanja cha mdigo mmoja akarogwa ikawa anaona usiku tu lakin mchana haoni .ila baadae vikao vingi vilifanyika na akasamehewa ila sasa wamerudia michezo yao ile ile.

Na hata akipelekwa polisi hapo chumbageni ni kama tu hamna kitu siku mbili wameachiwa kwa dhamana na wanaenda kuuza tena viwanja.
 
Kwanini ununue kiwanja kwa mwenyekiti? Na kwanini ununue kiwanja kisichopimwa?
 
Waswahili ni matapeli tapeli sana kwenye mambo hayo ya viwanja, ni kuwa makini hasa kama unanunua eneo ambalo halijapimwa na kupewa hati.
 
Kwanini ununue kiwanja kwa mwenyekiti?
na kwanini ununue kiwanja kisichopimwa?
1. Ya kwanza you have a point. Mwenyekiti hana mamlaka ya kuuza/kusimamia uuzaji/ununuzi wa viwanja. Watu masikii hawajiu, hasa wadigo wenzangu. Mbumbumbu kabisa na hawamwamini yeyote kama wewe si mdigo mwenzao. Nime deal nao sana nawajua fika kwa hilo. Wakishalizwa, ndiyo wanakuja kwako kuwa kumbe ulikuwa na msaada mkubwa kwao..

2. La pili siyo swa. Hakuna kosa/ujinga kununua ardhi ambayo haijapimwa. After all ardhi nyingi inamilikiwa kimila, ni mashamba ya watu wanayakata viwanja. La kushauri nikuwa kabla hujanunua eneo la mtu nenda ardhi uhakikishe mipango miji pale kuna plan ya kitu gani ie makazi, viwanda, garage kanisa ,msikiti, njia/barabara etc etc .. Othewise hakuna tatizo kubwa kununua ardhi ambayo haijapimwa ukizingatia hilo la kwenda Mipango miji!
 
Lakin sasa kwa ni hata polisi na wao wanashirikiana na matapeli.

Kama polisi ni kulinda watu na mali zao kwa nini hawa wanalinda matapeli na utapeli wao

Hawa wakina masumbuko na mjata wanajulikana sana chumbageni polisi na hakuna hatua zinazo chukuliwa juu yao

Inamaana wapo juu ya serikali hii ni aibu kubwa
 
pale mitaa ya mabawa juzi napita naona wanatakiwa waondoke wawapishe waarabu kwenye eneo lao
Wapumbavu sana miaka ya mwanzoni ya 2000's nilikuwa pale ule uwanja wa mzalenso waliuziwa waarabu wakafnya mkaburi achana na haya ya mabawa yanayotazamana karibu na kituo cha polisi.

Aliyeuza alikuwa ni meya wa jiji na hakuna kitu walimfanya..ule uwanja wa mzalendo aisee uliibua vipaji vingi sana enzi izo ila uliuzwa😥
 
You can reclaim it if it was fraud
 
1. Ya kwanza you have a point. Mwenyekiti hana mamlaka ya kuuza/kusimamia uuzaji/ununuzi wa viwanja. Watu masikii hawajiu, hasa wadigo wenzangu....
Ardhi chache Tanzania zina ramani za mipangomiji . Kama unatokea Dar ukawnda udigoni kununua ardhi, basi ipime kwanza ndiyo uinunue.

Tafuta majirani, jaza SF92 peleka kata wapitishe maombi uipime. Ikiwezekana uandae TP kabisa.

Otherwise risk ipo palepale . Kuna ardhi dar es salaam hazina TP sembuse udigoni.

Kama unataka ardhi ya kuishi wewe na familia yako, basi iwe ardhi ya Kijiji (siyo ilyo Chini ya serikali ya mtaa) au iwe imepimwa na unaweza kuangalia matumizi au any incumbrances.

Ardhi ya Kijiji ipo Chini ya village council, na ikipitisha manunuzi you stand a good chance kwanza itakuwa poa. Kukiwa na matatizo utashitaki Kijiji which is a body corporate.

So make sure Kuna kikao cha village council with a quorum na balance ya wanawake kwa wanaume kama inavyotakiwa (at least 2 females). Pata minutes na approval halafu Fanya manunuzi kimkataba.
 
distinction between the two ie serikali ya mtaa na serikali ya kijiji
Serikali ya mtaa zinaundwa chini ya Local Government (urban authorities) Act, na serikali za vijiji zinaismamiwa na Local Government (District authorities) Act.
Kwenye Local Government (Urban authorities )Act, pia kuna village governments.

Village government (village council) ni body corporate na ina vitongoji (hamlets) chini yake, pia council yake in wajumbe 27 kama sikosei, wakati Serikali ya mtaa siyo mamlaka bali ni extension tu ya kata ili ifanye kazi kwa ufanisi, pia ina wajumbe 7 tu. na siyo body corporate, huwezi ishitaki.

Village government ni trustee wa village land na msimamizi wa biashara zote za village (under Local government Finance act). kwa hiyo transactions zote especially za immovable property lazima ziwe approved na village council.
 
Asante nimekupaya vema.
Hata nikitaka kuuza shamba langu la urithi Kwa mfano, approval ya Kijiji ni lazima?
 
Yes,
Pia ni vizuri uonyeshe mgawanyo wa mali hiyo ya urithi. Angalau muhtasari wa kikao cha familia. ila ni vyema kuonyesha usimamizi wa mirathi na mgawanyo ulivyofanyika.
Hapo ndiyo ukaombe consent ya village council.
 
Yes,
Pia ni vizuri uonyeshe mgawanyo wa mali hiyo ya urithi. Angalau muhtasari wa kikao cha familia. ila ni vyema kuonyesha usimamizi wa mirathi na mgawanyo ulivyofanyika.
Hapo ndiyo ukaombe consent ya village coun

Nilikuwa najiuli sana kuhusu issue hiyo huko nyuma baada ya kuoma kesi hii page 8. Nikashituka kuwa ardhi yangu niombe kijiji consent? ndiyo maana Lisu anasema ni ushenzi wa katiba hii.

By the way, it seems haya mambo ya shria unauelewa nayo. Ngoja nikuletee kifungu unipe tafsiri yake. Kuna appeal inakwenda CA kuomba tafsiri maana wanasema kuna mkanganyiko wa interpretation.
 
Attachments

Serikali ya mtaa zinaundwa chini ya Local Government (urban authorities) Act, na serikali za vijiji zinaismamiwa na Local Government (District authorities) Act.
Kwenye Local Government (Urban authorities )Act, pia kuna village governments.

Village government (village council) ni body corporate na ina vitongoji (hamlets) chini yake, pia council yake in wajumbe 27 kama sikosei, wakati Serikali ya mtaa siyo mamlaka bali ni extension tu ya kata ili ifanye kazi kwa ufanisi, pia ina wajumbe 7 tu. na siyo body corporate, huwezi ishitaki.

Village government ni trustee wa village land na msimamizi wa biashara zote za village (under Local government Finance act). kwa hiyo transactions zote especially za immovable property lazima ziwe approved na village council.
Ebu soma hiyo kesi uone Adv. Chamani anavyosema
 
Nisaidie hii kitu, seems unaijua sheria. kama nimekusumbua , appology!
 
Back
Top Bottom