Tanga Pazuri Sana Sema Sijui kwa Nini Pako Vile

Tanga ushirikina sana yaani mtu akiumwa kidgo tu mawazo yashahamia kwenye kurogwa, hiyo ya uvivu ni kweli kabisa shemeji yenu akiendaga kwao basi familia yote mpaka mume wa dada yake wanakusanyika kula hapo hapo, sembe inapikwa kilo 3 mpaka 4 kwa mara moja, wali ndio kabisa unaweza sema Kuna sherehe na mtoaji wa pesa ni Mimi basi Huwa nakereka sana, mm ni mnyaturu
 
Daaah hili nalo ni shida ingine
T
๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ––๐Ÿพ
 
Too much umwinyi is equals to 2-2
 
Nadhani wasambaa wanaongoza! Kama mmoja ana kazi au uwezo fulani ukoo mzima wanahamia hapo!
 
Ni pazuri hali ya hewa. Kuhusu wanawake kuwa makini sana. Wana mapenzi mazuri ila hawakai kwenye ndoa. Pia ukienda kikazi ukapata demu ukijieleza akakujua ukitoka unamwacha ana mimba. Kama u aheshashimu watoto basi ndio wako tena. Yeye anaendelea kulea wewe unatunza. Akiukizwa, babake yuko Dar au Arusha na sasa Dosoma. Hawachelewi kwa hilo.
 
Wenyeji wapunguze ushirikina
Tanga Ni nzuri sana ingekuwa inakimbizana na dar basi tu ushirikina umezidi
...Ni kweli. Zamani Tanga ilikuwa inakimbizana na Dar, lakini mwenzake Dar akasonga mbele yeye akabaki pale pale na kupitwa na 'watoto' ambao kwake walikuwa Hawasemi, Mwanza, Moshi, Mbeya, Morogoro n.k [emoji846] !
 
...Acha Uchoyo, Mnyaturu ! [emoji846]...
 
Nilijaribu kuishi Tangq mjini pale kwasababu niliipenda mandhari yake lakini nililazimika kurudi nyumbani Dar kwasababu maisha magumu sana pale. Tanga akieleweki mpaka vijana wazawa wa pale hawakai pale. Afadhari mikoa ya nyanda za juu kusini kuliko pwani ile.
 
Kweli ulipaswa kuwa bonge la jiji baada tu ya Dar lakini ndio hivyo serikali yetu huwa hainaga mipango ya kuendeleza miji inaachwa tu ikue hovyo hovyo.
 
Kwa kutusagiร  huko lazima tutakutumia zongo uhangaike nalo.
 
Mkuu hapo kwenye ushirikina ni hulka za baadhi ya watu, na kuhusu maendeleo ya mji hata serikali na viongozi waliopo wanachangia sana kwa kutokuipa kipaumbele Tanga. Na watu wanaridhika mapema sana kiasi kwamba mtu akiwa na uhakika wa kula na kulala haumizi akili yake kabisa! Mjini pale wengi wanaringia majumba ya urithi! Pia kuna fitna na chuki sana kwenye nyanja mbalimbali mfano siasa, michezo n.k
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ