Pre GE2025 Tanga: Rais Samia agawa mitungi ya gesi (LPG) na kuzungumza na wananchi wa Muheza
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Tanga: Rais Samia akigawa mitungi ya gesi (LPG) na kuzungumza na wananchi wa Muheza, Tanga Februari 27, 2025.


Ester Barua ambaye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Magila iliyopo Muheza mkoani Tanga akiwa kwenye kiti cha Rais Samia Suluhu Hassan baada ya Rais kumpisha kutokana na kuvutiwa na wasilisho lake, ambapo alielezea miradi mbalimbali inayotekelezwa nchini na uchapa kazi wa Rais Samia huku akitumia lugha ya Kiingereza.

Snapinst.app_480985581_18464915101068597_2515690432420135814_n_1080.jpg

FB_IMG_1740658190828.jpg

FB_IMG_1740658195598.jpg
Rais Samia Suluhu Hassan anaendelea na ziara yake mkoani Tanga, ambapo leo akiwa katika Uwanja wa CCM Jitegemee wilayani Muheza anagawa mitungi ya gesi (LPG) na kuzungumza na wananchi.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala ya Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Advera Mwijage amesema kuwa Mkoa wa Tanga unatekeleza miradi minne ya kusambaza umeme katika vijiji, miji, vituo vya afya, pampu za maji, maeneo ya migodi pamoja na viwanda vidogo ambayo thamani yake ni shilingi bilioni 137.87.

Amefafanua kuwa vijiji vyote 763 vya Mkoa wa Tanga mpaka sasa vimeshapata umeme kwa asilimia 100, pamoja na vitongoji 2,382 kati ya 4,531sawa na asilimia 52.6, navyo tayari vimewekewa umeme.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza mkoani Tanga, Hamis Mwinjuma (MwanaFA) amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kujenga soko la kitaifa la machungwa wilayani humo akitoa sababu kuwa wilaya hiyo ndio mzalishaji mkubwa wa machungwa nchini.

MwanaFA ameongeza kuwa kuna changamoto kubwa katika ununuzi wa machungwa wilayani Muheza, kwani madalali wengi wamekuwa wakinunua pasipo utaratibu mzuri unaowanufaisha wakulima huku akisema endapo soko hilo litajengwa litadhibiti uporomokaji wa bei na kuwasaidia wakulima katika kuhifadhi mazao yao pamoja na kuwasaidia kuuza kwa bei maalumu na si bei ya kutupa.

Rais Samia Suluhu akizungumza na wananchi wa Muheza

"Nilipomteua Mwana FA na yule Mkuu wangu wa Wilaya ya Kibaha anaitwa Nikki wa Pili watu hawakuelewa [..] lakini kwa faraja kubwa, hawa wananisaida sana."

"Tunataka ifikapo mwaka 2034, asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia nishati safi ya kupikia. Matumizi ya kuni na mkaa yamekuwa na athari kubwa kwa mazingira na afya, hususan kwa wanawake na watoto. Gesi zinazotokana na kuni na mkaa zinasababisha maradhi ya kupumua, macho mekundu na hata vifo vya mapema. Pia, watoto wa kike hupata ujauzito wakiwa safarini kutafuta kuni, jambo linalokatisha ndoto zao za elimu."
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Akigawa Mitungi ya Gesi (LPG) na Kuzungumza na Wananchi wa Wilaya ya Muheza, leo tarehe 27 Februari, 2025.
 

Attachments

  • FB_IMG_1740658186801.jpg
    FB_IMG_1740658186801.jpg
    80.5 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1740658188610.jpg
    FB_IMG_1740658188610.jpg
    70.7 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1740658190828.jpg
    FB_IMG_1740658190828.jpg
    88.6 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1740658193201.jpg
    FB_IMG_1740658193201.jpg
    96.7 KB · Views: 2
  • FB_IMG_1740658195598.jpg
    FB_IMG_1740658195598.jpg
    116.1 KB · Views: 2
Back
Top Bottom