Mkazamoyo
JF-Expert Member
- Sep 3, 2013
- 1,638
- 2,817
Wakati serikali ikiwahimiza wananchi wake kupunguza mikusanyiko na safari zisizo za lazima ikiwa ni pamoja na kuzifunga shule zote na vyuo vyote nchi nzima kwa lengo la kupunguza athari za kusambaa kwa Virusi vya CORONA, imebainika hali ni tofauti huko mkoani Tanga kwani katibu Tawala wa mkoa huo amewaagiza Wakurugenzi wa halmshauri za mkoa huo akiwataka wawataarifu wakuu wa shule na walimu wahudhurie shuleni ili kuendelea na majukumu mengine yasiyohusiana na ufundishaji wakati huu ambapo shule zimefungwa kwa agizo la serikali.
Mojawapo ya majukumu watakayotakiwa kuyatekeleza ni pamoja na "kuhakikisha kuwa mazingira yote ya nje na ndani ya ofisi yanakuwa safi".
Sasa hapa utajiuliza wanafunzi hawapo je hayo mazingira ya nje na ndani nani wa kuyasafisha? Lakini pia nchi hii kuna serikali mbili moja inasema shule stop wanafunzi na walimu wasifike shuleni nyingine inasema walimu wao waendelee kwenda.
Walimu kweli kazi mnayo
Wacha tuendelee na maombi ya kitaifa.
Sent using Jamii Forums mobile app