Sioni tatizo la maelekezo yaliyotolewa kwenye barua hiyo.
Waalimu ofisi yao ni shuleni!!, Wanafunzi ndiyo waliofunga shule, wakati wote na waalimu wanatambua Hilo, shule zinapofungwa katika mazingira ya kawaida ni wanafunzi pekee wanaokuwa likizo huku wakipangiwa tarehe za zamu kwa ajili ya usafi.
Hili janga ni la dharura, lkn halimfanyi Mwl aache kwenda ofisini kwake kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye waraka wa RAS.
Vinginevyo, nurse, hakimu, magereza, ofisi za umma, polisi nk nao pia wabaki nyumbani kisa Corona!! bado hatujafikia hatua hiyo kwa mujibu wa maelekezo ya serikali.
Usafi, hili ni la muhimu sana katika mazingira ya shule zetu hizi za umma ni jukumu sasa la waalimu wakuu/wakuu wa shule , kuandaa bajeti ndogo na kuifikisha kwa RAS kwa ajili ya utekelezaji.
Waalimu wasiachwe wazurure hovyo kutafuta riziki ni wakati wao serikali kuwawekea mazingira Bora ya kazi na motisha kipindi hiki cha upweke kwao.