Tanga: RAS aagiza Walimu waendelee kuhudhuria kazini licha ya agizo la Serikali kuzuia mikusanyiko

Mkazamoyo

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2013
Posts
1,638
Reaction score
2,817
Wakati serikali ikiwahimiza wananchi wake kupunguza mikusanyiko na safari zisizo za lazima ikiwa ni pamoja na kuzifunga shule zote na vyuo vyote nchi nzima kwa lengo la kupunguza athari za kusambaa kwa Virusi vya CORONA, imebainika hali ni tofauti huko mkoani Tanga kwani katibu Tawala wa mkoa huo amewaagiza Wakurugenzi wa halmshauri za mkoa huo akiwataka wawataarifu wakuu wa shule na walimu wahudhurie shuleni ili kuendelea na majukumu mengine yasiyohusiana na ufundishaji wakati huu ambapo shule zimefungwa kwa agizo la serikali.

Mojawapo ya majukumu watakayotakiwa kuyatekeleza ni pamoja na "kuhakikisha kuwa mazingira yote ya nje na ndani ya ofisi yanakuwa safi".

Sasa hapa utajiuliza wanafunzi hawapo je hayo mazingira ya nje na ndani nani wa kuyasafisha? Lakini pia nchi hii kuna serikali mbili moja inasema shule stop wanafunzi na walimu wasifike shuleni nyingine inasema walimu wao waendelee kwenda.

Walimu kweli kazi mnayo

Wacha tuendelee na maombi ya kitaifa.

​

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Amechoka kazi huyu. Subiri mkuu atoke aliko. Utaniambia. Wambea walishapeleka faili lake kunakohusika
 
Ingekuwa vizuri zaidi Wizara ya Elimu ingetoa utaratibu wa kitaifa ili Jambo liwe na uzito kwa walimu wote.

Walimu wa Tanga ni sawa na wa mikoa mingine
 
Wewe mkazamjomba soma barua uielewe! Maelezo yako yanakinzana na barua yenyewe.
 
Acha utetezi wa kipumbavu..
Unataka kutuambia hatuelewi kiswahili !!?
Wewe mkazamjomba soma barua uielewe! Maelezo yako yanakinzana na barua yenyewe.
 
Huu ni ujuha,, unakwenda Sawa halafu ukifika unafanya nini?.. kupiga story au?.. tuna dizaini ya viongozi WA ajabu ajabu halafu tume pose tunasubiri tz ya viwanda via mburulazi hawa gademit
 
Kufagia.... Sasa sijui Walimu wana immune ya Corona au la... Ujuha kabisa...
Huu ni ujuha,, unakwenda Sawa halafu ukifika unafanya nini?.. kupiga story au?.. tuna dizaini ya viongozi WA ajabu ajabu halafu tume pose tunasubiri tz ya viwanda via mburulazi hawa gademit
 
Huyo katibu tawala nae ni mapuuza tu, kwahiyo walimu wakafagie huko mashuleni?
 
Huu ni ujuha,, unakwenda Sawa halafu ukifika unafanya nini?.. kupiga story au?.. tuna dizaini ya viongozi WA ajabu ajabu halafu tume pose tunasubiri tz ya viwanda via mburulazi hawa gademit

Maelekezo ya barua yapo vizuri labda hatuisomi vizuri au tunataka kuitafsiri tunavyotaka sisi.
 
Mkazamoyo,
Kwani wanafunxi ndio kazi yao usafi wa shule si huwa ni msaada tu. Walimu waende wakafanye mbinu shule zao ziwe safi au kwa kuwapa watu vibarua au kwa kusafisha wao wenyewe.

Jamani hata usafiq wa sehemu zao za kazi mpaka aseme Waziri Mkuu au Rais?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…