Tanga: RAS aagiza Walimu waendelee kuhudhuria kazini licha ya agizo la Serikali kuzuia mikusanyiko

Huu ni ujuha,, unakwenda Sawa halafu ukifika unafanya nini?.. kupiga story au?.. tuna dizaini ya viongozi WA ajabu ajabu halafu tume pose tunasubiri tz ya viwanda via mburulazi hawa gademit
Ni kutafuta sifa za kingese tu sasa kwa hali hii hiyo F unaiondoa kwa sanitaiza au kitu gani?Mheshimiwa ras utulie sio unakurupuka tu kutia watu taharuki Ndio nyie Mh waziri mkuu alisema tuwapuuze Nchi inajitahidi kupambana we unaibuka na maono yako ya kwenye boha
 
Kiswahili huwa nasoma mara moja tu. We kilaza endelea rudiarudia. Amka uwahi shule ukafagie class area.
Naenda tukutane huko shule! Hakuna pahala barua inasema walimu waende shule isipokuwa Mwalimu wa zamu. Kwanini? Shule haziiafungwa na hata zingekuwa zimefungwa, Ofisi za shule hufungwa siku kuu na jumamosi na jumapili tu.

Mfanyakazi yeyote hatakiwi kuwa nje ya Makazi yake isipokuwa kwa ruhusa ya kiongozi wake. Kuhakikisha Usafi unafanyika ni jukumu la uongozi wa shule (siamini wanaofagia hata wakati wa likizo ni walimu).

Dogo walimu walokuwa wanafundisha masomo yaliyotajwa 2019 wamekumbusha kufanya upembuzi (analysis) na waweza kuzifanyia majumbani mwao. Acha kijana mihemko ya kitoto, soma barua ukiwa ‘sober’
 
Asilaumiwe RAS.
Maana ni kawaida shule zikifungwa,walimu kuendelea kwenda kazini hadi aombe likizo.

Sasa kwa suala hili,waziri husika alipaswa kutoa mwongozo wa nini kifanyike kwa walimu na watumishi wengine wa taasisi hizi.Kama hakuna maelekezo yoyote,RAS ana wajibu wa kuhakikisha watumishi wanawajibika kama kawaida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani wanafunxi ndio kazi yao usafi wa shule si huwa ni msaada tu. Walimu waende wakafanye mbinu shule zao ziwe safi au kwa kuwapa watu vibarua au kwa kusafisha wao wenyewe.

Jamani hata usafiq wa sehemu zao za kazi mpaka aseme Waziri Mkuu au Rais?
NATAMANI KUTOA TUSI, LAKINI............
 
Ingekuwa vizuri zaidi wizara ya elimu ingetoa utaratibu wa kitaifa ili Jambo liwe na uzito kwa walimu wote.

Walimu wa Tanga ni sawa na wa mikoa mingine

Mkuu jambo hili ni dogo sana kwani walimu wanauwezo wa kufanya kazi wakiwa nyumbani 100% na kisiharibike kitu, nikupe mfano mmoja wa ubalozi hapa Tanzania, wao wameambiwa wafanye kazi wakiwa nyumbani

lakini kila siku kuna watu watatu tu wanafika kazini ambao ofisi zao zipo mbalimbali na wanapokezana zamu kila siku na kazi zinaenda kama kawaida ......tatizo linakuja hapa kwenye ngozi nyeusi sijui tumelaaniwa kushindwa hata kujipanga hivyo ili tupunguze maambukizi?
 
Huyo RAS kwanza niseme ni incompitent.. Au kapotoshwa au hajui majukumu yake. Vyeo vya kupeana kindugu.

Anataka kutuambia kwamba Mkoa wa Tanga Walimu bado hawajafanya analysis ya matokeo ya 2019!!!

Jamani walimu wa Tanga is this true.!? Watu analysis ilishafanyika na utendaji wake upo in place muda mrefuu.

Incompitent RAS. Sitashangaa Tanga ikiendelea buruza mkia.
 
Nilipokuwa mdogo nilikuwa na mawazo mfu sana. Nilifikiri mpaka mtu awe kiongozi nilazima awe smart sana hasa kichwani na mwenye busara ya hali ya juu. Sasa kumbe maskini fikira zangu zilikuwa tofauti kabisa na uhalisia.

Kumbe bila kujua hata yule bongo lala darasani yaani yule zero bran anaweza kuwa kiongozi tena mkubwa tu ilimradi tu anae mtu juu anaemshika mkono au ushawishi wa pesa

Na matokeo yake ndo haya sasa. Huyu anafanya hivi si kwamba anauchungu sana elimu bali anaona ni moja ya njia ya kumfurahisha bwana wake aliemweka hapo kuwa anafanya kazi kwelikweli.

Poor my Country
 
Tatizo watoa maelekezo wanajichanganya sana.
Aliyesitisha masomo alitoa maelekezo na yaka fuatwa.Kama kuna mabadiliko nayo yatolewe kiufasaha yatafatwa, hakuna tatizo kama inatakikana walimu wawepo kwenye vituo vyao vya kazi.

Tatizo linakuja maelekezo yanayotolewa saa hizi hayako realistic.Kufanya analysis saa hizi wakati ilishafanyika na ilikuwa kwenye utekelezaji kabla ya janga.Hilo la kufanya usafi linawezekana,na wala halishindikani.

Swala ni mlundikano wa watu sehemu moja ndio tatizo hapo.Mbona tunapoteana Watanzania?
Ngoja tumalize maombi ya siku tatu
 
Bora walimu wangezunguka mtaani kutoa elimu ya corona na njia za kujikinga,,,,,maoni yangu tu...
 
Hakukua na document mkuu sasa ndio nimeelewa kwamba mlete mada hataki kufanya kazi
Wakati mwingine huwa nawapenda ladies wapo sober na sincere! Lakini wavulana mh! Unajua kuna sheria ya kazi hapa Tanzania ambayo usipofika kazini siku 5 mfululizo unakuwa umejifukuza kazi, na serikali haikusema mashule yafungwe, hivyo at any time t, mwajiri anaweza kumwita Mfanyakazi yeyote kutoka majumbani kwa kazi maalum.

Imagine wewe kila siku unakuwa mtu wa mihemko kazini na umejichukulia madaraka ya kutoka katika Kituo chako cha kazi upo mbali na siku tano zaidi napita, si kibarua kinaota nyasi? Aidha hata ukiwa likizo kutoka mkoa mmoja hadi mwingine lazima uombe kibali kwa mwajiri. Tunadharau haya mambo lakini likikufika utaumia.
 
Wanafunxi[emoji808] Wanafuzi[emoji818]

Kwani wanafunxi ndio kazi yao usafi wa shule si huwa ni msaada tu. Walimu waende wakafanye mbinu shule zao ziwe safi au kwa kuwapa watu vibarua au kwa kusafisha wao wenyewe.

Jamani hata usafiq wa sehemu zao za kazi mpaka aseme Waziri Mkuu au Rais?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuliambiwa tutapata all information through 3 Person especial this hard time of fighting with CORONA,Tukatangaziwa mashule hadi Vyuo vikuu vimefungwa hakuna kuhudhuria sio WALIMU wala wanafunzi means haitakiwi misongamano.

Lakini cha ajabu huyu RAS wa Mkoa wa Tanga kaagiza Walimu wote waende mashuleni kwa kisingizio cha kuweka mazingira sana,ofisi ziwe safi maeneo yote ya shule yawe safi sasa hapa anataka WALIMU wafagie maeneo hayo na kupiga deki ofisi na kufuta mavumbi au?

Je, hapo kutakuwa na mkusanyiko au hakuna hivi kwa nini kila mtu anataka kujiona ni zaidi ya mwingine mie naona RAS ni mtu mdogo sana lakini cha ajabu kwa kuwa anajiona ana sharubu kama KAMBARE ndio maana ameamua kufungua mashule kiania ati anapiga kazi lol.

Sasa tuwasikie Rais wa nchi hii,Waziri mkuu wa nchi hii na Waziri wa afya au RAS na AFISA ELIMU WA MKOA WA TANGA au? HAWA WATU WAWILI NI WA KUTUMBUA MAPEMA SANA HAWAFAI YAANI TANZANIA NZIMA MASHULE YOTE NA VYUO VIMEFUNGWA ATI TANGA TU NDIO WALIMU WAENDE KAZINI KAMA KAWAIDA this is IDIOT IDEA
 
Labda anaandaa mijengo ya kuja kuhifadhi wagonjwa wa covid😜
Mfate ofisini umuulize.
 
Sioni tatizo la maelekezo yaliyotolewa kwenye barua hiyo.

Waalimu ofisi yao ni shuleni!!, Wanafunzi ndiyo waliofunga shule, wakati wote na waalimu wanatambua Hilo, shule zinapofungwa katika mazingira ya kawaida ni wanafunzi pekee wanaokuwa likizo huku wakipangiwa tarehe za zamu kwa ajili ya usafi.

Hili janga ni la dharura, lkn halimfanyi Mwl aache kwenda ofisini kwake kutekeleza majukumu yake kama yalivyoainishwa kwenye waraka wa RAS.

Vinginevyo, nurse, hakimu, magereza, ofisi za umma, polisi nk nao pia wabaki nyumbani kisa Corona!! bado hatujafikia hatua hiyo kwa mujibu wa maelekezo ya serikali.

Usafi, hili ni la muhimu sana katika mazingira ya shule zetu hizi za umma ni jukumu sasa la waalimu wakuu/wakuu wa shule , kuandaa bajeti ndogo na kuifikisha kwa RAS kwa ajili ya utekelezaji.

Waalimu wasiachwe wazurure hovyo kutafuta riziki ni wakati wao serikali kuwawekea mazingira Bora ya kazi na motisha kipindi hiki cha upweke kwao.
 
Sijui kalogwa huyu mtu mwenye cheo cha RAS? Real he' an Idiot.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…