Tanga: Watu watano mbaroni kwa kuzua taharuki kuibiwa Nyeti

Tanga: Watu watano mbaroni kwa kuzua taharuki kuibiwa Nyeti

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linawashikilia watu watano kwa tuhuma za kumshambulia na kumjeruhi mtu pamoja na kuzua taharuki katika jamii kufuatia matukio mawili tofauti yaliyotokea katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo.

Akizungumzia matukio hayo, Jeshi la Polisi lilieleza kuwa tukio la kwanza lilitokea Aprili 5, 2026 majira ya saa 2:00 usiku katika Bar ya Kivuga Point iliyopo Kijiji cha Mazingara, Kata ya Mkata, Tarafa ya Mazingara, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Katika tukio hilo, Santiel John, mkazi wa Mazingara, alishambuliwa kwa kupigwa ngumi na mateke sehemu mbalimbali za mwili wake na watu wawili wanaotajwa kuwa ni Vado Mchungu, mkazi wa Suwa, pamoja na Fadhili Nuru, ambaye pia ni mkazi wa Suwa.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha shambulio hilo ni madai ya uongo yaliyoenezwa na mtuhumiwa Fadhili Nuru aliyedai kuwa amepoteza uume wake huku akimtuhumu Santiel John kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo, uchunguzi wa haraka uliofanywa na Jeshi la Polisi ulibaini kuwa madai hayo hayakuwa ya kweli na mhusika alikutwa akiwa salama.

Mtu aliyejeruhiwa alipatiwa rufaa na kupelekwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kwa ajili ya matibabu, huku watuhumiwa wote wawili wakiwa wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi kwa ajili ya mahojiano zaidi wakati taratibu za kuwafikisha mahakamani zikiendelea.

Katika tukio la pili lililotokea Aprili 6, 2026 majira ya saa 12:30 jioni katika eneo la Mabanda ya Papa, Tarafa ya Mabawa, Kata ya Ngamiani ndani ya Jiji la Tanga, watu watatu walikamatwa wakiwa ndani ya gari la usafiri wa umma aina ya Hiace baada ya kuzua taharuki kwa kumtuhumu abiria mwenzao kuwa amewaondolea sehemu zao za siri.

Watuhumiwa waliokamatwa ni Haji Mbwana, Mbwana Mluku na Amiri Rashid, wote wakazi wa maeneo husika.

Jeshi la Polisi limesema watuhumiwa hao wamefikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bombo mkoani Tanga kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu, na mara uchunguzi utakapokamilika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.



Chanzo: Wasafi
 
Kama Kuwa na Busha ni moja ya Heshima na fahari kubwa huko Tanga ...kuibiwa nyeti itakuwa Shambulio la kigaidi kabisa.
 
Nadhani yule kamanda aliyesema ni kweli nyeti zinaibiwa na hurudi taratibu taratibu atakaeibiwa asiwe na wasi atawajibishwa pia!

Nchi ya hovyo kabisa hii and by the way,jana kuna huyo mmoja hapa mtaani aliibiwa zake inch nne akarudishiwa inch tisa!
 
Back
Top Bottom