Tanga: Watu watatu wafariki dunia kwa kuchomwa moto ndani ya gari Handeni

Black Butterfly

Senior Member
Joined
Aug 31, 2022
Posts
130
Reaction score
368
Watu watatu wamekutwa wamefariki dunia kwa kuchomwa moto na watu wasiojulikana eneo la msitu wa Hifadhi ya Korogwe Fuel, uliopo Kijiji cha Sindeni wilayani Handeni mkoani Tanga.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 24, 2024 kuhusu tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema tukio hilo limetokea jana Septemba 23, saa tatu usiku.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kuwatafuta wahusika.

Kamanda amesema walipokea taarifa ndani ya msitu huo kuna gari ndogo inaungua moto na pembeni yake kuna watu wawili wanaungua.

Kamanda amesema askari polisi walifika eneo hilo na kukuta kuna gari ndogo linaungua moto na pembeni yake kukiwa na watu wawill wameungua kwa moto na kufariki dunia wakiwa pembeni ya gari hilo.

Mchunguzi amesema baada ya uchunguzi wa awali ilibainika miili iliyokuwa nje ya gari ni ya jinsia ya kike na ndani ya gari kiti cha nyuma ulionekana mwili mwingine ambao umeungua moto hadi kupoteza sura na haijabainika ni wa jinsia gani.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa kushirikisha na vyombo vingine vya uchunguzi kubaini walioteketea kwa moto ni kina nani, nini kiliwatokea kabla ya umauti na waliofanya tukio hilo ni watu gani ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani.

Amesema miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Handeni, kwa ajili ya uchunguzi.

Kamanda Mchunguzi ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa zitakazosaidia kukamilisha uchunguzi wa tukio hilo.

Msitu wa Korogwe Fuel unamilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Handeni.

MWANANCHI
 
Watu watatu wamefariki dunia baada ya kuungua moto katika eneo la ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Korogwe Fuel katika Kijiji cha Sindeni wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema Septemba 23, 2024 majira ya saa 03:45 usiku walipokea taarifa kwamba ndani ya msitu huo kuna watu wameungua moto.

"Askari Polisi walifika eneo hilo na kukuta kweli kuna gari aina ya IST lenye namba T T 305 EAL linaungua moto na pambeni yake kukiwa na watu wawili wameungua kwa moto".amesema Kamanda Mchunguzi

Soma pia: Jeshi la Polisi lawashikilia watu watatu akiwemo mtoto anayedaiwa kuiba watoto sita

Ameongeza baada ya uchunguzi wa awali wa miili iliyokuwa nje ya gari ilibainika ni ya jinsia ya kike na ndani ya gari kiti cha nyuma ulionekana mwili mwingine ambao umeuungua moto hadi kupoteza sura na haujabainika ni wa jinsia gani.

Miili ya watu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Handeni huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi ili kubaini watu hao walioteketea kwa moto ni akina nani , na nini kiliwatokea kabla ya umauti na waliofanya tukio hilo ni watu gani ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Source: TBC Online
 
Yani miili imeteketea kwa moto pembeni ya gari? Mbona haiingii akilini?

Kwamba hao watu walisimama pembeni ya gari linalowaka moto hadi wakateketea?
Huyo aliyetekea ndani ya gari naweza kuelewa.

Anyways, wapumzike kwa amani.
 
Siyo Wanachama wa CHADEMA kweli hao na labda Jana walikuwa katika Maandamano wakashikwa na leo kama Kawaida?
 
Yani miili imeteketea kwa moto pembeni ya gari? Mbona haiingii akilini?

Kwamba hao watu walisimama pembeni ya gari linalowaka moto hadi wakateketea?
Huyo aliyetekea ndani ya gari naweza kuelewa.

Anyways, wapumzike kwa amani.
Walitoka nje ya gari inamaana hyo wakiwa tayari wameshika moto. Reason hata kidgo basi.
 
Yani miili imeteketea kwa moto pembeni ya gari? Mbona haiingii akilini?

Kwamba hao watu walisimama pembeni ya gari linalowaka moto hadi wakateketea?
Sahivi tz watu wanafanyiana umafia tu,sahv mtu akikuambia anakupoteza anakupoteza kweli
Mmedhulumiana,mmechukuliana mke au mme watu wanafanyiana
Yajayo yanafurahisha,muanze kuishi kwa kuzoea mambo haya sasa Tlaatlaah

Ova
 
Back
Top Bottom