Tanga: Watu watatu wafariki dunia kwa kuchomwa moto ndani ya gari Handeni

Tanga: Watu watatu wafariki dunia kwa kuchomwa moto ndani ya gari Handeni

Watu watatu wamefariki dunia baada ya kuungua moto katika eneo la ndani ya Msitu wa Hifadhi ya Korogwe Fuel katika Kijiji cha Sindeni wilayani Handeni Mkoa wa Tanga.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi amesema Septemba 23, 2024 majira ya saa 03:45 usiku walipokea taarifa kwamba ndani ya msitu huo kuna watu wameungua moto.

"Askari Polisi walifika eneo hilo na kukuta kweli kuna gari aina ya IST lenye namba T T 305 EAL linaungua moto na pambeni yake kukiwa na watu wawili wameungua kwa moto".amesema Kamanda Mchunguzi

Soma pia: Jeshi la Polisi lawashikilia watu watatu akiwemo mtoto anayedaiwa kuiba watoto sita

Ameongeza baada ya uchunguzi wa awali wa miili iliyokuwa nje ya gari ilibainika ni ya jinsia ya kike na ndani ya gari kiti cha nyuma ulionekana mwili mwingine ambao umeuungua moto hadi kupoteza sura na haujabainika ni wa jinsia gani.

Miili ya watu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Handeni huku Jeshi la Polisi likiendelea na uchunguzi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya uchunguzi ili kubaini watu hao walioteketea kwa moto ni akina nani , na nini kiliwatokea kabla ya umauti na waliofanya tukio hilo ni watu gani ili waweze kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Source: TBC Online
Yani miili miwili ikutwe nje na mmoja ukutwe ndani tena siti ya nyuma!?
Haya ni mauaji yamefanyika kabisa.
Typically killing.
 
Sahivi tz watu wanafanyiana umafia tu,sahv mtu akikuambia anakupoteza anakupoteza kweli
Mmedhulumiana,mmechukuliana mke au mme watu wanafanyiana
Yajayo yanafurahisha,muanze kuishi kwa kuzoea mambo haya sasa Tlaatlaah

Ova
ofcourse ni muhimu sana kuheshimiana kwenye ndoa,
lakini pia ni ustaarabu kutodhulumiana fedha, mali au hata uongozi kwa tamaa binfsi...

kuna watu hawawezi kuvumilia hali hiyo, wala hawawezi kuongea neno kujibizana mwizi wa mke wake au mdhulumati wa fedha kwa maneno, wao hujibu kwa matendo tu.

unaweza kumdhulumu fedha, mke au mali, nae baada ya muda ukijisahau, akakudhulumu uhai wako. Tuishi kistaarabu.

Pole sana waliopoteza wazazi, ndugu, jamaa na marafiki kwenye tukio hili baya sana.. :NoGodNo:
 
Yajayo yatazidi kufurahisha
Ila elewa,sahv mtu akikuambia
Ntakupoteza ujue anakupoteza kweli syo masiharaa

Ova
 
Yajayo yatazidi kufurahisha
Ila elewa,sahv mtu akikuambia
Ntakupoteza ujue anakupoteza kweli syo masiharaa

Ova
hiyo sifahamu na sina hakika mrangi,

ila kuheshimiana ni jambo la kistaarabu mno hasa tunapochangamana miongoni mwa jamii zinazotuzunguka 🐒
 
Back
Top Bottom