TANGA: Watumishi wabainika kuongeza idadi ya Wagonjwa wa VVU ili kunufaika na Fedha za AMREF

TANGA: Watumishi wabainika kuongeza idadi ya Wagonjwa wa VVU ili kunufaika na Fedha za AMREF

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Watumishi wa afya katika wilaya ya Muheza waliohusika kusajili wagonjwa hewa 313 wa virusi vya Ukimwi (VVU) ili kuonyesha takwimu zipo juu za wanaoishi na VVU kwa maslahi yao binafsi ikiwemo kujinufaisha na fedha zinazotolewa na shirika la afya la AMREF.

Awali akitoa taarifa kwa waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa TAKUKURU mkoa Tanga Zainabu Bakari, amesema walibaini udanganyifu huo baada ya uchunguzi na kugundua watoa huduma za afya wilayani Muheza wanahusika na kusajili majina hewa ya wagonjwa wa Virusi vya Ukimwi ili kuzidisha takwimu za ugonjwa huo kwa maslahi yao binafsi.

Alisema wahudumu wa afya wanaohusika na zoezi la kusajili na kuwafuatilia watu wanaoishi na VVU wilayani humo, wamekuwa wakilipwa posho ya gharama ya usafiri na mawasiliano kiasi cha sh. 20,000 kwa siku kila wanapowatembelea wagonjwa hao.

Aidha amesema idadi hiyo ya wagonjwa iliondolewa kwenye mifumo na wahusika waliohusika na usajili wa wagonjwa hewa walipewa barua na kujieleza kwa kitendo cha kusajili wagonjwa hewa ambapo Wizara ya Afya imetoa maelekezo ya kufanya uhakiki kwa wateja wanaotumia dawa ambao sio halisi.

Chanzo: EATV
 
Kwani lini bongo upigaji uliisha?
Au ndiyo maana wahusika wanajitahidi wagonjwa wa Covic-19 wawe wengi? Hivi vitu hewa vimerudi kwa kasi ya mwanga. Rasilimali za Bongo zimeanza tena kupigika kama ngoma.
 
Hii ni TAKUKURU ya nchi gani? Canada.

Mchezo wa kupika data unaofanywa na NGO za hapa Tanzania ni WA kutisha! Wakifukua chanjo za covid-19, uzazi wa mpango watazimia, nimesema hii ni TAKUKURU ya Canada kwa maana serikali yenyewe wanapika data kuwafurahisha wafadhili na hao hao watumishi wa afya ndio wanaotumika.

EATV achana na maigizo hayo, kupika takwimu hapa Tanzania ni halali na hata sensa upo ushahudi makarani walipika hasa!
 
Yaani hakuna watu wabaya kama waizi masikini.

Wanaiba na hawanufaiki na hela hizo zaidi ya kula na kuhonga.

Wazungu wanasaidia sana na waanajua hela au misaada haiwafikii walengwa zote

Kila taasisi wwnaiba tu maana njaa zao hawa watu mpaka chakula cha misaada wanaiba na kuuza.

Wakimbizi mpaka wagonjwa ni kupigwa tu.
 
fikiria kwenye level ya taifa wameongezwa wangapi?
 
Back
Top Bottom