TANGA: Watumishi wabainika kuongeza idadi ya Wagonjwa wa VVU ili kunufaika na Fedha za AMREF

Yanarudi yale yale ya Covid-19,kwahiyo kumbe kuna michezo ya kupikwa takwimu ili muonekane wagonjwa wengi,watu wapige hela.
Siku ukisikia idadi ya watu waliochanjwa chanjo za uviko kuanzia Sept, Oct na Novemba mwaka huu utazimia...hii ndio Tanzania iliyofunguliwa!

Jiwe alikuwa sahihi kuzuia baadhi ya NGO hapa nchini. iCap, Marie Stopes, nk wanachokifanya hapa Kanda ya ziwa Mungu anawaona!

Ona sasa watumishi wameamua kupika takwimu za waathirika kisa 20,000/= kwa siku, huku WHO inatuweka kwenye "nchi zenye wahonjwa wengi wa ukimwi" Kisha Madelu anaenda kukopa pesa za "kuongeza kasi ya mapambano dhidi ya ukimwi" na kununua ma vx V8!
 
Hii ni TAKUKURU ya nchi gani? Canada....
Mchezo wa kupika data unaofanywa na NGO za hapa Tanzania ni WA kutisha! Wakifukua chanjo za covid-19, uzazi wa mpango watazimia...
Walipika kikaiva, au siyo?
 
takwimu ni kitu sensitive sana aisee. hawa wachukuliwe hatua kali kabisa . unakosa uadilifu na kukiuka maadili kwa kiwango hicho... hapana
 
Nataka Kujua, Je zaidi Yaa ARV kuna kingine waathirika wa HIV wananufaika na Fedha za Amref?
 
Ukijumlisha hata sensa unapata jibu jingine.Hapo hujaingia kwenye MATUMIZI ya mikopo ya fedha za nje
 
Shida ni kutoa Posho kwa kazi ambazo ni wajibu wa Mhusika,
 
Wanajifunza kutoka kwa baba yao CCM anavyoiba na kufoji hesabu za kura wakati wa uchaguzi.
 
Hiyo nikwasbabu hii miradi inatumia pesa nyingi kutaka data io inasababisha watu kupika data
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…