Tanganyika haikuwahi kukaliwa na watu

Tanganyika haikuwahi kukaliwa na watu

Jamani thread hii inasikitisha. Kwa bahati mbaya mleta mada hana habari za historia alileta kitu alichosikia sijui wapi? Wako 2,3 wanaokumbuka kidogo habari halisi (kama Kilwa kutembelewa na Ibn Battuta mnamo mwaka 1300 BK). Lkn wengi wanaelea hewani kabisa!
Olduvai (iko Tanzania!) hawakuwa binadamu kama sisi, ni hatua ya nyuma zaidi katika kutokea kwa homo sapiens.
Lakini je, Isimila - Iringa haijulikani? Hapa karahana kubwa ya zana za mawe na mifupa ya kibinadamu ilipimwa kuwa na umri wa miaka 260,000. Ilhali zana za mawe zilitengenezwa kibiashara maana yake,, wakati ule walikuwepo tayari watu ambao a) walichonga zana hizi, b) walizibeba penginepo kwa biashara na c) waliokuwa tayari "kuzinunua" (hawakuwa na pesa, lakini kwa njia ya biashara ya mali kwa mali.

Eneo la Tanganyika (si Tanganyika yenyewe, maana ilianzishwa tu kama nchi-koloni mnamo 1919/20) lilikuwa na watu tangu miaka mielfu. Usijali makabila - maana makabila yalitokea na kupotea na kuundwa upya mara kwa mara. Miaka 200 si historia ndefu.

BTW: Tabora ilianzishwa katika karne ya 19, labda kuanzia 1840/50, tena na wafanyabiashara Waswahili na Waarabu kwenye nia kwenda Ziwa Tanganyika. Wajerumani waliwakuta.

Jamani someni vitabu! Msitumie pesa yote kwa pombe, soda, kuku na chipsi (zitakazokupa kisukari tu). Acha mlo ukanunue kitabu! Historia ya Tanzania iko dukani.
Angalau soma makala za historia katika Wikipedia! (nimeweka viunganishi pale juu)
 
Tanganyika takribani karne 4 zilizopita haikuwa na mwenyewe, haikukalika and was purely a virgin land same goes to Namibia (South West Africa) and Cameroon.

The secret behind this ni sababu ya Tanganyika "at that time" ilikuwa ni msitu, maziwa na vito. Pia Cameroon ilikuwa hivyo hivyo while Namibia ikiwa jangwa.

Taratibu watu walianza kujisogeza karne 2 ziliyopita hadi kufika Tanganyika at that time ikiwa na territory ya Rwanda-Urundi watu wengi walitokea Kaskazini Magharibi na Southern Part (Rhodesia) huku Eastern part walitokea Arabian Peninsula na visiwa vya bahari ya Hindi na India pia.

Hadi ujio wa Germany, Tanzania ilikuwa na wahamiaji na watu wachache sana walioloea maeneo ya Southern Part's, North Eastern Part na Northern Western Part nikimaanisha maeneo yanayotambulika kwa sasa kama Tanga, Mbeya, Coast and Sanzibar pia Rwanda na Burundi.

Tactically Tabora ni mji uliotengenezwa at the time na Germany. Huku walowezi waliendelea hadi Walvis Bay, Rehoboth na hadi kufika Windhoek, Namibia. Same kwa Cameroon wali-emerge maeneo ya Adjou.

Ukihitaji kufahamu hili haitaji kuwa PhD holder bali jiulize Tanganyika, Rwanda-Urundi na Sanzibar 1961 ilikuwa na wakazi takribani Million 8.9

Tanganyika (Tanzania) haina wenyewe hii inatokana na tafiti yangu kuonesha maajabu ya watu wa Tanzania kuwa different in type niseme tu ni Spices za watu tofauti.

Utaweza kuona Nigeria ikiwa na watu Million 54 while Southern Africa ikiwa na watu Million 34 back in the days. Utaona Eastern Side haikuwa na watu kabisa.

Karibu,
Karne nne zilizopita, thats 400 years ago!
Mkuu kweli elimu yako ya kata na ya siku hizi imeshuka sana,
Kwa hiyo michoro ya kwenye miamba huko Kondoa Irangi na mifupa ya Olduvai Gorge yenye miaka mamilioni ni hadithi za kutungwa?
Alafu unweza kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa mbunge, tutakuwa tumekwisha!
 
Hoja kuu ni hii, zaidi ya 90% ya makabila yaliopo sasa Tanganyika haykuepo zaidi ya miaka 400 nyuma na huo nii uhalisia. Kila mtu alifanyie research kabila lake atapata jibu.

Kuhusu kuwa kuna reference za ki science za miaka zaidi ya elfu nyuma kuwa kulikua na watu hilo linawezekana. kwamba walikuepo watu na baadae wakaondoka kwani hayo yalikua ndio maisha ya zama hizo hasa africa yakua kukaa sehemu baadae wakahama nakuhamia maeneo mengine.
 
Mkuu unaongelea historia iliyoandikwa na mzungu mbayo wewe ndio mejikita nayo.
Prehistoric Tanganika ilikuwepo na watu walikuwepo ingawaje si kwa mipaka hii tunayoiona.
Uthibitisho wa kuwepo wtanganyika wa miaka zaidi ya milioni 2 nyuma ni kam ilivyogunguliwa mifupa ya watu wa kale huko Olduvai Gorge kama nilivyosema.
Vile vile rock paintings za Kondoa Irangi.
1585220014336.png

Michoro hii imekisiwa kuwepo zaidi ya miaka 2000 hadi 50,000 iliyopita.
Unahitaji uthibitisho gani zaidi ya huu kuwa tupo na tulikuwepo?
 
View attachment 1399885
Michoro hii imekisiwa kuwepo zaidi ya miaka 2000 hadi 50,000 iliyopita.
Unahitaji uthibitisho gani zaidi ya huu kuwa tupo na tulikuwepo?

mkuu naona hujanielewa, na zaidi unapinga historia ya mzungu wakati hicho unachokisimamia pia kinatokana na mzungu.

Sipingi kama hakukua na watu katika eneo la Tanganyika hizo zama unazozitaja, ila hoja yangu ni kuwa sisi watanzania wa leo hatuna mahusiano yoyote ya hao wa miaka elfu 5 nyuma, kwasababu zaidi ya 90% ya makabila yetu hayakuepo katika eneo la Tanganyika miaka 400 nyuma.
 
Karne nne zilizopita, thats 400 years ago!
Mkuu kweli elimu yako ya kata na ya siku hizi imeshuka sana,
Kwa hiyo michoro ya kwenye miamba huko Kondoa Irangi na mifupa ya Olduvai Gorge yenye miaka mamilioni ni hadithi za kutungwa?
Alafu unweza kuteuliwa au kuchaguliwa kuwa mbunge, tutakuwa tumekwisha!
Naendelea kutia machozi. Bwana, miaka milioni? Anachosema huyu mleta mada si kweli, lakini akisema "Tanganyika hakuna watu miaka 400 iliyopita" si kweli lakini anafikia ukweli zaidi kuliko wewe ukisema eti michoro ya Kondoa Irangi ni miaka mamilioni!
Hakuna anayejua kuhesabu miaka katika uwanja huu???
 
Michoro ya Kondoa Irangi ni miaka karibia 2000, wakati mifupa ya Oduvai Gorge ni miaka milioni 1.5 hadi 2,5 iliyopita.
Google habari hiyo mwenyewe.
 
Michoro ya Kondoa Irangi ni miaka karibia 2000, wakati mifupa ya Oduvai Gorge ni miaka milioni 1.5 hadi 2,5 iliyopita.
Google habari hiyo mwenyewe.
Hivi sawa, lakini uliunganisha yote katika sentensi moja na kutaja miaka milioni. Tena Olduvai hawakuwa Homo sapiens. Hakuna uthibitisho kwamba hao walioacha nyayo walikuwa mababu zetu.
 
Back
Top Bottom