Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Mkuu, ndivyo ilivyokuwa? Mbona hatukufundishwa hayo mashuleni?

Lakini wewe unayaonaje hayo mapinduzi, yalikuwa Mapinduzi Tukufu kweli au Mauaji Katili?

Nani aliyekuwa katika njia sahihi? Nyerere kumsaidia mpindua Serikali halali au Mwingereza aliyetaka kuirejesha madarakani Serikali iliyopinduliwa?
 
Viongozi kutoka Zanzibar hata rais wa Zanzibar ndio wanaojua madhara ya kuvunja muungano, hao wengine wanajisemea tu. Zanzibar haijaweza bado kujitegemea kifedha siku wakiweza muungano utavunjika hapo hapo!
Inavyoonekana, ni Tanganyika ndiyo inayoung'ang'ania Muungano! Unataka kusema Tanganyika inawapenda sana Wazanzibar hivyo imeamua kuendelea kuwasiaida hata kama hawana shukrani?
 
Umwambie Samia na Mbarawa na mawaziri wa Zanzibar waliopo serikali ya muungano kwamba muungano uvunjwe sasa hawatakubali ila baada ya wao kustaafu tena shingo upande manake wana mali nyingi bara.
Kwani hapana wasomali wenye mali nyingi bara? Tumeungana nao? Wahindi wangapi wanamiliki mali nyingi sana hapa Tanganyika, hadi bank of India, tumeungana nao?

Wapo wazungu wanamiliki mahoteli kadhaa hapa bongo, tumeungana nao?

Kumiliki mali sio lazima muungano.
 
Inavyoonekana, ni Tanganyika ndiyo inayoung'ang'ania Muungano! Unataka kusema Tanganyika inawapenda sana Wazanzibar hivyo imeamua kuendelea kuwasiaida hata kama hawana shukrani?
Tanganyika hatuna la kupoteza muungano ukivunjika ila Zanzibar watapoteza bajeti, nafasi tele za uteuzi, biashara, ajira nyingi, na mali nyingi ikiwemo ardhi wanazomiliki huku bara.
 
Ukiacha hizo semekana zako, wewe mwenyewe unadhani ukweli upoje kwa kutazama tu hali ilivyo, ni nani mnufaika mkubwa wa Muungano
 
Na kuna Watanganyika wenye majumba na Mali zinginezo nje ya mipaka ya Tanganyika - Zanzibar, South Africa, Dubai n.k.
 
Tanganyika hatuna la kupoteza muungano ukivunjika ila Zanzibar watapoteza bajeti, nafasi tele za uteuzi, biashara, ajira nyingi, na mali nyingi ikiwemo ardhi wanazomiliki huku bara.
Kwa nini Tanganyika haitaki kuwarejeshea uhuru wao?
 
Inasemekana, Wazanzibar wanatamani kuwa huru, hata leo ikiwezekana. Tatizo ni Tanganyika ndiyo haitaki kuwatejeshea uhuru wao!
Kuwapa uhuru wao!?? Ambaye hana uhuru si huwa anaudai au kuupigania? Waliwahi kuudai?

Zanzibar wakiambiwa wajitegemee, hata mwaka hauiishi, wataanza kutaka mwungano uvunjike. Lakini kwa sasa, wakati huu wanaoutunzwa na bara, hawawezi kuthubutu kutaka mwungano uvunjike.
 
Ukiacha hizo semekana zako, wewe mwenyewe unadhani ukweli upoje kwa kutazama tu hali ilivyo, ni nani mnufaika mkubwa wa Muungano
Mnufaika Namba moja ni watawala wa Tanganyika na Zanzibar.

Mnufaika Namba mbili ni nchi ya Zanzibar.

Mnufaika namba tatu ni wananchi wa Zanzibar japo hawalitambui hilo!

Nchi ya Tanganyika yenyewe imeambulia kilio cha mamba huku watu wake wakiwa na jukumu la kuondoa vyombo mezani baada ya "wakubwa" kumaliza kula.
 
Inasemekana, kuna aliyewahi kutaka kufanya hivyo akashikishwa adabu! Alikuwa nani vile? Ni mzee Jumbe au mwingine?
 
Kwahiyo Zanzibar iwaombe radhi watanganyika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…