Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Tanganyika iiombe radhi Zanzibar?

Tatizo ni kwamba Zanzibar hawataki kujitegemea na wanapenda vya bure kutoka Tanganyika. Bajeti ya Zanzibar inatoka bara la sivyo Zanzibar wangekuwa wameshavunja muungano kitambo.
Zanzibar Haina Jeshi. Zanzibar ipo mikononi mwa Tanganyika. Itaanzaje kufurukuta?

Bila Tanganyika kuamua, Zanzibar haitathubutu kufanya hivyo. Hata watamanije, maamuzi yapo Tanganyika.
 
Ukiona mtu anasema, inasemekana... achana naye... hapa ungekuja na facts na siyo gossip
 
Viongozi kutoka Zanzibar hata rais wa Zanzibar ndio wanaojua madhara ya kuvunja muungano, hao wengine wanajisemea tu. Zanzibar haijaweza bado kujitegemea kifedha siku wakiweza muungano utavunjika hapo hapo!


Of cource viongozi wanajua madhara kwani wameiba sana na kuuwa watu , wanaogopa kupelekwa mahakamani
 
Sii kweli!, baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Manowari za Uingereza zilitia nanga Mombasa tayari kuivamia Zanzibar, kuikomboa. Karume akaja kwa Nyerere kuomba ulinzi, ndipo, Nyerere akamshauri Karume tuungane kuwa nchi moja, Karume akajibu hata leo, wewe Rais mimi Makamo.
Kwahiyo waingereza waliogopa kupigwa na Nyerere wakageuza meli?

Vyovyote ilivyo, suala la kuongelea kuvunja muungano si busara especially baada ya miaka 60 toka tuungane. Busara ni kujadili kero zilizopo kwa haki na kuzitatua kwa haki kila upande ukawa umeridhika.

Wenye akili ndogo tu ndo watang'ang'ania kuvunja muungano kwa hapa tulipofika.
 
Ukiona mtu anasema,inasemekana......... achana naye....hapa ungekuja na facts na siyo gossip
Tundu Lissu kasema...

Mzee Mohamed Said kasema...

Fatma Karume kasema...

Wazanzibar wengi wameshasema...

Hata humu JF yashasemwa mengi...

Hayo yasemwayo ni gossip au facts?
 
Ila Ka Nyerere kalikuwa kichwa kale kajamaa aisee. Sijui kalimwingiaje Karume mpaka akaingia kingi kwenye hili limuungano la kimagumashi 😁😁😁
Please Sir! Usimwite mzee "ka", plse!!!

Ila kwa kweli, mzee alikuwa kichwa.

Kawasaidia Wasouth weusi kuingia madarakani nchini kwao!

Kazisadia nchi nyingi za Afrika kupata uhuru!

Kaiunganisha Tanganyika na Zanzibar bila ridhaa yao lakini mpaka sasa wanalitii agizo lake la kulinda Muungano kwa gharama yo yote.

Ni kweli, mzee Nyerere alikuwa kichwa mnoo!!!
 
Sii kweli!, baada ya yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Manowari za Uingereza zilitia nanga Mombasa tayari kuivamia Zanzibar, kuikomboa. Karume akaja kwa Nyerere kuomba ulinzi, ndipo, Nyerere akamshauri Karume tuungane kuwa nchi moja, Karume akajibu hata leo, wewe Rais mimi Makamo.

Sii kweli, huo ni uongo wa wapinga Mapinduzi Matukufu, ukweli ni huu Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa! Walikimbia Wenyewe - Mzee Sukari

Sii kweli

Sii kweli

Sii kweli, Zanzibar ilikuwa sehemu ya Tanganyika kabla haijamegeka!. Hivyo ni sehemu yetu kihalali kabisa!.

Sii kweli

ni kweli ila mengine ni ya kweli, mengine ni ya uongo!

Si kweli

Na kama ni uongo?.

Uungwana ni vitendo ni kweli kuna ndivyo sivyo

Naunga mkono hoja na hata mimi hili nilishauri Wanzanzibar amueni moja, ama acheni kelele za muungano!, ama pigeni Kura ya Maoni, muamue moja

Hapa tuko pamoja.
P
Kama utakuwa umesoma vizuri history, muungano wa Tanganyika na Zanzibr una mkono mrefu. Kumbukumbu zinaonyesha kwa wakati huo, vita baridi kati ya ukomunism na ubepari ulikuwa upo katika kilele.
Kipindi hicho Tanganyika halikuwa taifa la kijamaa na wala Zanzibar vilevile.
Zanzibar ni kisiwa, ni kisiwa kilichowahi tawala mpaka ndani mwa nyika. Ni Taifa lililoogopeka kuanguka katika mikono ya kicommunism kama vilivyokuwa visiwa vingi kabla yake, hali ambayo ingeweza kuathiri Afrika Mashariki yote kutokana na itikadi na hali iliyokuwepo wakati ule - kipindi ambacho nchi nyingi ziliangukia katika mkono wa Marxism-Lenism hivyo basi mataifa makubwa ikiwemo Marekani ilitoa baraka zote kwa mapinduzi yale kufanyika.

Pamoja na hilo lipo pia suala la imani ambalo linafungamana mno na dini, rasilimali fedha iliyokuwa nayo Zanzibar iliyobebwa na uchumi mzuri kabla ya mapinduzi na hata baada ya mapinduzi. Vyote hivi vilivutia Muungano baina ya nchi hizi mbili kuwa ni jambo lisilo budi kutekelezwa. Mfumo ukaingia kazini na kuyaratibu vizuri mapinduzi kuanzia kule Pangani mpaka kisiwani.

Pasi na kuficha, ni kweli Tanganyika ilikuwa na mkono mzuri katika mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Lakini kwa sasa faida zake Muungano ni kubwa zaidi kwa maslahi mapana ya Taifa, sote wa Bara na Visiwani.

N.B: ZANZIBAR LILIKUWA NI TAIFA HALALI LENYE MAMLAKA YAKE KAMILI KUITWA NCHI. KAMWE NDUGU PASKO, ZANZIBAR HAIKUWA SEHEMU YA TANGANYIKA. ZANZIBAR ILIKUWEPO HATA KABLA YA UWEPO WA TANGANYIKA.
 
Kama utakuwa umesoma vizuri history, muungano wa Tanganyika na Zanzibr una mkono mrefu. Kumbukumbu zinaonyesha katika wakati huo, vita baridi kati ya ukomunism na ubepari ulikuwa upo katika kilele.
Kipindi hicho Tanganyika halikuwa taifa la kijamaa na wala Zanzibar vilevile.
Zanzibar ni kisiwa, ni kisiwa kilichowahi tawala mpaka ndani mwa nyika. Ni Taifa lililoogopeka kuanguka katika mikono ya kicommunism ambayo ingeweza kuathiri Afrika Mashariki yote kutokana na itikadi na hali iliyokuwepo wakati ule kipindi amvacho nchi nyingi ziliangukia katika mkono wa Marxism-Lenism.
Pamoja na hilo lipo pia suala la imani, na rasilimali fedha iliyokuwa nayo Zanzibar vyote hivi vilivutia Muungano baina ya nchi hizi mbili.
Pasi na kuficha, ni kweli Tanganyika ilikuwa na mkono mzuri katika mapinduzi matukufu ya Zanzibar. Lakini kwa sasa faida zake Muungano ni kubwa zaidi kwa maslahi mapana ya Taifa, sote wa Bara na Visiwani.

N.B: ZANZIBAR LILIKUWA NI TAIFA HALALI LENYE MAMLAKA YAKE KAMILI KUITWA NCHI. KAMWE NDUGU PASKO ZANZIBAR HAIKUWA SEHEMU YA TANGANYIKA.
Kama hautojali, naomba nikuulize hili! Yalikuwa Mapinduzi Tukufu au Mauaji Katili?
 
Back
Top Bottom