Tanganyika Packers palipokuwa Kiwanda kilichotoa ajira zaidi 2000, pamefunguliwa Kanisa. Watu wanauziwa udongo, mafuta na maji

Tanganyika Packers palipokuwa Kiwanda kilichotoa ajira zaidi 2000, pamefunguliwa Kanisa. Watu wanauziwa udongo, mafuta na maji

Wenzetu wazungu wamebuni ajira nyingi sana kwenye dini na hata sherehe zingine na kodi zinalipwa pia
Kuanzia Xmas cards mpaka father Xmas, chocolates na vyakula na zawadi kede kede za sherehe hizi
Ila nyie mnauziwa udongo na maji na tapeli anapita na hela zote bila kulipa kodi akisingizia dini
Mna safari ndefu ya kuja kujitambua
Haya ndio upinzani kuyqpigia kelele na sio sisi
 
tukiwaambiaga nyerere ndo kirusi namba moja kwenye hii nchi mnakomaza fuvu. hii nchi isingetawaliwa na nyerere tungekuwa mbali sana.
Nchi zote za Afrika, Nyerere ndiye alikuwa mtawala? Nenda hapo Congo tu ambako Mobutu ndiye alikuwa rais kipenzi cha mataifa ya Magharibi usiposema bora hata Nyerere. Ila una hoja, tatizo ni watawala ila umefanya kosa kusema ni Nyerere na kuacha marais wa kiafrika wengine. Tena Nyerere alikuwa nafuu angalau alituachia madini na kutuunganisha.
 
Leo vijana wa Mwamposa walikua wanapita mtaani kusambaza posters zao za mkesha wao.

Ukiwaona tu, kwa ule muonekano wao ni dhahiri shahir wanajitolea kufanya ile kazi...

Yule mzee sijui huwa anawalisha nini hawa watu mpaka wanakua loyal kwake kama mungu mtu vile.

Ajabu sasa hizo posters anagawa bure na ni nyingii huenda hata zaidi ya laki 5 ila posters za kuelezea kitu chochote kiroho, sijui uponyaji anauza.
 
Kwa maelezo hapo kiwanda kilikufa rasmi 1993,mpaka hapo tu bado hakukuwa na akili mpya ya kukiendesha?na wala sio kiwanda pekee kilichotushinda.Ufundi pekee tuliojaliwa ni kuorodhesha visingizio.Mtu muulize tu kwa nini umefeli basi atajaza kaunta book kumi za visingizio.Huo ujamaa au Mwalimu unakuzuia nini leo kufufua like kiwanda cha General tyre kwa mfano?Watu weusi tu macalio sana.
Watu weusi macalio wa ukoo wenu na wale walioamini serikali dhaifu za kifisadi zinaweza kuendesha miradi kibiashara.
 
Nchi zote za Afrika, Nyerere ndiye alikuwa mtawala? Nenda hapo Congo tu ambako Mobutu ndiye alikuwa rais kipenzi cha mataifa ya Magharibi usiposema bora hata Nyerere. Ila una hoja, tatizo ni watawala ila umefanya kosa kusema ni Nyerere na kuacha marais wa kiafrika wengine. Tena Nyerere alikuwa nafuu angalau alituachia madini na kutuunganisha.
tanganyika packers ipo tz haipo drc, alituunganisha kwan tulikuwa tumetengana?
 
Back
Top Bottom