Tangawizi, limao, apple vinegar na vitunguu swaum vimeniletea shida

Tangawizi, limao, apple vinegar na vitunguu swaum vimeniletea shida

Uli Over doze kwani Limao ina shusha presha Kitunguu saumu kina shusha presha Siki ya Apple Cider Vinegar ina shusha presha na Tangawizi pia ina shusha presha sasa wewe ulikuwa na presha yenye ukubwa wa aina gani mpaka utumie dawa zote hizo kwa pamoja?
Asante kwa ushauri mkuu Mzizi.
 
Hebu tujuze lengo hasa la kunywa izo vitu ilikuwa ni nini!
 
mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu swaumu unapelekea damu iwe nyembamba sana, ukiendelea kunywa unaweza kushangaa damu inakutoka puani, kwa sababu inakuwa imekuwa nyembemba sana, moyo ukisukuma inakwenda kasi zaidi kuliko ikiwa viscous, kuwa makini
 
Asante k
mchanganyiko wa tangawizi na vitunguu swaumu unapelekea damu iwe nyembamba sana, ukiendelea kunywa unaweza kushangaa damu inakutoka puani, kwa sababu inakuwa imekuwa nyembemba sana, moyo ukisukuma inakwenda kasi zaidi kuliko ikiwa viscous, kuwa makini
Asante kwa ushauri mkuu
 
Hbr zenu wakuu,nisaidieni kuelewa haya yaliyonikuta Leo,nimeamka asbh nikachemsha tangawizi kali,,kiasi cha kikombe kile kikubwa then nikachanganya na vitu vifuatavyo nusu limao na Apple vinegar kiasi cha kijiko kimoja cha chakula nikanywaaa halafu nikachukua punhe 8 zile Nene za vitunguu swaumu nikavikatakata nikanywa kwa kusukumizia maji kidogo,jamani jamani baada kama ya dk 40 nimejisikia vby Sn yaani kama vile nikawa nawasiwasi iliyopitiliza halafu siwezi kutulia,pia nikawa mdhaifu ghafra na kakizunguzungu kwa mbaliii,yaani kama nimelewa hivi halafu pumzi nikawa nahisi kama inabana kwa mbaliii...haraka nikanywa maji mengi kidogo nikajisikia afadhali ingawa ingawa ka udhaifu ka Mwili nakahisi kwa mbalii bado kapo,hii ni mini jamani? Au huo mchanganyiko haufai kiafya?
Mamchanganyiko mengine sumu!!
 
Kaa! Jamaaa una moyo yaani APPLE CIDER VINEGAR,HALAFU NA TANGAWIZ HALAFU TENA KITUNGUU SWAUM mmmmmh mkuu pole Sana .wakati mwingine changanya na zako!
 
Wewe ni nani aliye kufundisha hiyo dawa? Wewe umeona wapi kuchanganya Limao pamoja na Siki ya Apple Cider Vinegar? Limao ni Asidi na Apple Cider Vinegar ni asidi inakuwaje unavichanganya pamoja?unajitafutia upatwe na maradhi? Kitu haujuwi bora

uulize sio kuparamia vitu na kujifanyiwe wenyewe utakuja kujidhuru shauri yako. Vitunguu saumu ,Tangawizi limao na Apple Cider Vinegar kazi yake ni kushusha Presha ya moyo sasa wewe umevichanganya vyote pamoja ndio

maana ukaona mabadiliko ya mapigo yako ya moyo yalikuwa yanashuka kwa haraka sana usije kutumia siku nyingine vitu hivyo kwa pamoja tutakuja kukusahau hapa jukwaani.Tumia hivi Chukuwa Vitunguu saumu punje 2 kijiko 1

kidogo cha unga wa tangawizi kijiko 1 cha limao kamuwa upate maji yake changanya kwenye glasi au kikombe 1 cha maji ya moto utie na asali safi ya nyuki kijiko 1 ni dawa nzuri kwa maradhi mengi tu. Au toa Limao weka Kijiko 1 cha Apple cider vinegar.Koroga vizuri upate kunywa asubuhi kabla ya kula kitu.
Huo mchanganyiko unajibu nini? Au unamsaidia nini? Hizo punje za kitunguu swaum,unazitwanga au unachanganyaje kwenye huo mchanganyiko? Unakunywa kila siku au?.
 
Back
Top Bottom