Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Pascal Mayalla,
Rais anatakiwa kusaidiwa vitu vingi tu. Najua una maanisha ana mapungufu mengi yaliyo wazi sana.

Hata hivyo alikuwa anajaribu kuendana na kasi ya kigogo wa twita ambaye kwa maneno yake ya shombo angesababisha collateral damage kwa image ya chenkapa.
 
Sababu ya kifo hiki ni siri kubwa.
Na kwa nini iwe siri kifo cha mtu mkubwa hivyo katika jamii?
Watu wakuanza minong'ono kuwa kanyamazishwa watawalaumu?
Au kama ni ugonjwa, jee ni ugonjwa gani huo wa aibu hadi iwe siri?
Kaswende au kisonono? Utawala huu kila jambo ni siri siri tuu, kwa vile kwao kila kitu ni uongo na propaganda basi.
Hii aibu ya utawala huu ni vyema octoba tuiondoe na nchi irudi kwenye misingi yake na heshima sio uhuni uhuni bwana!
 
Lile swali aliloulizaga kwenye mkutano wa waandishi wa habari na mh.Rais linamponza sana.
 
Mtailaumu bure hiyo kurugenzi ya mawasiliano, kaa ukifaham yeye ndio kurugenzi husika anapanga ratiba mwenyewe na content to release. Hivyo hashauliki kwa mtu makini hakupaswa kutoa tamko usiku ule.
 
Pascal Mayalla,

Kwa mitandao ya sasa, mida ya saa kumi na mbili asubuhi hiyo isingekua taarifa tena kwa umma maana nchi nzima saa saba au nane ingekua imeshajua! Labda hii ingekua tamko tu la rais ila sio taarifa!

Kuna mida codes tupa kule.
Kiongozi kama yule hafii wadi ya Mwaisela kiasi cha kila daktari au nesi kujua kafa. Hivyo kuzuia habari hiyo masaa kama 6 tena usiku sio jambo gumu sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…