Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Tangazo alitoa ndani ya dk 1 na sekunde 15 kamaliza hakuna info zozote unajua muda ule nilipoona ile video nikashangaa sana nikajiuliza mbona kama aliyekufa ni Mjumbe wa Nyumba kumi yaani...halafu pia hakukua na uharaka wa kutangaza vile katika usiku ule.
Kwa sisi tuliofuatilia kwa Radio tangazo la Msiba wa Sokoine, tukaona tangazo la Msiba wa Mwalimu na Omar, tukaja tukamsikia JK akitangangaza msiba wa Kawawa, tunaungana na Mayala.
Juzi Tangazo limetoka kiwepesi na muda mbaya sana.
 
Huyu ndio Pascal Mayalla ninayemfahamu. Na kwa chokochoko hizi ni kama vile anatamani kutaja chanzo cha kifo cha mzee katika ile thana ya JF tuna right ya kuwa wa kwanza kupata habari lakini anaogopa.... lakini JK anasema Mzee Mkapa alikuwa analalamika tumbo linamuuma. Labda Rais wetu Kipenzi chetu sisi wanyonge atatuambia sababu ya kifo siku ya mazishi.
Tumbo limeungana na kifua, kwa ukubwa wa mwili ule ni rahisi kabisa ukakabwa koo ukahisi maumivu tumboni.
 
Pascal Mayalla,
Upo sahihi 100%, ila inakuwaje kama yeye mwenyewe aliamuru alitoe hilo tangazo muda huo huo baada ya kupewa taarifa?
Kuna watu wanasemaga mzee hasikilizi ushauri muda mwingine.

Haya ngoja tuwaachie wajuzi wanaoangalia on both sides of the coin
 
Yeye alitaka Tangazo liwafikie wa Tanzania wanyonge usiku ule ule, milundikano mingine ya kisheria inakwamisha mambo.
P
 
Tangazo la msiba wa aliyekuwa kiongozi mkuu wa nchi hukaa kwenye record hata kwa miaka mingi.

Hii ina maana namna ile alivyotangaza, alivyovaa na yale aliyoyasema, yatatazamwa na kuikiwa na vizazi vingi vijavyo. Hivyo inahitajika maandalizi na utulivu wa hali ya juu.

Mlioshuhudia kifo cha Princess Diana wa Uingereza, nadhani mliona. Diana alikuwa na watoto wake wawili teenagers. Katika hali ua kawaida wangeweza hata kutoa machozi hadharani kutokana na kifo cha ghafla cha Mama yao. Lakini kwa taratibu za kifalme, mfalme, malkia au wanafamilia wa ufalme hawaruhusiwi kulia hadharani. Na katika tukio zima hakuna aliyeonekana kutoa machozi hadharani. Ile haikutokea tu bali kulikuwa na maandalizi.

Sisi hatulazimiki kuiga ya watu wengine lakini tunalazimika kuwa na miongozo ya kila kitu.

Rais Magufuli katika hili, ni miongoni mwa wafiwa wakuu, kama kiongozi wa nchi na pia kwa mahusiano yao ya karibu. Alistahili kutulizwa, kulukezwa na hata kuvumiliwa. Kumwacha afanye kama alivyoongozwa na dhamira yake, haikuwa sahihi.

Kuna wakati watu wanakosa kutimiza wajibu wao halafu kujitetea kwao inakuwa ni rahisi tu - Rais hasikilizi ushauri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una uhakika hawakupendekeza hayo? Mtu ambaye hapangiwi Cha kufanya unafikiri anashaurika? Kwataarifa yako watendaji wa rais wanatembea na beat ya rais ili wasitumbuliwr. Chamuhimu taarifa umepata inatosha hayo mengine utawaponza wenzio. Au mzee baba mnaitaka nafasi ya msigwa? [emoji125][emoji125]

Hilo swali la mwisho ndio mzizi wa yote haya.
 
Wanabodi,
Naangalia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kipindi kinajadili Msiba wa Benjamin Mkapa.

Tangazo la Msiba lililotolewa na Rais Magufuli, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu imelaumiwa kwa kutokumsaidia rais kikamilifu kutoa tangazo hili, hali inayotafsiriwa kuwa katika baadhi ya matukio, Kurengenzi hiyo inahitaji kusaidiwa na manguli wazoefu ili waweze kumsaidia rais Magufuli katika baadhi ya matukio.

Manguli wa Mwanza, Dotto Bulendu, Edwin Soko na Moses Mathews, wamesema kwa vile hii ni shocking news, kulipaswa kuwepo kwa muda kidogo wa kumuandaa rais Magufuli kutoa tangazo hilo kulitangazia kuanzia, timing, dress code na content za tangazo lenyewe.

Timing
Kwa vile msiba umetokea usiku, kutoa tangazo saa 6:30 usiku was not the right timing kwa Watanzania, news ya msiba ingekuwa held, halafu Wahariri wakaitwa Ikulu usiku ule, halafu Tangazo litolewe live saa 12:00 asubuhi, rais akiwa na VP na PM.
TCRA kutoa taarifa vyombo vyote vya habari vya k electronic kujiunga na TBC ili hiyo live itangazwe Tanzania nzima.

Dress Code.
Kuna mavazi ya kawaida mtu anaweza kuvaa katika tukio lolote, lakini kuna dress code ya msiba. Wanasema rais Magufuli alipaswa kushauriwa kutoa tangazo hilo akiwa amevaa a proper dress code ya tangazo hilo.

Contents za Tangazo
Tangazo la msiba wa kiongozi wa kitaifa linaongozwa na sheria ya Vifo vya viongozi, sheria imeweka contents za kisheria ambazo lazima liwe na vitu 6
  1. Jina la Kiongozi ni nani
  2. Kifo kimetokea lini
  3. Kifo kimetokea wapi nchini, mkoani, safarini, nje ya nchi
  4. Mahali mahsus, kimetokea nyumba, hospitalini, safarini,
  5. Kama ni hospitalini, hospitali gani
  6. Sababu za kifo, kimesababishwa na nini, maradhi, ajali, usingizini, etc
Tangazo la rais Magufuli kutangaza kifo cha Mkapa, lilikosa, baadhi ya taarifa muhimu za kisheria, hivyo kuleta sintofahamu kwa jamii.

Hajawahi kusikika kuwa Benjamin Mkapa anasumbuliwa na maradhi yoyote, hivyo taarifa kuwa amefariki hospitali ni shocking, hospitali gani na ameumwa nini, ni maswali ambayo taarifa ya rais ilikosa.

My Take
Kwa vile taarifa ya msiba ni shocking news, flaws ndogo ndogo katika tangazo la msiba huo, zinavumilika.

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inafanya kazi nzuri katika upashanaji habari wa shughuli za rais, lakini lazima itenganishe matangazo ya kawaida ya rais kwa shughuli za kila siku za kazi za rais na tangazo la taifa, Watu wa Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas walipaswa kuhusishwa, na kwa vile mimi sio mserikali kujua nani alihusika, kama Dr. Abbas alihusika na bado tangazo la rais ndio lile, hii inamaanisha Dr. Abbas anaelemewa naye anahitaji kuwekewa wasaidizi.

Kwa maoni yangu, japo sheria inatamka tatangazo litolewe immediately kunapotokea msiba, kama msiba umetokea usiku wa baada ya saa 6:00, then alfajiri ni immediately kulikuwa hakuna uharaka wa kukimbilia kutangaza usiku mkubwa huo huo ili kutoa nafasi kwa rais kutangaza in a proper way na kufanya mashauriano na watu wawili watatu ili kutoa tangazo kamilifu kisheria, kikanuni na kiutaratibu na sio kumuharakisha rais kutangaza huku he looks sleepy!.

Namalizia kwa kutoa pole kwa Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli, Familia ya Mkapa na Watanzania kwa ujumla, kwa msiba huu mkubwa wa rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Paskali

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake!
Naunga mkono hoja. Hata mheshimiwa alitakiwa aandikiwe hotuba yenyewe maana kuna wakati alikuwa anarudia rudia contents ... na wimbo wa taifa ulitakiwa upigwe...kwa kweli limetolewa simple simple sana.
 
Back
Top Bottom