Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Wanabodi,
Naangalia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kipindi kinajadili Msiba wa Benjamin Mkapa.

Tangazo la Msiba lililotolewa na Rais Magufuli, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu imelaumiwa kwa kutokumsaidia rais kikamilifu kutoa tangazo hili, hali inayotafsiriwa kuwa katika baadhi ya matukio, Kurengenzi hiyo inahitaji kusaidiwa na manguli wazoefu ili waweze kumsaidia rais Magufuli katika baadhi ya matukio.

Manguli wa Mwanza, Dotto Bulendu, Edwin Soko na Moses Mathews, wamesema kwa vile hii ni shocking news, kulipaswa kuwepo kwa muda kidogo wa kumuandaa rais Magufuli kutoa tangazo hilo kulitangazia kuanzia, timing, dress code na content za tangazo lenyewe.

Timing
Kwa vile msiba umetokea usiku, kutoa tangazo saa 6:30 usiku was not the right timing kwa Watanzania, news ya msiba ingekuwa held, halafu Wahariri wakaitwa Ikulu usiku ule, halafu Tangazo litolewe live saa 12:00 asubuhi, rais akiwa na VP na PM.
TCRA kutoa taarifa vyombo vyote vya habari vya k electronic kujiunga na TBC ili hiyo live itangazwe Tanzania nzima.

Dress Code.
Kuna mavazi ya kawaida mtu anaweza kuvaa katika tukio lolote, lakini kuna dress code ya msiba. Wanasema rais Magufuli alipaswa kushauriwa kutoa tangazo hilo akiwa amevaa a proper dress code ya tangazo hilo.

Contents za Tangazo
Tangazo la msiba wa kiongozi wa kitaifa linaongozwa na sheria ya Vifo vya viongozi, sheria imeweka contents za kisheria ambazo lazima liwe na vitu 6
  1. Jina la Kiongozi ni nani
  2. Kifo kimetokea lini
  3. Kifo kimetokea wapi nchini, mkoani, safarini, nje ya nchi
  4. Mahali mahsus, kimetokea nyumba, hospitalini, safarini,
  5. Kama ni hospitalini, hospitali gani
  6. Sababu za kifo, kimesababishwa na nini, maradhi, ajali, usingizini, etc
Tangazo la rais Magufuli kutangaza kifo cha Mkapa, lilikosa, baadhi ya taarifa muhimu za kisheria, hivyo kuleta sintofahamu kwa jamii.

Hajawahi kusikika kuwa Benjamin Mkapa anasumbuliwa na maradhi yoyote, hivyo taarifa kuwa amefariki hospitali ni shocking, hospitali gani na ameumwa nini, ni maswali ambayo taarifa ya rais ilikosa.

My Take
Kwa vile taarifa ya msiba ni shocking news, flaws ndogo ndogo katika tangazo la msiba huo, zinavumilika.

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inafanya kazi nzuri katika upashanaji habari wa shughuli za rais, lakini lazima itenganishe matangazo ya kawaida ya rais kwa shughuli za kila siku za kazi za rais na tangazo la taifa, Watu wa Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas walipaswa kuhusishwa, na kwa vile mimi sio mserikali kujua nani alihusika, kama Dr. Abbas alihusika na bado tangazo la rais ndio lile, hii inamaanisha Dr. Abbas anaelemewa naye anahitaji kuwekewa wasaidizi.

Kwa maoni yangu, japo sheria inatamka tatangazo litolewe immediately kunapotokea msiba, kama msiba umetokea usiku wa baada ya saa 6:00, then alfajiri ni immediately kulikuwa hakuna uharaka wa kukimbilia kutangaza usiku mkubwa huo huo ili kutoa nafasi kwa rais kutangaza in a proper way na kufanya mashauriano na watu wawili watatu ili kutoa tangazo kamilifu kisheria, kikanuni na kiutaratibu na sio kumuharakisha rais kutangaza huku he looks sleepy!.

Namalizia kwa kutoa pole kwa Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli, Familia ya Mkapa na Watanzania kwa ujumla, kwa msiba huu mkubwa wa rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Paskali

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake!
Si jambo la kushangaza sana lakini wakti mwingine tujitahidi kutofautisha msiba na harusi.Msiba wa kwanza wa kitaifa ulikuwa wa Karume na wakati ule Radio ilikuwa moja tu RTD na redio set zikiwa chache sana,sina kumbukumbu vizuri ilikuwaje.Msiba wa pili ni wa Sokoine,haukutangazwa mara moja ili zilipigwa nyimbo za kijeshi mfululizo mno na watu tukahisi labda serikali imeanguka.Kama hiyo haikutosha Sokoine alifia Morogoro lakini Nyerere hakuamini mpaka maiti ilivyopelekwa Ikulu.
Hili sidhani ni jambo kubwa sana kwani wangesubiri mpaka asubuhi wangeipa chat mitandao ya kijamii.
 
Pia sehemu alipokaa wakati wa kutoa tangazo, nyuma kuna socket za umeme. Haipendezi
Hivi hamjui Magufuli? Kwenye hali kama hiyo atawaambia ''natangaza sasa hivi''. Wakimwambia mambo ya dress code, sehemu aliyokaa atawaambia ''natangazia hapa hapa chumbani, kwani nani ataniuliza?''
 
Pascal Mayalla,

Kwa mitandao ya sasa, mida ya saa kumi na mbili asubuhi hiyo isingekua taarifa tena kwa umma maana nchi nzima saa saba au nane ingekua imeshajua! Labda hii ingekua tamko tu la rais ila sio taarifa!

Kuna mida codes tupa kule.
Idadi kubwa ya watu mida ile ya saa 6:30 usiku ninaamini wangekuwa wamelala vitandani mwao, sasa habari za msiba wangezipataje Chief barafuyamoto?
Ndotoni?
 
Wanabodi,
Naangalia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kipindi kinajadili Msiba wa Benjamin Mkapa.

Tangazo la Msiba lililotolewa na Rais Magufuli, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu imelaumiwa kwa kutokumsaidia rais kikamilifu kutoa tangazo hili, hali inayotafsiriwa kuwa katika baadhi ya matukio, Kurengenzi hiyo inahitaji kusaidiwa na manguli wazoefu ili waweze kumsaidia rais Magufuli katika baadhi ya matukio.

Manguli wa Mwanza, Dotto Bulendu, Edwin Soko na Moses Mathews, wamesema kwa vile hii ni shocking news, kulipaswa kuwepo kwa muda kidogo wa kumuandaa rais Magufuli kutoa tangazo hilo kulitangazia kuanzia, timing, dress code na content za tangazo lenyewe.

Timing
Kwa vile msiba umetokea usiku, kutoa tangazo saa 6:30 usiku was not the right timing kwa Watanzania, news ya msiba ingekuwa held, halafu Wahariri wakaitwa Ikulu usiku ule, halafu Tangazo litolewe live saa 12:00 asubuhi, rais akiwa na VP na PM.
TCRA kutoa taarifa vyombo vyote vya habari vya k electronic kujiunga na TBC ili hiyo live itangazwe Tanzania nzima.

Dress Code.
Kuna mavazi ya kawaida mtu anaweza kuvaa katika tukio lolote, lakini kuna dress code ya msiba. Wanasema rais Magufuli alipaswa kushauriwa kutoa tangazo hilo akiwa amevaa a proper dress code ya tangazo hilo.

Contents za Tangazo
Tangazo la msiba wa kiongozi wa kitaifa linaongozwa na sheria ya Vifo vya viongozi, sheria imeweka contents za kisheria ambazo lazima liwe na vitu 6
  1. Jina la Kiongozi ni nani
  2. Kifo kimetokea lini
  3. Kifo kimetokea wapi nchini, mkoani, safarini, nje ya nchi
  4. Mahali mahsus, kimetokea nyumba, hospitalini, safarini,
  5. Kama ni hospitalini, hospitali gani
  6. Sababu za kifo, kimesababishwa na nini, maradhi, ajali, usingizini, etc
Tangazo la rais Magufuli kutangaza kifo cha Mkapa, lilikosa, baadhi ya taarifa muhimu za kisheria, hivyo kuleta sintofahamu kwa jamii.

Hajawahi kusikika kuwa Benjamin Mkapa anasumbuliwa na maradhi yoyote, hivyo taarifa kuwa amefariki hospitali ni shocking, hospitali gani na ameumwa nini, ni maswali ambayo taarifa ya rais ilikosa.

My Take
Kwa vile taarifa ya msiba ni shocking news, flaws ndogo ndogo katika tangazo la msiba huo, zinavumilika.

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inafanya kazi nzuri katika upashanaji habari wa shughuli za rais, lakini lazima itenganishe matangazo ya kawaida ya rais kwa shughuli za kila siku za kazi za rais na tangazo la taifa, Watu wa Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas walipaswa kuhusishwa, na kwa vile mimi sio mserikali kujua nani alihusika, kama Dr. Abbas alihusika na bado tangazo la rais ndio lile, hii inamaanisha Dr. Abbas anaelemewa naye anahitaji kuwekewa wasaidizi.

Kwa maoni yangu, japo sheria inatamka tatangazo litolewe immediately kunapotokea msiba, kama msiba umetokea usiku wa baada ya saa 6:00, then alfajiri ni immediately kulikuwa hakuna uharaka wa kukimbilia kutangaza usiku mkubwa huo huo ili kutoa nafasi kwa rais kutangaza in a proper way na kufanya mashauriano na watu wawili watatu ili kutoa tangazo kamilifu kisheria, kikanuni na kiutaratibu na sio kumuharakisha rais kutangaza huku he looks sleepy!.

Namalizia kwa kutoa pole kwa Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli, Familia ya Mkapa na Watanzania kwa ujumla, kwa msiba huu mkubwa wa rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Paskali

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake!
Corona bado ipo na inaua sana
 
Saa 12 asubuhi?...[emoji23][emoji23][emoji23] wazee wenzangu wa jamii forums usiku wa manane isingekuwa taarifa mpya tena..ingeshakuwa story.

So rais alikuwa anataka kuwa wa kwanza kutoa taarifa, mpaka akatoa taarifa isiyo na kiwango kama tetesi za kifo huku mitandaoni?
 
Rais mstaafu Mkapa alizidiwa ghafla usiku akiwa kihospitali cha hapo Makumbusho ambako hakuna hata ventilator. Kiukweli alibanwa na mapafu ila timing ikawa mbovu. Mzaha mzaha wa serikali ya Magufuli kuhusu mambo muhimu ya afya za watanzania yanawagarimu wengi.

Halafu Rais wa nchi kutangaza msiba huku umelegea kama umetoka kula ile kitu ya Mshana Jr au mrangi haileti picha ya kuwa Amir jeshi mkuu tena umewahi kuvaa gwanda kabisa. Kutangaza huku unalegeza mwili ili watanzania waone kuwa umeumizwa sana ni ulimbukeni. In short lile tangazo nililiangalia mwanzoni tu nikaachana nalo maana Rais alikuwa very weak! Kuwa vile hakukufanyi kuonekana eti umeumizwa sana na ni udhaifu mkubwa kwa Amir jeshi mkuu.
Mzeee baba hatii shaka kama amiri jeshi mkuu yes..ameshaonyesha hilo kwe vita dhidi ya corona,rushwa na ubadhilifu wa mali ya umma.he is fit " kamanda".but still ni binadamu kama wengine
 
Wangejifunza jinsi Mkapa alipotangaza kifo cha Mwalimu Nyerere

Kulia kwake alikuwepo Waziri mkuu ndugu Sumaye, Kushoto kwake alikuwepo Dr Omar Ali Juma na wote walivaa kimamlaka

Sasa Magufuli anavaa Shati la mchelemchele kututangazia kifo cha Raisi Mstaafu huku tukiwa tumelala usiku na yeye anaongea utafikiri alikuwa usingizini

Kisha anatoka hapo anaenda msibani huku amevaa shati la CCM

Nadhani Mkapa alimtendea haki sana Mwalimu Nyerere jinsi alivyohandle msiba wake kuliko jinsi yeye alivyotendewa na utawala huu
 
Saa ile ilikuwa mbaya sana, Rais kweli hakuandaliwa, nahisi huko aliko naye leo ana BP,

Sikusikia hata wimbo wa Taifa, hata ule wa Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote.

Hata kama alifia nyumbani au kituo cha afya wangesema, waseme pia aliugua nini,

Mbona maziko yamekimbizwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Mimi nilitegemea kwanza wimbo wa taifa kupigwa alafu ndo tuanze kujiuliza kuna nini?? Sasa ndo raisi ahutubie taifa kwa kutoa hiyo taarifa,
 
Kwa maoni yangu, japo sheria inatamka tatangazo litolewe immediately kunapotokea msiba, kama msiba umetokea usiku wa baada ya saa 6:00, then alfajiri ni immediately kulikuwa hakuna uharaka wa kukimbilia kutangaza usiku mkubwa huo huo ili kutoa nafasi kwa rais kutangaza in a proper way na kufanya mashauriano na watu wawili watatu ili kutoa tangazo kamilifu kisheria, kikanuni na kiutaratibu na sio kumuharakisha rais kutangaza huku he looks sleepy!.
Naunga mkono hoja ,asante kwa kututanabahisha ,
Lakini yawezekana Jiwe alipopata taarifa tuu akakurupuka kuitowa bila ya kufuata taratibu tajwa hapo juu.
Hii ni hulka yake ya pupa na kukurupuka juu ya mambo mingi.
Hata kutumbua ,huwa hafanyi upembuzi yakinifu, yeye akiona kosa ni papohapo,
Yampasa na yeye Mkuu ajiweke sawa, na ashirikishe wenzake ,Maana Uraisi ni Taasisi, si mtu mmoja tuu kama anavyotuaminisha mkuu kuwa Uraisi ni wake peke yake ,hahitaji Mtu amshauri.
 
Back
Top Bottom