Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Zile soccet mbili pale Nyuma nilijua mazingira hayakuwa sahihi kabisa Ni kama alitangazia gheto, harafu lile kochi sio presidential,

Nikiangalia na lile alilolitoa mkapa Ni tofauti kubwa
 
Pascal Mayalla , umeanza kuponda halafu mwishoni unapamba kuwa na msimamo mmoja au sema wazi kama Msigwa hatoshi
 
Baada ya kukosa teuzi umeanza zile mada zako halisi sio zile za kusifu na kuabudu
Pasco ana akili sana. Tatizo njaa ndio inamtesa.

Na kwa huu uzi hapewi uteuzi tena. Hapa ameongea ukweli tupu tena kitaalamu kitu ambacho "bosi mkubwa" hapendi.
 

PASKALI uko sahihi kabisa ....Kurugenzi ya Mawasiliano na Mkuu wa Itifaki wana kila sababu ya kuwajibika kwenye hili labda tu kama ataamua kuwabeba ...lakini kiuweledi wamekosea sana ......Rais alionekana kama mtu aliyeamshwa usingizini ,na kama binadamu alionekana kuwa mtu aliye katika taharuki kama mtu ammbaye hajaandaliwa kabisa kutoa tangazo hilo kwa kufuata msingi ya contents kikatiba .. tena angetakiwa atoe tangazo hilo akiwa amesimama .
Tangazo la kifo cha kiongozi hutanguliwa pia na wimbo wa Taifa ...na ikiwa ni kiongozi aliye madarakani kabla na baada ya tangazo nyimbo za jeshi huendelea kupigwa kwa muda kadhaa kabla ya programu zingine kuendelea
 
Kama kawaida unanapenzi kweli na corona
 
Hili na mie kidogo nilianzishie uzi, nikaona nisianze kutoa lawama mzee wetu bado hajapumzishwa. Nililiweka kiporo. Ila kiukweli Magu alikuwa kama hostage anaomba msaada wa kuokolewa toka kwa mateka wake kwenye ile kideo.
Yaani hii kurugenzi ni hovyo kuwahi kutokea. Nadhani tatizo pia viongozi wake ni wapuuzi, wanafanya kazi kwa ushabiki badala ya kitaaluma, hivyo hawanaga ushauri kwa raisi. Niliwaza ile habari angeitoa Majaliwa, angetokea ki- stateman zaidi.

Jamani, serikali ina kitengo maalum ambacho huwa kiko tayari saa zote kwa ajili ya misiba ya kitaifa, hata inayotokea gafla.
Hili taifa linaviongozi kadhaa wanaikimbiza miaka 100, lazima siku zao za kuishi zinahesabika na hicho kitengo kinatakiwa kiwe tayari wakati wote.

Isitoshe tayari tuna archive ya jinsi akina Mkapa walivyohandle kifo cha Mwalimu. Yaani Magu hata kumgeza Mkapa alishindwa? Alitakiwa awe ameandika chini alichotakiwa kusema badala ya kujikanyaga kanyaga, kiasi kwamba mtazamaji unaotea anachokwenda kukisema kabla hajakisema.
Wakati anaanza kuongea nilihisi ni ishu itamhusu Mzee Mwinyi, sababu ya umri. Lakini aliposema `` tumepokea habari za kusikitisha, kwamba mzee wetu ....Mkapa, leo...´´ nilijua tu Mkapa katuaga kabla Magu hajatamka. Kwakweli ilikuwa poor delivery.
 
Ukiona jinsi Mkapa na sumaye walivotangaza musiba wa Nyerere Tena kavaa official na wimbo wa taifa ukapigwa ilionyesha u serious wa tukio Mimi kuona mheshimiwa anatangaza ya Mkapa I thought was a joke kwa kweli,hyo kurugenzi wajiangalie
Magufuli katangaza msiba wa rais mstaafu kama msiba wa msela wa bar.

Hajafanya fair kabisa
 
nasisitiza tu "TUCHAPE KAZI"
Niliandika sehemu "watz mpaka tushtuliwe!" Sina mengi ya kuongeza zaidi ya hilo.
 
Kura moja kawe
 
Hata mm niliona kama hakujiandaa as if ametoka kugegedana chap akaibukia live kutangaza kifo. Proper way ingekuwa SAA 12 ASUBUHI AKIWA SAMBAMBA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WENGINE. ILE AMEKAA KWENYE SOFA LAKE LA CHUMBANI HAIKUWA SAWA.

NAUNGA MKONO HOJA.
Nilishangaa kuona socket za umeme nyuma yake
 
Hizo taarifa muhimu na sheria inatamka wazi wazi kuwa rais rasmi aseme mahali alikofia na sababu za kifo chake.

Ndiyo maana nasema sheria imevunjwa rais anatoa taarifa za msiba wa kiongozi wa nchi kama anatoa msiba wa kitoto kichanga.
 
Magufuli katangaza msiba wa rais mstaafu kama msiba wa msela wa bar.

Hajafanya fair kabisa
Simlaumu Mh. Rais katika hili, kwake ilikuwa ni shocking news alipaswa kufarijiwa kwanza na kuandaliwa vema kabla hajatangaza rasmi msiba huo mkubwa. Kwa tuliokwishafiwa watu muhimu ndani ya family tunalitambua vema hili.
Unaweza mpigia simu mtu wa mbali ukamsahau aliye jirani nawe.
 
Ila una vituko!!
 
Hospitali ya Dar es Salaam ni ipi ?
 
Pascal Mayalla,

Kwa mitandao ya sasa, mida ya saa kumi na mbili asubuhi hiyo isingekua taarifa tena kwa umma maana nchi nzima saa saba au nane ingekua imeshajua! Labda hii ingekua tamko tu la rais ila sio taarifa!

Kuna mida codes tupa kule.
Pia Kwa Mila zetu za kiafrika sidhani mbwembwe zilikua ni necessary, after all haijaondoa fact kwamba kafariki na sio kila mmoja wetu analalamika jinsi alivyopata taarifa..waandishi wa habari nyie ndio mliosomea hayo Mambo ya proper presentation but the rest of us can not care less..NOTe; KAZI ya mkurugenzi wa mawasiliano pia hufanyiwa lobbying na ninadhani kila mwanahabari angependa kupata nafasi Ile na ikibidi Kwa kuonesha udhaifu wa incumbent.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…