Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu lawamani. Inahitaji kusaidiwa kumsaidia Rais - Jicho Letu Ndani ya Habari

Kuna kitu kinaitwa institutional reporting and narrative taratibu sio kigezo vile isipokuwa interface kati ya active institutional na audience.

Kwa ivyo kwa mtazamo wa Ikulu walichokifanya ni kuonyesha kiasi gani msiba umewagusa na ulimwengu utawaelewa kwa sababu habari yenyewe sio for local audience only but international too.

Hayo ndio kama malalamiko ya Ulimwengu kuhusu udikteta wa Mkapa uwezi kufanya kazi magazeti ya serikali kama unataka kuwa critic wa serikali; similarly uwezi kuandika kwenye gazette la WHO kama wewe unataka ku-promote mitishamba. Unapozuiwa kufanya ivyo na mhariri sio udikteta ni kwamba kazi yako aiendani na institutional narrative.
Hivi unadhani kuvaa malapulapu au hovyohovyo kwenye msimba ndio uthibitisho kuwa unamachungu sana au??
 
Natazama YouTube Tangazo la Kifo cha Baba wa Taifa kilichotangazwa na Rais Mkapa, namuona Omary Ali Juma na Sumaye pembeni. Lakini naiona speech ya Rais katika tangazo la Kifo hiko.

Kabla sijamaliza kuisikiliza ghafla natazama tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa kilichotangazwa na Mheshimiwa Rais wetu (Sitaki kujadili sana juu ya tangazo hilo)

Nikirudi kwa tangazo la Kifo cha Mwalimu,

Mkapa alitieleza, Lini Mwalimu alikufa (Saa na muda) Wapi Mwalimu amekutwa na umauti, lakini akatueleza pia nini kimesababisha Kifo cha Mwalimu. Akatutia nguvu (Watanzania wote) akatutaka tuwe na Mshikamano, yeah niliiona Sura halisi ya Mtangazaji. Content ya Tangazo unaiona hasa.

Anyway ninyi mnaweza kutafakari msiseme sana

Fundi Mkuu
 
Ina maana mpaka sasa hujui kafia wapi or how long did it take you to learn that.

It was a developing story mengine yanafuata kadri muda unavyosogea.

Ulishaambiwa hospital Dar inatosha labda awakutaja kwa sababu maalum pengine watu wangeweza jazana hospitali usiku wa manane na hakukuwa na security (for crowd control purposes) who knows the exact reasons.

Ikulu awakukurupuka kwa hili wameonyesha weledi mkubwa sana.
 
Nyerere alikufa kabla Mkapa hajaingia second term of his presidency, Mkapa naye kafa kabla Magufuli hajaingia second term of his presidency!
Mkapa alikuwa kijana wa Nyerere na Magufuli ni "kijana" wa Mkapa.
Daaaaa.....mnyie jamaa😀😀
 
Hakuna hata moja la msingi katika waliyoeleza ndiyomaana enzi hizo Marehemu BMW aliwaambia waandishi wengi tz wanabore,niwazito nakweli has Hawa wa star tv
 
Ni mwendelezo wa ushamba na ulimbukeni.......
Niseme pia kutangaza ule msiba usiku ule ule kuliharibu sana ratiba za kesho yake Ijumaa ambazo zilishapangwa na kuandaliwa kwa ghsrama! Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kiliahirisha majafali yaliypkuwa yafanyika ijumaa hiyo hiyo asubuhi! Ona sasa hofu ya baadhi ta viongozivwa taasisi wameahirisha jambo ambalo halikuwa lazima kuahirisha. Graduation ilikuwa yacwatu wachache na ingeweza kufanyika bila shamrashamra pale ukumbuni mlimani city. Baadaye watu waendelee na shughuli zao na sgerehe zao kwacwale waliokwisha andaa sherehe na kusafurisha ndugu kutoka sehemu za mbali!
 
Watanzania kwa lawama hatujambo,angechelewa wanoko mkajua mapema napo mngepata la kuongea oooh mkapa ni kiongozi mkubwa kwann habari imechelewa kufikia umma.

Mimi sioni tatizo labda ungeongelea code tu maan uso unaonesha huzuni ya maumivu ya msiba....hayo mengine unataka uonekane tu umeongea .

Siku ukiacha unafiki brother ndo siku utaingia nafasi nzuri ya uongozi.

Point ni habari umepata .
 
Natazama YouTube Tangazo la Kifo cha Baba wa Taifa kilichotangazwa na Rais Mkapa, namuona Omary Ali Juma na Sumaye pembeni. Lakini naiona speech ya Rais katika tangazo la Kifo hiko.

Kabla sijamaliza kuisikiliza ghafla natazama tangazo la kifo cha Benjamin Mkapa kilichotangazwa na Mheshimiwa Rais wetu (Sitaki kujadili sana juu ya tangazo hilo)

Nikirudi kwa tangazo la Kifo cha Mwalimu,

Mkapa alitieleza, Lini Mwalimu alikufa (Saa na muda) Wapi Mwalimu amekutwa na umauti, lakini akatueleza pia nini kimesababisha Kifo cha Mwalimu. Akatutia nguvu (Watanzania wote) akatutaka tuwe na Mshikamano, yeah niliiona Sura halisi ya Mtangazaji. Content ya Tangazo unaiona hasa.

Anyway ninyi mnaweza kutafakari msiseme sana

Fundi Mkuu
Sas mkapa c muandishi wa hbr jmn kwahvhyo jiwe yey Ni sahii kbsa alivyofanya. Coni kosa au mnatak. Nafsi ya msigwa nn
 
Nadhani hapo mnazungumzia protokali za Rais kama taasisi,ila Rais kama anko Magu mwenyewe najua ameumia sana kuondokewa na jembe lake asingeweza kufanya yote hayo kwa mshtuko alioupata.
 
Nadhani hapo mnazungumzia protokali za Rais kama taasisi,ila Rais kama anko Magu mwenyewe najua ameumia sana kuondokewa na jembe lake asingeweza kufanya yote hayo kwa mshtuko alioupata.
sio ameacha baadhi ya details makusudi ili badae aje aseme mwenyewe ?
 
Wanabodi,
Naangalia Kipindi cha Jicho Letu Ndani ya Habari, kipindi kinajadili Msiba wa Benjamin Mkapa.

Tangazo la Msiba lililotolewa na Rais Magufuli, Kurungenzi ya Mawasiliano Ikulu imelaumiwa kwa kutokumsaidia rais kikamilifu kutoa tangazo hili, hali inayotafsiriwa kuwa katika baadhi ya matukio, Kurengenzi hiyo inahitaji kusaidiwa na manguli wazoefu ili waweze kumsaidia rais Magufuli katika baadhi ya matukio.

Manguli wa Mwanza, Dotto Bulendu, Edwin Soko na Moses Mathews, wamesema kwa vile hii ni shocking news, kulipaswa kuwepo kwa muda kidogo wa kumuandaa rais Magufuli kutoa tangazo hilo kulitangazia kuanzia, timing, dress code na content za tangazo lenyewe.


Timing
Kwa vile msiba umetokea usiku, kutoa tangazo saa 6:30 usiku was not the right timing kwa Watanzania, news ya msiba ingekuwa held, halafu Wahariri wakaitwa Ikulu usiku ule, halafu Tangazo litolewe live saa 12:00 asubuhi, rais akiwa na VP na PM.
TCRA kutoa taarifa vyombo vyote vya habari vya k electronic kujiunga na TBC ili hiyo live itangazwe Tanzania nzima.

Dress Code.
Kuna mavazi ya kawaida mtu anaweza kuvaa katika tukio lolote, lakini kuna dress code ya msiba. Wanasema rais Magufuli alipaswa kushauriwa kutoa tangazo hilo akiwa amevaa a proper dress code ya tangazo hilo.

Contents za Tangazo
Tangazo la msiba wa kiongozi wa kitaifa linaongozwa na sheria ya Vifo vya viongozi, sheria imeweka contents za kisheria ambazo lazima liwe na vitu 6, likianza na National Anthem na kumalizika na National Anthem.
  1. Jina la Kiongozi ni nani
  2. Kifo kimetokea lini
  3. Kifo kimetokea wapi nchini, mkoani, safarini, nje ya nchi
  4. Mahali mahsus, kimetokea nyumba, hospitalini, safarini,
  5. Kama ni hospitalini, hospitali gani
  6. Sababu za kifo, kimesababishwa na nini, maradhi, ajali, usingizini, etc
Tangazo la rais Magufuli kutangaza kifo cha Mkapa, lilikosa, baadhi ya taratibu za tangazo muhimu kama hilo ikiwemo wimbo wa taifa, na taarifa muhimu za kisheria, hivyo kuleta sintofahamu kwa jamii.

Hajawahi kusikika kuwa Benjamin Mkapa anasumbuliwa na maradhi yoyote, hivyo taarifa kuwa amefariki hospitali ni shocking, hospitali gani na ameumwa nini, ni maswali ambayo taarifa ya rais ilikosa.

My Take
Kwa vile taarifa ya msiba ni shocking news, flaws ndogo ndogo katika tangazo la msiba huo, zinavumilika.

Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu inafanya kazi nzuri katika upashanaji habari wa shughuli za rais, lakini lazima itenganishe matangazo ya kawaida ya rais kwa shughuli za kila siku za kazi za rais na tangazo la taifa, Watu wa Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas walipaswa kuhusishwa, na kwa vile mimi sio mserikali kujua nani alihusika, kama Dr. Abbas alihusika na bado tangazo la rais ndio lile, hii inamaanisha Dr. Abbas anaelemewa naye anahitaji kuwekewa wasaidizi.

Kwa maoni yangu, japo sheria inatamka tatangazo litolewe immediately kunapotokea msiba, kama msiba umetokea usiku wa baada ya saa 6:00, then alfajiri ni immediately kulikuwa hakuna uharaka wa kukimbilia kutangaza usiku mkubwa huo huo ili kutoa nafasi kwa rais kutangaza in a proper way na kufanya mashauriano na watu wawili watatu ili kutoa tangazo kamilifu kisheria, kikanuni na kiutaratibu na sio kumuharakisha rais kutangaza huku he looks sleepy!.

Namalizia kwa kutoa pole kwa Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli, Familia ya Mkapa na Watanzania kwa ujumla, kwa msiba huu mkubwa wa rais Mstaafu, Benjamin Mkapa.

Paskali

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake!

Nchi hii ukiitaja corona unakuwa Kama umemtia mtu kidole jichoni,yaani tutalinda uzembe na maamuzi ya kipuuzi ya mtu kwa gharama zozote zile hadi yeye mwenyewe atakapokufa kwa corona ndo tutaanza kuusema ukweli
 
Watanzania kwa lawama hatujambo,angechelewa wanoko mkajua mapema napo mngepata la kuongea oooh mkapa ni kiongozi mkubwa kwann habari imechelewa kufikia umma.

Mimi sioni tatizo labda ungeongelea code tu maan uso unaonesha huzuni ya maumivu ya msiba....hayo mengine unataka uonekane tu umeongea .

Siku ukiacha unafiki brother ndo siku utaingia nafasi nzuri ya uongozi.

Point ni habari umepata .
Wabongo ndivyo tulivyo
 
Hata mm niliona kama hakujiandaa as if ametoka kugegedana chap akaibukia live kutangaza kifo. Proper way ingekuwa SAA 12 ASUBUHI AKIWA SAMBAMBA NA VIONGOZI WAANDAMIZI WENGINE. ILE AMEKAA KWENYE SOFA LAKE LA CHUMBANI HAIKUWA SAWA.

NAUNGA MKONO HOJA.
Ujuaji uliopo kwenye jukwaa Hili Kwa kweli!
 
Back
Top Bottom