Tangazo la nafasi za Kazi 1,904 kutoka Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma

Watu wa kilimo huwa hawana kaxi hasa huko halmashauri huwa wanakaa juu ya meza na kupiga stori tu .
Basi utaziona za Kilimo pia, kama Suala la kukaa Ofisini na kupiga story Kili kada wanafanya hvyo acha wivu kwa wakulima.. unakwenda chooni kwa sababu ya wakulima..
 
Hongereni na kazi kwenu ili mjenge Taifa.
Mpatapo kazi mkumbuke kuwa wazalendo kwa nchi yetu... Wananchi tunawategemea sana.
 

Punguza mihemko mkuu,

Ukiangalia vizuri kwenye tangazo kuna nafasi 8 za Engineering and Construction, ama na wewe ulisomea uhandisi wa nini ?
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS, SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb.Na.JA.9/259/01/A/83 28 Mei, 2022

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI


Katibu wa Sekretarieti ya Ajira Katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Makatibu Wakuu wa Wizara, Watendaji Wakuu wa Idara Zinazojitegemea, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa
Halmashauri za Jiji/Manispaa/Miji na Wilaya anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania
wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi Elfu moja mia tisa na nne (1904) kama ilivyoainishwa katika
tangazo hili.

1.0.1 AFISA UTALII DARAJA LA II (TOURISM OFFICER II) - NAFASI 9

1.0.2 MAJUKUMU YA KAZI


i. Kukusanya taarifa za maeneo mapya yenye vivutio vya utalii kwa kushirikiana na wadau wote;
ii. Kutoa Leseni za utalii kwa mahoteli na wakala wa utalii ;
iii. Kukusanya na kuweka takwimu za watalii na safari za kitalii;
iv. Kutafuta na kupanga nafasi za masomo ya utalii ndani na nje ya nchi;
v. Kujibu malalamiko kutoka kwa watalii;
vi. Kutoa ushauri wa kitalaam kwa wadau katika uendeshaji wa Biashara ya utalii;
vii. Kuandaa kaguzi mbalimbali za Wakala wa utalii;

2
viii. Kuchambua miradi ya wakala wa utalii na hoteli;
ix. Kukagua hoteli, loji na migahawa;
x. Kujibu na kufuatilia malalamiko yanayoletwa na watalii;
xi. Kukusanya takwimu za watalii kwenye sehemu/vituo nchini vya kuingilia na kutoka wageni;
xii. Kutunza Kumbukumbu za vitabu/majalada ya Maktaba ya Utalii;
xiii. Kukusanya taarifa ya kila mwezi ya takwimu za watalii walioingia nchini na mapato
yaliyopatikana;
xiv. Kufanya tafiti ndogo “Survey” kwenye Hifadhi za Taifa na maendeleo tengefu ili kupata idadi
kamili ya Hoteli au Loji zinazotoa huduma kwa watalii;
xv. Kufuatilia kwa karibu na kusirikiana na VETA juu ya maendeleo ya vyuo vinavyotoa mafunzo
ya utalii nchini;
xvi. Kuratibu miradi yote inayohusiana na utoaji wa mafunzo ya utalii;
xvii. Kutayarisha ripoti ya mwezi,robo mwaka na za mwaka mzima;
xviii. Kufuatilia kwa karibu maendeleo ya Sekta kwa kufanya survey;
xix. Kuitisha mikutano ya Tourism Facilitation Committee;
xx. Kutayarisha ripoti na kusambaza kwa wajumbe na kutuatilia utekelezaji wa maazimio;
xxi. Kupitia miongozo inayohusu “Tourism Facilitation Committee;
xxii. Kuratibu shughuli za kubuni vivutio vya utalii na mienendo mipya ya kuendeleza utalii;
xxiii. Kutayarisha na kuhakiki vivutio vya utalii nchini;
xxiv. Kuitisha mikutano/semina za uhamasishaji kuhusu uendelezaji utalii;
xxv. Kushiriki katika kupitia ripoti za EIA kuhusu miradi ya utalii;
xxvi. Kushirikiana na Mashirika/taasisi mbalimbali za mazingira katika shughuli zihusuzo utalii na
mazingira; na
xxvii. Kukusanya rasilimali za uendeshaji katika vyanzo vya ndani na nje.
1.0.3 SIFA ZA MWOMBAJI

3
Kuajiriwa wenye Shahada/Stashahada ya juu katika mojawapo ya fani za Utalii au Hoteli kutoka
katika vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

1.0.4 NGAZI YA MSHAHARA
Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D.

1.1.1 AFISA WANYAMAPORI DARAJA LA II (GAME OFFICER II)-NAFASI 20

1.1.2 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kutekeleza kazi za ushirikishaji wadau katika uhifadhi;
ii. Kudhibiti utoaji wa leseni za biashara ya nyara na vibali vya kukamata wanyama hai;
iii. Kushiriki katika kusuluhisha migogoro ya matumizi ya wanyamapori;
iv. Kudhibiti matumizi haramu ya leseni za uwindaji na kuhakikisha kufuatwa kwa maadili katika
kutumia wanyamapori;
v. Kuthibiti matumizi haramu ya wanyamapori;
vi. Kufuatilia utekelezaji wa miongozo mbalimbali ya uhifadhi wanyamapori;
vii. Kuhakiki viwango vya kukamata wanyama hai kwa ajili ya biashara na ufugaji;
viii. Kufanya kazi za kuzuia ujangali;
ix. Kukusanya taarifa, na takwimu za Uhifadhi; na
x. Kutekeleza kazi za uhifadhi katika Mapori ya Akiba.

1.1.3 SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wenye Shahada ya Sayansi ya Wanyamapori kutoka Chuo kikuu kinachotambuliwa na
Serikali.

1.1.4 NGAZI YA MSHAHARA

Kwa kuzingatia ngazi za mishahara ya Serikali TGS D.

1.2.1AFISA LISHE DARAJA LA II (NUTRITION OFFICER II) - NAFASI 70

1.2.2 MAJUKUMU YA KAZI

i. Kukusanya taarifa na takwimu za lishe kutoka kwa wadau na makundi mbalimbali na kutoa
ushauri kuhusu lishe bora katika ngazi ya wilaya;

ii. Kuchambua takwimu za lishe na kuandaa taarifa ya watoto na makundi mengine yenye lishe
duni;

iii. Kushiriki katika kuandaa mipango na bajeti ya lishe katika ngazi ya wilaya;
 
Nafasi 1904.

Na hakuna sehemu naweza apply.
Hata mimi hapo sina nafasi lakini zipo nafasi mama alishazitoa na nishaziapply nasubiria...kama zile za TRA. Hivyo elewa hizo post zinawafaa wenzetu ambao hawajaitwa zile zingine kama za TRA. Sikutegemea eti daktari wa mifugo aone post yake TRA.
Hakika mama Samia anachokifanya Mungu atamlipa mema zaidi. Tunamuombea kwa roho yake nzuri na kuwapenda waTanzania wenzie.
 
Acha kulia lia njoo gulf countries upige kazi zenu za mainjinia nje nje.We endelea kujifungia tu hapo.
 
Mimi tangu nimalize chuo hakuna post ambayo nimeweza kuomba
 
We m
Punguza mihemko mkuu,

Ukiangalia vizuri kwenye tangazo kuna nafasi 8 za Engineering and Construction, ama na wewe ulisomea uhandisi wa nini ?
What's 8 jobs to hundreds of thousands engineering graduates in the streets ?
Mbona TRA huko wanatoa jobs in their thousands ,are accountants more valuable than engineers?
 
What's 8 jobs to hundreds of thousands engineering graduates in the streets ?
Mbona TRA huko wanatoa jobs in their thousands ,are accountants more valuable than engineers?
Punguza kujilizaliza humu ndani as if sisi wasomaji ni mama au bibi zako.
 
Afisa Tawala ✔

Afisa Biashara ✔

Afisa Habari ✔

Afisa Usafirishaji ✔


Any way, au basi tu.
Afisa biashara hapo naona wamesema mtu aliyesoma Masoko ila ukiingia hapo inagoma imekaaje hii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…