Tangazo la vodacom "nimeshinda nimeshinda"

Tangazo la vodacom "nimeshinda nimeshinda"

Hakya nani tangazo limekaa ki darasa la pili lilee!! Kwanza waigizaji wameshindwa kabisa kuvaa uhalisia! Alieshinda anaonekana ali concentrate na camera badala ya maudhui!! Kwenye hali ya kawaida hakuna lecture anaeweza kukubaliana na hali kama ile, ati ameshinda then anarudi kukaa na ticha anaendelea!! Pale ilitakiwa wanafunzi na mwl wote wahamaki na issue ya kitabu kukatishwa au tisha amtoe nje aloshinda buku liendelee!! Wenzake sasa, hawana mwamko kabisaaa!! JAMANI TUPENI AJIRA NA SIE HUKU TUNAWEZA ILA HATUNA MA GODFATHER!!!!!
 
Ukiangalia idea ni nzuri ila tatizo ni poor camera work, poor acting, poor quality....yaani no creativity at all.

Wao voda wamejitahidi kutoa fursa kwa wabongo, ila tatizo la wabongo ni kwenye utendaji...tunachojua ni siasa na mboyoyo miiingiiiiiii...

Next time wakitoa kazi kwa kampuni ya nje tunaanza kulialia.

Tujifunze kwa citizen hapo jirani tu.....yaani matangazo yao ni burudani tosha.


.......................Nikuone na simu mkebe tena................
 
wanafunzi wa chuo wanafundishwa hawana hata meza za kuandikia utafikiri wapo tuition
 
Ni tangazo zuri sana ila ikifika wakati dada anasonga nini sijui huwa natazama kando. Hakuwa na sababu ya msingi ya kucheza vile
 
waliotengeneza tangazo waliwekwa kindugu. ndo mana blunders haziishi
 
hongera vodacom kwa kutimiza malengo
 
Lile la taarifa ya habari "Nimeshinda nimeshinda"
yule dem anaweza kuwa kabila gani?
Maon si matusi
Wewe unadhani unafanya mzaha lakini unapanda mbegu ya ukabila polepole bila ya kutambua tukosoe bila kutaja makabila na imani jamani!
 
Mimi na mke wangu hatulipendi vibaya sana hili Tangazo. Likianza huwa tunazima TV. Naomba waliache mara moja na walete lingine.
 
tangazo la kijinga sana lile....akili ya matope kabisa!!!!!!!!
 
Wewe unadhani unafanya mzaha lakini unapanda mbegu ya ukabila polepole bila ya kutambua tukosoe bila kutaja makabila na imani jamani!

wala hakuna ukabila hapo ni swala la kucomment tu, Tanzania bado san ishu ya ukabila mkuu
 
Mimi na mke wangu hatulipendi vibaya sana hili Tangazo. Likianza huwa tunazima TV. Naomba waliache mara moja na walete lingine.

inabidi mtafute njia mbadala maana kuzima tv inaweza kuungua ikawa shida tena
 
Back
Top Bottom