Tangazo Maalum: Mradi wa Kazi Majuu!

Tangazo Maalum: Mradi wa Kazi Majuu!

Status
Not open for further replies.
- Wakuu wote JF, bila kumbagua yoyote nina rafiki wa kike wa kizungu ...

yani huyo dada kuwa mzungu ndio one of the qualifications? Wabongo baado tuna mental slavery ... everything white is good. Tutaendelea kweli jamani?😕

Mwanangu, unavyo endelea kuitete hilo dili unazidi kujidharaulisha...
 
Bonge,

Endelea na hatua ya pili $ 300 kwa Mr Mpala!

we humpendi mwenzio sasa... nilipotoa onyo awali watu walidhani najaribu kuwaharibia; ndio maana nikaja na kusema mwenye kufikiri hii ni bahati aende kubahatisha.
 
Yo Yo Kuna shori matata sana hapa mtaani amemaliza Mzumbe, nimemchomekea kuna nafasi za kazi majuu....sasa kwa kuwa wewe uko karibu na FMES ongea naye atupatie hizo $ 300, tuapply kwa ajili ya huyu mtoto...huwezi jua kinaweza eleweka mbele ya safari...

Chonde chonde

Mzee Masa
tehe tehe tehe mkuu mwambie awe na subira tunasubiri jibu toka Florida
.....tufunge mkanda.....
 
we humpendi mwenzio sasa... nilipotoa onyo awali watu walidhani najaribu kuwaharibia; ndio maana nikaja na kusema mwenye kufikiri hii ni bahati aende kubahatisha.
wewe nawe ....mbona umempa thanks? mie nimeitoa....kuonyesha hukubaliani na dili hili fake kaiondoe thanks
 
Jamaa anajaribu kuifanya eti iko for real, baharia wakati mwingine anapotea....vipi lakini sijakusikia kwa masaa kadhaa upo poa?

Changa la macho tu hilo au ndo itakula kwako ukijiingiza mkenge!..
Haya kwa vile wewe na huyo sista+Yo Yo kwa vile bado mnasubiria jibu, endeleeni kutega masikio..
Mimi nipo, majukumu tu ishalaah naendelea vyema..
 
Mimi nadhani tuliangalie jambo hili objectively. Wengi wetu tumeona watu wakitapeliwa au tumekuwa victims wa utapeli wa style hii na hivyo basi tuko consious enough ku-avoid matokeo ya once beaten twice na tuko chonjo kuhakikisha kwamba wengine hawaingii kwenye mkenge.

Hata hivyo sio kila tangazo la aina hii nilakitapeli ingawa ni vigumu kutolihusisha. Cha msingi ni kupata information za kutosha kutoka kwa organization husika ili kujiridhisha juu ya uhalali wa tangazo na asasi husika.

Mambo mawili yanahitaji uangalifu katika kutafakari jambo hili. Moja ni information ambazo FMEs anazo na hajazitoa JF vs zile alizozitoa. FMEs anaonyesha kuridhika kwamba ziko information zinazokosekana katika tangazo lake na kwamba yuko tayari kuzitoa kwa njia ya PM. Kutokana umuhimu wa data ambazo hazijatolewa kwa potential candidates na udhahifu wa sababu alizozitoa FMEs za kutoweka information zote hofu ya utapeli kwa potential candidates imeongezeka.

Takriba members wote JF tumevaa vinyago, na maombi ya kazi husika yanahitaji vitambulisho halali ambavyo hatupendi kuvitoa JF. Akiwa anajuwa hili, Mkuu FMEs alitakiwa aanike kila kitu hadharani ili mwombaji kazi husika HASIJITAMBULISHE KWA FMEs na badala yake aendelee kuvaa kinyago JF huku akisaidiwa na JF kupita FMEs kupata kazi. Mkuu FMEs amedai kwamba hawezi kuanika kila kitu kwani JF inapitiwa na watu kama mabalozi nk, swali ambalo ningependa kumuuliza mkuu FMEs ni kwamba anajuwa vipi kwamba watakao omba information kwa PM nao si watu ambao hataki wasome kila kitu ambacho angekianika? That tells me FMEs may have tools to indetify who is who in JF, mana vinginevyo angeweza tu kuwasiliana na JF members anaowafahamu kwa majina na kuwapa tangazo hili. Kadhalika guarantee aliyotoa FMEs ku refund $300 za watakao tapeliwa haina mantiki yeyote kwani kwenye JF FMEs anatambulika kwa kinyago chake na sio kwa kitambulisho chake. Kwanza kinyago chake miaka ya awali kilikuwa ni Sam, kikaja kuwa Es kabala JF haijampa uongozi wa wapiganaji katika safu ya mashambulizi (FMEs). Ili refund policy ya mkuu FMEs iwe valid ni dhahiri kwamba FMEs na mwombaji kazi lazima wabadirishane vitambulisho halali. Na hii inaongeza maswali: kwanini wana JF tutambulishane? Kwanini ili nisaidiwe ni lazima nijitambulishe kwa FMEs? Je faida za msaada ni kubwa kuliko hasara za kutambulika kwangu na FMEs? Hata kama organization sio ya kitapeli, kazi za vinyago vyetu na kutotilimilika kwa information alizotoa FMEs na zinatisha potential candidates.

Jambo la pili ambalo linatakiwa uangalifu ni masharti ya kupata kazi. Hapa naongelea dola 300. Ni vyema tukajiuliza kama hii ni kawaida katika upatikanaji wa ajira katika mazingira huru. Cha ajabu utapeli wa aina hii MARA NYINGI uhusisha ajira wa kwatu wa nchi masikini za Afrika. Tujiulize. Website nyingi USA na Canada za serikali na NGO zimekuwa zikionya watu kuto omba ajira katika mashirika au kampuni zinazotoza waombaji wanapopeleka maombi kwa madai kwamba kampuni au mashirika ya aina hiyo ni yakitapeli. Uki google maneno kama "online job scams" au "avoid online job application scams" utakutana na website kibao zinatoa maonyo na namna ya kupambana nayo.

Lakini haya yote yasiwe sababu ya kumshutumu FMEs kwa sababu kuu tatu (a) labda na yeye hakujuwa na alitoa tangazo akiamini anawasaidia watu (b) labda maswali yetu na wasiwasi wetu unaweza kujibiwa na information ambazo FMes hajazitoa (assuming ipo siku atazitoa), (c) makampuni au asasi za kitapeli hazina utofauti kiutendaji na kampuni au asasi halali (in fact ndio maana tunatapeliwa), hivyo basi yawezekana organization anayoisema FMEs ni halali.

Hitimisho ni kwamba FMEs anatakiwa afanye kazi ya ziada kutuaminisha juu ya uhalali wa organization, pia atuambie namna ya kupata information zaidi bila kuvua vinyago vyetu mbele ya kinyago chake.
 
- Wakuu wote heshima mbele sana, ndio kwanza nimemaliza shuguli zangu, sasa niko njiani kurudi home, I got all the info nilizozitaka sasa ninahitaji kuzi-diggest na kuwasajili watu wangu watatu kwanza, mpaka nitakapomalizana na hawa watu wangu ndio nitatoa info zaidi, ninafanya hivi ili kuepusha mwananchi yoyote mwingine kuibiwa au kudhulumiwa kwa sababu hawa watatu nitawalipia mwenyewe kwa hela zangu,

- Info za mwanzo zilikuwa nusu nusu, nyingi hazikuwa straight kama nilivyojionea huku bondeni, ni processs ndefu na ngumu kidogo kuliko ilivyokuwa imewekwa, kwenye msafara wa mamba huwa kuna kenge, na hata huku kwenye hii deal pia kuna makenge na yote nimeyaona wazi mwenyewe,

- Sitegemei mtu yoyote atatuma dola 300 kama mwenda wazimu hilo nimewaonya wale wote niliongea nao kwa simu, kwa hiyo nimeamua ku-experience mwenyewe kwanza, which is what I should have done from the beggining, maana naona hii hatred ninayoiona hapa JF is just incredible, ninajiuliza ni kwa kosa gani hasa? Anyways, wakuu wengine wote nimewasikia, na sasa nimeamua kuyaoga haya maji mwenyewe kwanza and then nitawaarifu matokeo huko mbele ya safari.

Ninaheshimu mawazo yote yaliyokwisha tolewa, na ninawashukuru wananchi wote ambao tumekwua intouch in the last four days on this ishu, ninaheshimu mawazo ya kila mtu, ila binafsi I am moving forward na nitatoa matokeo yatakapopatikana, kwa mwenye tatizo zaidi anaweza kunitafuta nipo, sijawahi kukimbia maswali wala wajibu. Nimeona matusi mengi na kashfa za bila kosa, lakini tunasinga mbele wakuu ninaanza mwenyewe kwanza nikiliwa nitasema wazi kuwa nimeliwa!

Respect na Mungu Aibariki JF.

Field Marshall Es!
 
Hitimisho ni kwamba FMEs anatakiwa afanye kazi ya ziada kutuaminisha juu ya uhalali wa organization, pia atuambie namna ya kupata information zaidi bila kuvua vinyago vyetu mbele ya kinyago chake.

- Mkuu ahsante sana kwa busara nzito ulizonazo, Mungu akubariki na ubarikiwe sana. I must admit mbele ya huu umma kwamba I was wrong kuweka hizi info hapa, maana this is crazy man sasa nitaweka tu zitakapotokea results, ili kuepusha confusion samahani wakuu wote kwa usumbufu, lakini in all this kuna wananchi wengi wa Tanzania nilioongea nao kwa simu one on one, ninawaahidi tu kwamba watulie na nikiwa through nitawatafuta mwenyewe namba zenu ninazo.

Again samahani sana kwa usumbufu wakuu, ila tu nime-notice tu hii hatred ya ajabu sana, naona ni kwa sababu ya misimamo yangu kwenye jukwaa la siasa, haiwapendezi wengi, naona mngependa wote tuimbe wimbo mmoja. Anyways nitachukua a timeout kuchangia huko kwenye siasa ili niweze ku-review kama ni worthy kuendela kuchangia, maana hii ni chuki ni deep na ni serious na imenishitua sana, ninawatakia mijadala ya amani wakuu.

FMEs!
 
- Wakuu wote heshima mbele sana, ndio kwanza nimemaliza shuguli zangu, sasa niko njiani kurudi home, I got all the info nilizozitaka sasa ninahitaji kuzi-diggest na kuwasajili watu wangu watatu kwanza, mpaka nitakapomalizana na hawa watu wangu ndio nitatoa info zaidi, ninafanya hivi ili kuepusha mwananchi yoyote mwingine kuibiwa au kudhulumiwa kwa sababu hawa watatu nitawalipia mwenyewe kwa hela zangu...


Field Marshall Es!

Hao watatu itakuwa mzigo ($900) kuwasajili, lakini nakutakia kila la heri nguyangu. Mizimu ya mababu zetu ikuongoze na kukulinda, Afrika.
 
- Tunaongozwa na Mungu mkuu na sio anything else!

Respect.

FMEs!

Aah, yule mwenye malaika weupe weupe, eti? Sio mizimu ya mababu zetu ambayo walituambia ni primitive, si ndio mwafrika mwenzangu?

Hivi wako uliletewa na nani? Warabu au wazungu (missionaries)?


I am sorry, but I could not let this pass - everything white is good, everything black is evil!
 
Ndugu yangu FMEs, uwe unajaribu ku-analyze unayoombiwa na watu, watu wengine wana critisize sio for nothing, kuna watu wameshapigwa na hao jamaaa na wako humu ndani ya JF lakini hawawezi kusema wamepigwa , sasa wanakuwa wakali kukwambia kama hao jamaa sio 'kwa faida yako' na hao jamaa zako, isije ikawa hawa jamaa wakala visent vyako unavyovitafuta baharini kwa taaabukitu kingine lazima ukiweke kwenye akili yako kama hiyo organization ni ya muda mrefu na kuna watu wengi humu kutwa wanashinda kwenye mitandao ni lazima washacome-across na hiyo kitu, hapo cha muhimu ni kumwambia huyo rafiki yako wa kidhungu "SIDANGANYIKI"
 
Ndugu yangu FMEs, uwe unajaribu ku-analyze unayoombiwa na watu, watu wengine wana critisize sio for nothing, kuna watu wameshapigwa na hao jamaaa na wako humu ndani ya JF lakini hawawezi kusema wamepigwa , sasa wanakuwa wakali kukwambia kama hao jamaa sio 'kwa faida yako' na hao jamaa zako, isije ikawa hawa jamaa wakala visent vyako unavyovitafuta baharini kwa taaabukitu kingine lazima ukiweke kwenye akili yako kama hiyo organization ni ya muda mrefu na kuna watu wengi humu kutwa wanashinda kwenye mitandao ni lazima washacome-across na hiyo kitu, hapo cha muhimu ni kumwambia huyo rafiki yako wa kidhungu "SIDANGANYIKI"

- Kushinda mtandaoni na kuona kwa macho as I did ni vitu viwili tofauti.

Respect.

FMEs!
 
Nadhani somo limemuingia FMES angalau kidogo, ingawa ndio hivyo tena mtu mzima hakosei. Kila nnapoendelea kusoma post zake ni kama napata picha ya kwamba hata yeye ameanza kuwa muangalifu kidogo-kidogo, tofauti na mwanzoni ambapo alikuwa tayari hata ku-guarantee pesa za watu ikiwa watakosa nafasi.

Iliyopo tumsubirie atupe matokeo ya kuwajaribia hao ndugu zake. Mzee FMES ni mtu wa busara sana. Natumaini hatasita kutupa matokeo hata kama imekula upande kwake. Ikitokea amefanikiwa, basi ndio itakuwa wakati wa sisi wengine kula matapishi yetu.

Ila mzee FMES epuka ku-rush haraka haraka na kuchukulia kwamba mtu anaugomvi na wewe personally pale anapoku-criticize, na kumchukulia kila mwenye mawazo tofauti na wewe basi ni adui yako au ametumwa.
 
Unajua wengine hawajazoea kuwa criticized, sasa inapotekea hivyo wao huona ni kama personal attack! Ninafurahi hakuna mtu aliyesupport hii kitu na kukubali kuliwa $ 300 na hii SCAM
 
- Naona a lot of frustrations maana hakuna more info, kama nilivyosema yalikua ni makosa makubwa sana kuweka zile info hapa, nimeshawalipia watu wangu watatu, kama nilivyosema na wanaendelea na process.

- Itakapokuwa through nitasema na ikikwama nikaliwa hela zangu nitasema, ila for now sitatoa any more info, ambazo nimezikusanya huko bondeni.

Respect.

FMEs!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom