- Wakuu wote heshima mbele sana, ndio kwanza nimemaliza shuguli zangu, sasa niko njiani kurudi home, I got all the info nilizozitaka sasa ninahitaji kuzi-diggest na kuwasajili watu wangu watatu kwanza, mpaka nitakapomalizana na hawa watu wangu ndio nitatoa info zaidi, ninafanya hivi ili kuepusha mwananchi yoyote mwingine kuibiwa au kudhulumiwa kwa sababu hawa watatu nitawalipia mwenyewe kwa hela zangu,
- Info za mwanzo zilikuwa nusu nusu, nyingi hazikuwa straight kama nilivyojionea huku bondeni, ni processs ndefu na ngumu kidogo kuliko ilivyokuwa imewekwa, kwenye msafara wa mamba huwa kuna kenge, na hata huku kwenye hii deal pia kuna makenge na yote nimeyaona wazi mwenyewe,
- Sitegemei mtu yoyote atatuma dola 300 kama mwenda wazimu hilo nimewaonya wale wote niliongea nao kwa simu, kwa hiyo nimeamua ku-experience mwenyewe kwanza, which is what I should have done from the beggining, maana naona hii hatred ninayoiona hapa JF is just incredible, ninajiuliza ni kwa kosa gani hasa? Anyways, wakuu wengine wote nimewasikia, na sasa nimeamua kuyaoga haya maji mwenyewe kwanza and then nitawaarifu matokeo huko mbele ya safari.
Ninaheshimu mawazo yote yaliyokwisha tolewa, na ninawashukuru wananchi wote ambao tumekwua intouch in the last four days on this ishu, ninaheshimu mawazo ya kila mtu, ila binafsi I am moving forward na nitatoa matokeo yatakapopatikana, kwa mwenye tatizo zaidi anaweza kunitafuta nipo, sijawahi kukimbia maswali wala wajibu. Nimeona matusi mengi na kashfa za bila kosa, lakini tunasinga mbele wakuu ninaanza mwenyewe kwanza nikiliwa nitasema wazi kuwa nimeliwa!
Respect na Mungu Aibariki JF.
Field Marshall Es!