Kwa niaba ya mwenyekiti, naomba nitowe rai na pole kwa wale wote walio jeruhiwa na swala la picha.
Pili nipende kusema kwamba jf inaonekana kuvamiwa na vijana wasio na adabu na wasio na hekma hata kidogo, hali iliyo pelekea kukosa staha na kufanya mambo ya ajabu tena yenye kuitweza jinsia yetu.
Binafsi naamini wengi wapo humu wanao fahamiana, na pia kutofautiana ni jambo LA kawaida hata huku kwenye familia zetu, sasa linapo kuja swala la utashi, pengine hata inapo tokea kijana akamtongoza mdada humu na kisha kijana huyo ikitokea amekataliwa basi isiwe nongwa maana unapo zoza kuna kukubaliwa ama kukataliwa.
Kuanika picha ya mtu humu pasipo ridhaa yake, hilo ni jambo baya tena baya sana