Tangazo: Wauguzi wasio na leseni mpya kufutwa kazi

Tangazo: Wauguzi wasio na leseni mpya kufutwa kazi

Pumbavu sana Agnes Mtawa, kwakuwa upo hapo ofisini kwenye kiyoyozi wenzako wanawaa barakoa na fase maska hadi nyuzo zimekuwa sugu kama kisigino huku wakiambukizwa covid-19 na kujifia, wauguzi wamepata ulemavu wa kudumu kwa sababu ya maumivu ya migongo....na bado unataka walipe ushuru wa "kaisari" kwa jina la usajili!

Wauguzi msilipe hizo leseni hadi wawaambie tangu ada hiyo ianze kulipwa matumizi yake ni yapi, kulipana posho za vikao na ujenzi wa makao makuu KIFISADI? Hata kuanzisha Jarida la Wauguzi kwa ajilili ya kuwaelimisha walipa ada limewashinda! Aibuuu!
download.jpg
 
Hii sio nursing tuu bali watu wote walio somea afya lazima ulipie gharama ya leseni yako (usajili) haijalishi umeajiliwa au umejiajiri,(famasi, nurse, madactari, watu wa lab, mionzi, meno, n.k)

Sio ombi ni sheria ilitungwa na wabunge wenu bungeni na ikapitishwa, tulaumu wabunge wetu na sio watekeleza sheria

Saivi kama huna no ya usajili na leseni kuajiliwa serikalini sahau na baadhi ya hospital zinazo jielewa
 
Wauguuzi x2
Taratibu jamani hayaa
Tutaonana wabaya hayaaaa
Daktari na manesi wauguuzi
 
Kwa aliyesoma. Mchawi ada au in wanatakiwa kufanya interview upya ndio wapewe tena leseni?
Hao kila baada ya mwaka 1 au miaka 2 wanatakiwa kurenew leseni na kwa kulipa ada ya ambayo ni kati ya shiling 60,000 mpaka 70,000 na wasio na leseni huwa kuna mtihan unaoandaliwa na baraza la ukunga
 
Watakua wanataka mapato kutokana na ada ya leseni, hizi professional organization za tanzania ni upumbavu mtupu.
 
Baraza la wauguzi na wakunga TNMC la Tangaza kufuta kwenye daftari la usajili, wauguzi wasiokuwa na lesseni zilizohuhishwa na kukoswa kazi ndani na nje ya nchi.

Hayo yametanganzwa na Agnes Mtawa, Msajili wa Wauguzi TNMC

Hizo leseni mpya walipie tu. Na haya yote wameyataka wenyewe. Nilisikia hata walimu nao eti wanataka kutengeneza professional organization ili wawe na leseni zao za kuwatambulisha ili kuwazuia watu ambao hawajasomea ualimu kuingilia ajira zao.
 
Wazo zuri wangekomaa mpaka walipie kuliko kuwafutia usajili watu wanaokomaa na vidonda, covid 19 wapo harafu wakifa ni kiapo, likitokea janga wanawekwa mbele wakati mabosi wao wanakula viyoyozi kwenye ofisi, ingewezekana hata serikali ingewalipia lesseni kazi za hawa watu ni za hatari sana, wengi wanakufa kwa kazi zzao
 
Hizo wanatakiwa walipie wenyewe, mkuu.
Maana wanapenda sifa. Na hiyo kazi na yao. Waliochagua wenyewe.
 
Hiii kada bana huwa wanamaamuzi magumu sana lakini utekelezaji wake na utendaji ndio unashangaza maana kwa mfano mtu unataka awe analipia leseni kila mwaka na mtu huyo ajapata ajira yupo mtaani na hakawai kuitumia leseni yake sasa hii inakua kulipia kitu ambacho haukifanyii kazi kama utawafungia leseni waliopo makazinj sawa waangalie upamde wa pili pia
Hii kada kazi zake ngumu lakini mishahara sasa ndo utafurahiii
Sh ngapi mkuu, kuna dogo hapa kitaa ana kadiploma ka hiyo kada na nimwajiliwa pale BMC anatutambia sana ambao hatujapata vibarua rasmi. Huwa natamani sana kujua mpunga anaovuta!
 
Hahaa muulize maana kana ni binafsi kuna makubaliano mzee ila wa selikari inajulikana
 
Wambieni waache umaku tumewachoka hawa mbwa ajira hakuna nilipie lessen ili iweje
 
Ila kuna hospitali kumuona tu dakitari ni shailingi 50,000/=angalau zingine ni 12,000/= na zingine za rahisi ni angalau 4,000/= kwa kichwa sasa akipata vichwa 10 tu kwa siku mbona ni hela mingi tu?
Ndg hizo gharama za leseni ni deal za watu ambao wanajipa vyeo vya msajili nk. Lengo la leseni ni zuri tatizo ni hizo gharama kuwa kubwa sana. Ukienda wizara ya afya utakuta wamejipa kijiofisi na wameacha majukumu ya uuguzi wanatumia hizo fedha kujilipa tuvikao na tusafari twa hapa na pale. Unapokuwa unafanya kazi hospitali gharama ya kumuona daktari inaingia kwa mwajiri na sio kwako wewe subiri mshahara wako basi. Huu ni unyonyaji skwea
 
Leseni inasaidia nini kwenye taaluma ?! Hizo pesa zinaenda kuboresha mishahara ya wanataaluma au zinaenda wapi, ni nani mtumiaji wa mwisho wa pesa za malicious ya leseni hizi za kila mwaka?!

Wanaolipia leseni wanafaidikaje kwa kuzilipia?!

Kuna tofauti kati ya certification na licensing kwenye taaluma?! Kwanini wana taaluma wasiwe certified badala yake wanakuwa licensed?!

Mfanyakazi anakatwa kodi zote za mshahara na tena anatozwa license fee, hii inaenda wapi sasa?!

Maisha magumu bado tunaumizana.
 
Ndg hizo gharama za leseni ni deal za watu ambao wanajipa vyeo vya msajili nk. Lengo la leseni ni zuri tatizo ni hizo gharama kuwa kubwa sana. Ukienda wizara ya afya utakuta wamejipa kijiofisi na wameacha majukumu ya uuguzi wanatumia hizo fedha kujilipa tuvikao na tusafari twa hapa na pale. Unapokuwa unafanya kazi hospitali gharama ya kumuona daktari inaingia kwa mwajiri na sio kwako wewe subiri mshahara wako basi. Huu ni unyonyaji skwea
Ni kweli mkuu
Lakin hivi unadhani daktari hajui kama kila kichwa kimuonapo basi kimeacha consultation fees?na sidhani3kama hajui ni kiasi gani
 
Sh ngapi mkuu, kuna dogo hapa kitaa ana kadiploma ka hiyo kada na nimwajiliwa pale BMC anatutambia sana ambao hatujapata vibarua rasmi. Huwa natamani sana kujua mpunga anaovuta!
Hii roho mbaya sasa
 
Hizi ndizo baadhi ya utitiri wa kodi za ovyo ambazo Mh. raisi amekuwa akizisema na kuzifuta. Eti muuguzi ambaye mshahara wake kwa mwezi unalingana na posho ya kikao kimoja cha masaa manne cha mbunge, analazimika kulipa ada ya leseni ya uuguzi sh. 100000 kila mwaka. Kwa daktari ni sh 250000 kila mwaka! Yaani ni zaidi ya leseni ya udreva wa semi traila ambayo ni sh. 40,000 kila baada ya miaka mitano.

Huu uonevu nadhani JPM bado hajauona.
Mwajiri ndio hulipia hizo leseni tatito lako nini? kwani unatoa mfukoni mwako?
 
Mwajiri ndio hulipia hizo leseni tatito lako nini? kwani unatoa mfukoni mwako?
Nani kakwambia zinalipwa na mwajiri? Usijiingize kwa mambo ambayo huyajui.
Hizi ada zinalipwa na kila muuguzi toka mfukoni mwake, awe ameajiriwa au hakuajiriwa au amejiajiri mwenyewe au amestaafu! Hata kama miaka ya nyuma mtu hakuzilipa kwa sababu yo yote ile bado anatakiwa kuzilipa ili atambulike na kubaliwa kufanya kazi ya uuguzi au udaktari nchini. Wako wengi wa wauuguzi/ madaktari hawa wana malimbikizo ya mamilioni ya pesa na mabaraza haya ya serikali (Medical Council of Tanganyika na Nursing Council of Tanzania) na ni kwa mjibu wa sheria (mbovu) zilizopitishwa bungeni.

Serikali isikie kilio cha wauguzi/ madaktari wetu hawa. Wengi walipaswa kuwa walishafutwa kufanya kazi nchini hapa kwa sababu ya malipo ya leseni za ku practice kila mwaka.
 
Back
Top Bottom