Tangu 2013 alipohitimu anatafuta kazi, anaishi kwa wazazi, nimshauri vipi?

Tangu 2013 alipohitimu anatafuta kazi, anaishi kwa wazazi, nimshauri vipi?

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,406
Reaction score
19,375
Unajua kuna kipindi inafika sisi kama vijana tuwe tunaamka kiukweli, Ndio penye nia pana njia, washindi hawakati tamaa, bidii huzaa matunda, n.k lakini haya mambo yana mazingira yake.

Nina rafiki yangu alihitimu mwaka 2013 ana degree ya uhasibu (accounting) na diploma ya procurement, yupo katika harakati za kutafuta kazi tangu amalize chuo, Anaishi kwao kidogo wazazi wana uwezo na yeye ni mtoto wa mwisho.

Kiukweli miaka inaenda maana muda haugandi, yupo mwanzoni mwa miaka ya 30s ila kufumba na kufumbua anaweza fikisha 40 yupo hapo endapo hatafanya maamuzi ya kubadilika.

Biashara anayo ila pesa inaishis lwenye kununua mabando , kutuma cvs, kusafiri kufanya written interviews, n.k

Je, nimshauri vipi ili astuke
 
Mwambie akomae na biashara aombe pesa kwao akapangee aangalie life lake Ila usiumie sana kuna familia Baada ya watoto wote kuondoka kuangalia maisha Yao mbele wanaonaga ni vizuri abake mmoja nyumbani kuangalia wazazi na shughuli za nyumbani Moshi nimeona familia nyingi
 
Kuna watu wamezaliwa kwenye neema ila neema yenyewe hawaitumii au hawajagundua kuwa ni neema.

1. Una wazazi wote wawili na hawakutegemei kwa lolote
2. Wazazi wana wanakiji uwezo kidogo..
3. Una sehemu ya kulala na kula

Atumie hizi sifa 3.. then kesho asubuhi amke awahi sokoni aangalie watu wanavyotafuta hela kwa namna yake, atumie jicho lake la utambuzi kutafuta hela au shughuli ya kumuingizia kipato angalau buku kwa siku, Mdogo mdogo ataanza kuongeza,

Kama and biashara japo ni ndogo aifanye rasmi kuwa ndo kazi yake, then plan b iwe kutafuta kazi...

Asikwambie mtu... ushauri bora huwa wa nini cha kufanya inategemeana na nia yako ndani umetaka kufanya nini?
 
Tatizo ni kuwa si kila mtu anaweza fanya biashara.
Ila hili life bila kujiongeza na kuwaza nje ya box, na usipokuwa na bahati basi utasubiri sana. Tena bora yy hata wazazi wana uwezo.
 
Kama ni binti ani dm, kuna mahali wanahitaji mwanamke, awe tayari lkn kufanya kazi nje ya mkoa wake, aje nimwekeze atume maombi, ila awe jinsia ya kike
 
Tofauti yake me na yeye nu kwamba ye Yuko 30

Me bado 25.me bado nakula maisha kdg niacheni
We bado wakuache bhana wo tayr wamefikisha umri wa kuoa hta mi nakuunga mkono, japo kumbuka kutoka 25 hadi 30 haichelewi co usifike nawe 30 bado upo nyumban ila kwa saivi tulia tu mda bado unaruhsu
 
Mwambie aolewe tu
Kuna Mmoja Anemaliza Diploma Alipoona Hapati Kazi Akasema Bora Azae Huenda Milango Itafunga Mpaka Sasa Hivi Analea Mtoto Milango Migumu Haina Grease and. Anapambana Kulea
 
Ukimaliza chuo kama ulivo sema kutafuta kazi isizidi miaka 2 mpaka 3 na hapo mitatu kuwe na sababu labda umejishikisha au unamishe.
 
Labda ana sababu zake mkuu. Na kama ana biashara kabisa sio wa kumbeza kisa anakaa kwao, labda kachaguliwa alinde nyumba na kutunza wazazi.
 
Back
Top Bottom