Wewe jamaa ni kilaz.a sana na ninasikitika kama nchi tuna wataalam wa afya wenye fikra mfu kama zako, Tangu nimefuatilia mjadala huu sijaona hoja ya maana kutoka kwenu madaktari.
Daud1990, sijui una maana gani kuniita kilaza, lakini neno "kilaza" naelewa ni mtu ambaye ni mjinga. Hilo halina shida, tuseme mimi ni mjinga na wewe mwerevu.
Pili, hakuna sehemu yoyote nilishawahi kusema mimi ni Dr. Hakuna. Na nilimkatalia Deception kwamba mimi sio Dr. Lakini pia, hutendi haki kwa madaktari wa kitanzania. Hutendi haki. Mtu hawezi acha kutibu aje hapa aanze kujadili siasa za Deception, never. Kwanza huyo Dr. atakuwa anakinzana na Wizara ya Afya.
Hoja zenu ni Kutia watu hofu, vitisho na huruma na sio tafiti na research za kitabibu kama afanyavyo deception and the likes....
Daudi1990, Deception hana utafiti wowote wa kitabibu. Hana. anapinga kitu ambacho hawezi kuthibitisha. You tube ndiyo utafiti?. Leta hapa paper iliyoandika hayo mnayosema, achana na you tube za miaka ya 1980........ Leta hapa machapisho ambayo yanasema hakuna HIV.
Page 10 zilizopita kabla ya hii deception alikuuliza maswali Mengi sana ulikimbia mbio ndefu sana..
Sikuona umuhimu wa kuendelea kujibizana na mtu ambaye anasema hakuna HIV. Akaawambie wadogo zake hamna HIV na sio vijana wa kitanzania. Vijana wanateketea kwa virusi, nyie mnasema hamna! ili iweje? wakapige kavu? acheni hizo.
Napata shaka na elimu ya madaktari Wetu ,sina imani nao kabisa. Kuna mmoja Jana nilimuuliza anaweza kunithibishia by evidence kuwa amewahi kumuona HIV??? Majibu aliyonipa ni aibu .
Sasa hapo ndipo unapokesea. Kwanza kabisa nilishasema kwenye post zangu huko nyuma kwamba mimi sio daktari na sijawahi kuwa Dr.
Pili madaktari wa kitanzania ndiyo huwa wanakutibu ukiumwa. Tatu, hao Madaktari ndiyo waliomtibu Tindu Lissu mpaka akastabilise. Nne, hao hao Madaktari ndiyo walimtibu mke wa Rais Magufuli alipolazwa pale muhimbili. So have respect. Siasa zako na Deception usiwaingize madakatri wa kitanzania.
Msikilize Karry Mullis Mgunduzi wa Kifaa cha PCR ambacho unakitumia ila naamini hujui huyu Mzee ndio inventor akizingumzia myth za HIV
Pamoja na wewe mwenyewe kuweka video lakini hujaelewa ulichokiweka.
Dakika ya 9:06 huyo Karry amesema "PCR came right about the same time that HIV did and it was.........." mpaka hapo amekiri HIV ilikuja muda huo huo. Anaendelea "people started looking with PCR for HIV, that was the only way to see it" Anasema hivi watu wakaanza kutumia PCR kucheck HIV, ilikuwa ndiyo njia pekee ya kuona HIV.
Anaendelea kusema mwaka 1983 - kulikuwa na MaDR. 2 ambao walikuwa wanajua mambo ya HIV, mwaka 1985- kulikuwa na MaDr. 500 tu na mwaka 1986 kulikuwa na MaDr. 500,000 waliokuwa wanajua kuhusu HIV. Kwa maana hiyo msitegemee sana hizo you tube zenu za miaka ya 80, kwa sababu bado maDr. wengi walikuwa hawana ufahamu.
Mwishoni kabisa huyo Karry anasema academy ya science ya marekani ni bunch of idiots. Hawana tafiti za maana zilizoandikwa. Kila mtu anaruka ruka. Huyu anasema vile, huyu anasema vile. Ni siasa kwenye utafiti.
Kasikilize 16:42 Peter Duesberg anasema "Chemotherapy iligunduliwa 30 years ago long before AIDS was known to kill human cells" kumbe mnajua AIDS inaua human cells. hahahaha
Madaktari wa Tanzania mnatutia aibu someni Basi mbona vitu vipo mtandaoni
Msihusishe maDr. wa kitantanzia kwenye siasa zenu na Deception.