Tangu Deception aanze kampeni yake kuhusu UKIMWI, kuna yeyote humu ndani ambaye amemuamini?

.....Anasema HIV haipo. Nimemwonyesha under electron microscope anasema hivo sio HIV.....

Wewe unachukulia mambo kirahisi sana.Sasa twende mdogo mdogo halafu watu wajipimie wenyewe.

Mimi nasema hakuna HIV,wewe unasema HIV yupo.Sasa tujadili hoja hii peke yake kwanza kisha tutakwenda kwenye hizo zingine.

Ili sayansi iitwe sayansi,kwenye hili suala la HIV/AIDS inabidi kile kilichosemwa kiendane na kile kinachotokea huku mitaani,sawasawa?Kama kilichosemwa hakiendani na kile kinachotokea huku mitaani basi hiyo sio sayansi ya kweli.

Sasa prove beyond any doubt kwamba kuna HIV,tutumie kile tunachokiona mitaani,usilete link hapa,hata mimi ninazo link nyingi tu ambazo najua hutaziamini,hivyo tambua pia hata hizo za kwako mimi sitazikubali....sasa twende kwenye uhalisia kwa kile tunachokiona.Thibitisha kwamba HIV yupo.

Tuanzie hapo.
 
Solution ya huu mjadala ni mtu achomwe damu yenye VVU halafu afanyiwe monitoring kwa muda

Otherwise hakutakua na mwisho
 

Mkuu Deception unapotosha umma.

Anza kwenda mtaani wewe. Anza na wizara ya Afya, kawaambie HIV virus ni fake. Waambie serikali inapoteza hela inapochangia kununua ARV.

Baada ya hapo nenda pale Muhimbili. Omba upewe rekodi za watoto wadogo waliozaliwa na akina mama wenye maambukizi ya HIV. Halafu wajibu hao madaktari kwanini watoto wengine wanazaliwa positive na wengine negative.

Halafu nenda kwenye clinic ya CTC chukua meza isimamie, chukua loud speaker waambie HIV virus ni fake.

Wewe ungekuwa ni mtaalam ungeachana na you tube, ujitike kwenye uchunguzi halafu uibuke na abstract.

So Naive.
 
...
Wewe ungekuwa ni mtaalam ungeachana na you tube, ujitike kwenye uchunguzi halafu uibuke na abstract......

Vipi kuhusu papers/proofs za kina Prof Peter Duesberg,David Rasnick na madaktari wengine wengi waliopinga suala hili, ulizifuatilia kabla ya kuhitaji ya kwangu?Usifikiri mimi naongea kitu rahisi kama unavyofikiri.
Kama unajiamini tuanzishe uzi tufanye debate kati ya mimi na wewe,nadhani hii ndio itakuwa njia nzuri zaidi ya watu kuona kama kweli wewe unajua unachokisema au la.Waokoe watu ambao mimi nimefanikiwa kuwadanganya kwenye hiyo debate,nimekupa nafasi hiyo itumie.

Galo amekuchanganya vibaya sana,elimu uliyonayo wewe kuhusu suala hili misingi yake ni uongo kutoka kwa R.Galo.Sasa nakusubiri kwenye hiyo debate.Usiongee maneno mengi kufurahisha watu hapa wakati ukweli unaukwepa.
 
Bushman10.

AIDS ni ugonjwa unaosababishwa na upungufu wa Kinga mwilini. Hilo sina ubishi.

Huyu aliyesema hayo maneno ambayo nime bold hapo juu ndio ananiambia mimi ni ignorant.Kama kuna mtu hajaelewa nina maana gani kuhusu hayo maneno hapo juu basi nakiri kushindwa mjadala huu.


Hahahahaa mkuu Deception, nimeipenda sana hii comment yako.

-Kaveli-
 
hakuna cha debate wala nini,waliokuelewa wainue mikono,tuwachanjie damu yenye HIV.
 
Mkuu, jambo dogo lipi ?

-Kaveli-
kuema AIDS ni ugonjwa usababishwao na Upingufu wa Kinga Mwilini badala ya AIDS ni Upungufu wa Kinga Mwilini
 


Madam Sky,

Ume-raise hoja ya msingi sana. If ''HIV=AIDS'' is a HOAX, then why wazungu hao hao waendelee kupoteza pesa zao nyingi sana ku-fund 'CURE' Researches??!

Swali lako linafikirisha.

-Kaveli-
 
Mkuu kuna watu niwavivu wakutumia akili zao so watakuelewa ila itachukua muda
 
Hahahahaa mkuu Deception, nimeipenda sana hii comment yako.

-Kaveli-

Mkuu Mzingo hakuna nilichojichanganya. Ni yeye mwenyewe hajui anachokisema.

Deception anasema hakuna virusi vya HIV. ila anakubali kuna AIDS.

Anasema AIDS haisababishwi na Virusi vya HIV bali sumu ya dawa za ARV.

Haelewi maana ya AIDS, ndiyo maana nikasema ni ugonjwa wa ukosefu wa kinga. Na HIV Virus wanavamia kinga ya mwili hatimaye ugonjwa.

Sasa nimechanganya wapi?

Deception ameaminishwa na you tube anachosema. Anajua vipi kwamba hao wanaosema hakuna HIV virus hawawatakii mema watu na hasa waafrika? anaamini vipi hawa watu? Mtu anakumbia hiki kitu kipo salama , usijali we endelea tu halafu pembeni yako watu wanakufa na hicho hicho kitu unachoaminishwa kipo salama.

Deception anasema twende mtaani. Mtaani kuna watu kibao wanaishi na virusi. Kabla ya dawa walikuwa hoi. Baada ya kuanza dozi afya zimerudi. Halafu Deception anasema twende mtaani.
 
Madam Sky,

Ume-raise hoja ya msingi sana. If ''HIV=AIDS'' is a HOAX, then why wazungu hao hao waendelee kupoteza pesa zao nyingi sana ku-fund 'CURE' Researches??!

Swali lako linafikirisha.

-Kaveli-

Amini usiamini,hizo pesa hazitumiki kwenye research kwa kuwa wanajua walichokifanya,wanajua wazi kwamba HIV=AIDS hypothesis is WRONG....hivyo pesa za research ni mojawapo ya target zao kuliwa na viwanda vya madawa ukiacha zile wanazozipata kwa kuuza ARVs...wananchi wanakamuliwa kodi wakijua kwamba zinatumika katika mambo kama haya ya research lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya pesa hizo zinaliwa na wajanja wa viwanda vya madawa..asilimia ndogo iliyobaki ndio wanazuga kufanya research.

Wameshindwa kupata 'CURE' kwa zaidi ya miaka 30.Sasa kama kweli wanatafuta 'cure' kwanini wasijaribu kufanya research kwenye alternative AIDS hypothesis ambayo ni LIFESTYLE/AIDS hypothesis ambayo tena ilishauriwa na madaktari nguli na maarufu duniani.Kama kweli wanatafuta tiba kwanini wanakwepa kujaribu hii hypothesis mbadala?Kwanini wanaipinga badala ya kujaribu kama kweli lengo ni kupata tiba?

Wanakula mabilioni ya dola ya walipa kodi pamoja na mauzo ya ARVs na dawa zinazoendana nazo...sasa wewe unafikiri watakwambia kama wamepata dawa kweli?This is very big business..watu hawajui tu..

Haya tutumie logic hapa pia:
Takwimu za WHO za miaka ya hivi karibuni zinasema kwamba...ugonjwa wa malaria unaua watu takribani laki 6 kwa mwaka,TB ni 1.5 mil,'HIV/AIDS' ni 1.5 mil na cancer ni 6 mil.....sasa ukijumlisha vifo vya malaria,TB na hiyo HIV/AIDS bado havifikii vile vya cancer...sasa kwanini nguvu kubwa zaidi iko kwenye 'HIV/AIDS' halafu cancer kuna nguvu ndogo sana?

Think about that,kama mtu atataka nimletee data za WHO kuthibitisha hilo nitamletea.
 
Mkuu Deception apeleke findings zake WHO, anaweza kupewa tuzo la Nobel kwa kugundua hakuna HIV, na akaitangaza Tanzania kimataifa.πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€.

Kwakifupi miaka kama kumi iliyopita walishakata tamaa ya kupata tiba, sasa hivi wanaregreat kuwa kusimamisha funds za research kumefanya dawa imechelewa kwa miaka kumi.https://www.google.co.uk/url?sa=t&r...ztKJZ7M3EbhmQju_w&sig2=RGYZ69ITrBREcmH7Zw48vA
 

Deception huo ni mtizamo wako.

System ya marekani kutoa hela kwenda kufanya research usifikiri ni kama hapa Bongo. Ni process na lazima research iwe documented kwenye kila stage. Sio rahisi fedha kwenda sehemu tofauti kama unavyosema. Wana rules na regulations. Na funding haidhinishwi na mtu binafsi bali ni congress.

Kwa taarifa yako tu ni kwamba dawa nyingi za ARV almost 80% kwa hapa bongo zinatoka India kwa sababu ni generic na sio brands za marekani.

Kaagalie history ya mwanamziki Prince wa marekani aliyefariki hivi karibuni. Aligundulika ni HIV positive miaka ya 90'.

Jamaa alikataa kutumia dawa. Miezi sita kabla ya kufa akagundulika tayari ana ugonjwa wa AIDS. Na alikataa kunywa dawa akiamini Mungu atamponya mpaka kifo chake.

Kwa nini nasema haya. Baada ya Prince kuwa HIV positive, aliendelea kula vizuri na kutunza afya yake, maana yake ni kwamba alikula vizuri hivyo kinga yake ikawa nzuri. Nafikiri hapo ndipo unabase kwenye theory yako ya LIFESTYLE/AIDS hypothesis.

Ila miaka ilivyozidi kwenda virusi vilidhoofusha kinga ya mwili kwa sababu virusi vya HIV vinazaliana kwa wingi na hatimaye mhusika kupata ugonjwa kwa sababu kinga ya mwili inakuwa imedhoofishwa.

Deception unashindwa kuelewa, dawa za ARV kwa sasa zina kazi tatu.

1. Kuzuia virusi vizisidi kureplicate ndani ya mhusika
2. Na virusi vikishindwa kuzaliana, Viral load inakuwa chini kiasi kwamba si rahisi mhusika kuambukiza mtu mwingine virusi (Usipotumia dawa ni rahisi kuambukiza mtu.)
3. Kuzuia mtoto aliye tumboni mwa mama kupata maambukizi ya HIV
4. Kama PEP - Kuzuia maambukizi kwa aliyebakwa, au kuzuia maambukizi kwa wataalam wa afya wanapokuwa contact na damu au vimiminika kutoka mwili wa binadamu na anaona ni hatarishi, au unapokuwa umefanya ngono hatarishi.

Cancer mpaka sasa researchers hawajui ni kitu gani kinachochea huu ugonjwa. Speculations ni nyingi. Na kumbuka Cancer haiambukizi sio kama Virusi vya HIV. Ningekuwa mimi ningepeleka research kutame ugonjwa ninaojua unaambukiza zaidi, na ndicho wanachofanya.

Hebu nikuulize ndugu unafikiri tajiri mkubwa kama Steve Jobs angekubali kufa na cancer ya ini bila kuchangia research apone?
 
mkuu wala hukuwa na haja ya kujisumbua kumwelewesha mtu ambaye hawez kuelewa.
 
Mkuu kaveli njoo wewe nikudunge damu yenye HIV then hapo kweli utakuwa mwanafunzi mzuri. Acha kujificha nyuma fadhili kanjanja!! Haha


Hahahahaa mkuu, wacha maskhara yako Dr. Mkuyati. Hii inshu nzito kaka. Kujiunga 'gridi ya Taifa' ni mtihani mzito shekh. πŸ˜€

Hapo umemaanisha 'fadhili muuza maji' ? πŸ™‚

-Kaveli-
 
Kaka nakuhakikishia hapa unatwanga maji kwenye kinu. Huyu jamaa hana background yeyote ya uelewa wa mgonjwa let alone HIV. Pia hana uelewa wowote wa ku assimilate research findings kisayansi, kwa lugha nyingine anachokiongea hakielewi vizuri. Lakini pia ni Mganga wa kienyeji,, you know the drill.... Hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…