Amini usiamini,hizo pesa hazitumiki kwenye research kwa kuwa wanajua walichokifanya,wanajua wazi kwamba HIV=AIDS hypothesis is WRONG....hivyo pesa za research ni mojawapo ya target zao kuliwa na viwanda vya madawa ukiacha zile wanazozipata kwa kuuza ARVs...wananchi wanakamuliwa kodi wakijua kwamba zinatumika katika mambo kama haya ya research lakini ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya pesa hizo zinaliwa na wajanja wa viwanda vya madawa..asilimia ndogo iliyobaki ndio wanazuga kufanya research.
Wameshindwa kupata 'CURE' kwa zaidi ya miaka 30.Sasa kama kweli wanatafuta 'cure' kwanini wasijaribu kufanya research kwenye alternative AIDS hypothesis ambayo ni LIFESTYLE/AIDS hypothesis ambayo tena ilishauriwa na madaktari nguli na maarufu duniani.Kama kweli wanatafuta tiba kwanini wanakwepa kujaribu hii hypothesis mbadala?Kwanini wanaipinga badala ya kujaribu kama kweli lengo ni kupata tiba?
Wanakula mabilioni ya dola ya walipa kodi pamoja na mauzo ya ARVs na dawa zinazoendana nazo...sasa wewe unafikiri watakwambia kama wamepata dawa kweli?This is very big business..watu hawajui tu..
Haya tutumie logic hapa pia:
Takwimu za WHO za miaka ya hivi karibuni zinasema kwamba...ugonjwa wa malaria unaua watu takribani laki 6 kwa mwaka,TB ni 1.5 mil,'HIV/AIDS' ni 1.5 mil na cancer ni 6 mil.....sasa ukijumlisha vifo vya malaria,TB na hiyo HIV/AIDS bado havifikii vile vya cancer...sasa kwanini nguvu kubwa zaidi iko kwenye 'HIV/AIDS' halafu cancer kuna nguvu ndogo sana?
Think about that,kama mtu atataka nimletee data za WHO kuthibitisha hilo nitamletea.
Deception huo ni mtizamo wako.
System ya marekani kutoa hela kwenda kufanya research usifikiri ni kama hapa Bongo. Ni process na lazima research iwe documented kwenye kila stage. Sio rahisi fedha kwenda sehemu tofauti kama unavyosema. Wana rules na regulations. Na funding haidhinishwi na mtu binafsi bali ni congress.
Kwa taarifa yako tu ni kwamba dawa nyingi za ARV almost 80% kwa hapa bongo zinatoka India kwa sababu ni generic na sio brands za marekani.
Kaagalie history ya mwanamziki Prince wa marekani aliyefariki hivi karibuni. Aligundulika ni HIV positive miaka ya 90'.
Jamaa alikataa kutumia dawa. Miezi sita kabla ya kufa akagundulika tayari ana ugonjwa wa AIDS. Na alikataa kunywa dawa akiamini Mungu atamponya mpaka kifo chake.
Kwa nini nasema haya. Baada ya Prince kuwa HIV positive, aliendelea kula vizuri na kutunza afya yake, maana yake ni kwamba alikula vizuri hivyo kinga yake ikawa nzuri.
Nafikiri hapo ndipo unabase kwenye theory yako ya LIFESTYLE/AIDS hypothesis.
Ila miaka ilivyozidi kwenda virusi vilidhoofusha kinga ya mwili kwa sababu virusi vya HIV vinazaliana kwa wingi na hatimaye mhusika kupata ugonjwa kwa sababu kinga ya mwili inakuwa imedhoofishwa.
Deception unashindwa kuelewa, dawa za ARV kwa sasa zina kazi tatu.
1. Kuzuia virusi vizisidi kureplicate ndani ya mhusika
2. Na virusi vikishindwa kuzaliana, Viral load inakuwa chini kiasi kwamba si rahisi mhusika kuambukiza mtu mwingine virusi (Usipotumia dawa ni rahisi kuambukiza mtu.)
3. Kuzuia mtoto aliye tumboni mwa mama kupata maambukizi ya HIV
4. Kama PEP - Kuzuia maambukizi kwa aliyebakwa, au kuzuia maambukizi kwa wataalam wa afya wanapokuwa contact na damu au vimiminika kutoka mwili wa binadamu na anaona ni hatarishi, au unapokuwa umefanya ngono hatarishi.
Cancer mpaka sasa researchers hawajui ni kitu gani kinachochea huu ugonjwa. Speculations ni nyingi. Na kumbuka Cancer haiambukizi sio kama Virusi vya HIV. Ningekuwa mimi ningepeleka research kutame ugonjwa ninaojua unaambukiza zaidi, na ndicho wanachofanya.
Hebu nikuulize ndugu unafikiri tajiri mkubwa kama Steve Jobs angekubali kufa na cancer ya ini bila kuchangia research apone?