Wewe una matatizo,tena matatizo makubwa sana,wapi nimesema hakuna ukimwi?Hebu tafuta post hata moja niliyosema kwamba hakuna ukimwi halafu ubandike hapa ili wanaokusoma wakuelewe unachomaanisha.
Sasa kama haya mambo madogo sana unashindwa kuyaelewa,itakuwa yale makubwa ya kufikirisha?Eti deception anasema hakuna ukimwi...sasa waoneshe watu wapi nimesema hivyo.Usipoweza kuwaonesha watu wapi nimesema hivyo jihukumu mwenyewe wewe ni mtu wa aina gani.
Halafu kama ikitokea watu wote humu hawaamini ndio itakuwaje sasa kwa unavyofikiri wewe?Kwa hiyo kwa mfano watu dunia nzima wakisema hatuamini kama kuna jua,basi ndio kweli hakuna jua,au vipi?
Miaka ya 1600 Galileo alisema dunia inazunguka jua,lakini watu wote kipindi kile hawakumwamini...kwahiyo ni kweli dunia haizunguki jua kwakua wengi hawakumwamini?
Huoni kwamba kuelewa ni suala la uwezo wa mtu binafsi?Ndio maana darasani kuna wa kwanza na wa mwisho.
NB:
Hata kama wote humu watasema hawaniamini,ndio inakuaje sasa?Kama wote humu ni wajinga na wavivu wa kufikiri sasa mimi nitawasaidiaje?Ninachokiweza ni kutoa elimu kwenu,kama hamtaki kuelewa au hamwelewi sina uwezo wa kuwalazimisha kwakua kila mtu ana uhuru wake...kwani ni lazima kuwaokoa watu wote?Lazima wapo watakaopotea,sasa hilo si kosa langu.
Hapa hatuangalii IMANI,hii ni sayansi bwana...kama huelewi hilo tatizo lako binafsi....mtu unashindwa kutofautisha hata HIV na ukimwi mambo ambayo ni very basic..kwenye ukimwi unasema HIV kwenye HIV unasema ukimwi....sasa wewe unafikiri nitakusaidiaje...hicho ni kilema kikubwa sana.