Tangu mabando yapande bei, Diamond pekee kaweza kupata views milioni kwa siku, kahamia muziki unaoweza kusikika na kila mtu ila ni wachache wanauimba

Una shida aisee. Wamesema top earners in africa sio watumiaji wote. Na ni mambo yote sio wasanii tu. Changamsha ubongo acha kukurupuka
 
Diamond kuanza kuimba hizo nyimbo ni kawaida kwa sababu ndio bongo flava ya kipindi kile Ila baada ya kupata mafanikio makubwa baada ya collabo na davido, diamond ndio alianza focus na biashara zaidi kuliko taste ya muziki. Wimbo hata usiwe mzuri sana , atapiga kiki, video kali na promo na muziki ukaenda.
Hata WCB imejengwa hivyo hivyo

Hizo zingine unazosema ni mbinu za kimasoko ndio maana utaona kila kitu kimeenda na timing. All in all tuinjoi muziki mzuri
 
Duu brother Nitarejea,Mbagala,Je Utanipenda............ Mbona Mondi alianza zamani sana.

Sema aliswitch alivyoanza kuimba Number 1 hapo Mondi akabdilika kabisa, hizi za kulialia ndio uwanja wale wa nyumbani.....
Nilikuwa naongelea kwa kipindi cha sasa brother kwa sababu hata context ya mada ni kwa jinsi alivyoswitch ladha. Mleta mada alivyoileta ni kama diamond ndio kaanza na mimi nimemuonesha tu kuwa kuna nyimbo nyingi tu clean watu wameimba na zimefanikiwa kipindi ambacho diamond anaimba hizi commercials.
Kwa hiyo yeye apongezwe kwa kuswitch Ila wasiweke kama yeye ndio anabadili muelekeo wa game while watu kama kiba, konde na jay melody walikuwa wanatoa hits zenye muelekeo huo tayari📌
 

Hit song kubwa mwaka uliopita ni nakupenda ya jay melody

Sikiliza nyimbo za konde kama leave me alone

Sikiliza album nzima ya kiba na mega hit kama utu

Uliiskiza hit song ya nandy - siwezi

Sikiliza nyimbo za marioo nyingi tu ni clean kama for you na mi Amor na zote ni mega hits


Kwa hiyo hawa wasanii wote ni wadogo na wana airtime ndogo na wamefumbia macho kitu wanachokifanya tayari.
I wish tufikie level za grammy, BET, MTV au billboards ambapo msanii anapewa anachostahili bila kuangalia fan base kuliko bongo na teams zetu
 
Yote tisa Mondi ndiye anaye set trend kwenye vitu vyingi, hivi kipindi Harmo anaimba hizi za kulialia nani ulimsikia anaimba type hizo. Ila mimi nakupa miezi mitatu then subiria nyimbo zitakazo achiwa na wasanii wengine.

Kiba ni msanii ambayo si anayebadilika kwani unaweza kupredict ataimba style ipi ya mziki labda Harmo ngumu kumtabiri ila Kiba anatabirika kabisa.

Najua utarefer amapiano ila kwa bongo Mario ndiye wa kwanza kutoa nyimbo ya Amapiano na ikahits na ana nyimbo 3 za Amapiano zote hit, baada ya Mama Amina ndipo zikaanza kufumuka.
 
Kwa new generation, marioo ndio standard maana wakati anatoa nyimbo kama inatosha, hakuna aliyekuwa anaamini kama hizo slow bongoz zinaweza kuhit na mwishowe upcoming wengi wakarudi huko. Hata wimbo wa Raha, ukisikiliza mahazi ya kizamani mixer kisasa ndio unapata zingine kama za rudi darasani ya aslay hadi huyu hapa ya mbosso. Nasikitika tu marioo kaanza kupoteza hiyo nguvu yake kwa kuwa commercial zaidi

Mwingine ni Baddest, sio fan wake Ila jamaa ana influence sana kwa new generation, anachoimba ndio kinatrend

Kwa wasanii waliopita of course diamond ni standard na vijana wengi wanamuangalia, naamini hata akitaka kuipeleka singeli international anaweza maana impact ya "nasema nawe" Ilidhihirisha hilo na hicho ndicho diamond kashindwa kukifanikisha. Kuwa na identity ya muziki kama mb dog, Mr nice, saida, Cpwaa, THT artists kiujumla etc

I wish awe na hiyo legacy kimuziki maana kuwa tu influencial commercially kupitia u copy cat wa genre za nje mara nyingi rekodi haidumu kama kuacha your own sound.
 
Kukopi genre za nje kama zipi na ngapi au ile Asake kwenye nyimbo moja ya Mbosso? Brother wasanii wengi wanakopi ila Mondi anaoneka anakopi sana sababu yy ni mkubwa, ila ukitizama inakuzwa sana.

Halafu cha ajabu huyo anaye ambiwa anakopi genre za watu ndiye anayefanya vizuri kulio hao wengine. Mondi ktk nchi za Sahara zaidi ya 90% kishapiga show ila ulaya ndipo anastrugle.
 
Ni wasanii wangapi A-list wa Africa waliopo hapo.
 
Kwa hiyo hizo hela YouTube wanazopata hizi online video wanawatumia wakuna nani?

Wakina Millard Ayo,Simulizi na Sauti,Diamond nk hela wanapewaje na YouTube wakati hawa julikani.
Ku-argue na hater usitegemee kufikia muafaka, kuna content creators wengi wanasafiri kila mara around the world na YouTube acc zao ni ndogo sana, wanajenga mijengo ya maana lakini hata 25% ya views anazopata Diamond hawafikii.
 
Konde anajiimbia mwenyewe
 
Exactly, Nasib anaplay part kubwa sana kwenye utayarishaji wa video zake- nilipata dodoso hii kwa mtu wangu wa karibu(Director fulani wa bongo)

Ni kawaida hii kama una kipaji cha ubunifu lazima utataka uelekeo wa kazi zako vile unavyopanga.
 

Mkuu umepost yote hayo ku prove nini?

Kwamba wasanii wa usafini hawalipwi according na views?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…