Tangu mwaka umeanza nimeishi kama anavyotaka Prof. Janabi, leo asubuhi nimeanguka kwa njaa

Utofauti wa masikini na tajiri ni huu
Masikini akiugua na kupelekwa hospital ataambiwa aongeze bidii katika kula ila
Tajiri akiugua na kupelekwa hospital ataambiwa apunguze kula
Kwako mwandishi
 
Habari za leo wakuu

Mimi ni kijana wa makamo, wakati fulani nilikuwa nikimsikiliza sana Prof. Mohamed Janabi kuhusu ulaji na mtindo Bora wa maisha, awali nilikuwa nakula kutwa mara tatu sana sana vyakula vya mafuta na sukari nyingi ikiwemo ngano na ugali lakini baada ya kusikiliza ushauri wa huyu daktari bingwa nikabadili mtindo wangu wa ulaji, ikawa nikiamka asubuhi nakunywa maji tu then naenda kwenye shughuli zangu, mchana nakula ugali kidogo na mboga za majani na mtindi, jioni nakula matunda na mtindi tena, ratiba hii hubadilika lakini sitoki nje ya vyakula vya aina hiyo.

Wakuu leo asubuhi nimeamka vizuri kwenda kwenye shughuli zangu, kufika mahali fulani nikaanza kujihisi kizunguzungu nikakaa chini huku jasho linanitoka, njaa nayo ikawa inanikomoa kwelikweli utumbo wote unakata. Nikajikongoja mpaka hospitali fulani kupimwa naambiwa sukari imeshuka kutokana na ulaji duni nikashauriwa niache ubahili nile vya kutosha. Kwa sasa sijambo nipo nyumbani navuta nguvu wife kaniandalia supu ya kuku wa kienyeji, juice ya matunda kaniwekea sukari nyingi pamoja kachori, baadae ataniandalia chapati na mishikaki ya nundu.

Prof Janabi nakuita mara tatu
Sijapenda ulitaka kunitoa roho kwa ushauri wako wa hovyo.
Nimecheka Sana bila hata kusoma uzi
 
Mimi mkuu nilisema, sitarudia kabisa! Nilishindwa mpaka kuendesha baiskeli ikabidi nitafute mti nipumzike maana miguu ilikuwa haiwezi tena kunyanyuka na nimebakiza kama kilomita 30 hivi kufika home. Ikabidi nitafute mtu wa kukodi kuniendesha mpaka kwenye centre ili nipate msosi!
 
Mm bhana asubuhi naamkia shambani sasa ple nitapata dafu,pensheni,parachichi au papai apo nikijiona nipo vzr nasubiri mchana kma leo nimebugia madafu ata mchana sijala hpa ndo naenda kula
 
Habari za leo wakuu

Mimi ni kijana wa makamo, wakati fulani nilikuwa nikimsikiliza sana Prof. Mohamed Janabi kuhusu ulaji na mtindo Bora wa maisha, awali nilikuwa nakula kutwa mara tatu sana sana vyakula vya mafuta na sukari nyingi ikiwemo ngano na ugali lakini baada ya kusikiliza ushauri wa huyu daktari bingwa nikabadili mtindo wangu wa ulaji, ikawa nikiamka asubuhi nakunywa maji tu then naenda kwenye shughuli zangu, mchana nakula ugali kidogo na mboga za majani na mtindi, jioni nakula matunda na mtindi tena, ratiba hii hubadilika lakini sitoki nje ya vyakula vya aina hiyo.

Wakuu leo asubuhi nimeamka vizuri kwenda kwenye shughuli zangu, kufika mahali fulani nikaanza kujihisi kizunguzungu nikakaa chini huku jasho linanitoka, njaa nayo ikawa inanikomoa kwelikweli utumbo wote unakata. Nikajikongoja mpaka hospitali fulani kupimwa naambiwa sukari imeshuka kutokana na ulaji duni nikashauriwa niache ubahili nile vya kutosha. Kwa sasa sijambo nipo nyumbani navuta nguvu wife kaniandalia supu ya kuku wa kienyeji, juice ya matunda kaniwekea sukari nyingi pamoja kachori, baadae ataniandalia chapati na mishikaki ya nundu.

Prof Janabi nakuita mara tatu
Sijapenda ulitaka kunitoa roho kwa ushauri wako wa hovyo.
Ushauri kuhusu kupanga kula unatakiwa kutolewa baada ya mtu kupimwa afya yake. Na hautolewi kiujumla kwa watu wote, kwa sababu watu hawako sawa.

Dr. Janabi anakosea sana kutoa ushauri wa jumla katika jambo ambalo watu wanatakiwa kupimwa na kushauriwa kwa mujibu wa hali zao.
 
Kwa sasa sijambo nipo nyumbani navuta nguvu wife kaniandalia supu ya kuku wa kienyeji, juice ya matunda kaniwekea sukari nyingi pamoja kachori, baadae ataniandalia chapati na mishikaki ya nundu.
Mkuu unavyosimulia kama nakuona vile! Hii hali ndiyo hiyo hiyo na mimi ilinikuta! Nilikuwa sijala usiku eti kulipokucha nikachukua baiskeli kwenda kufukuzia manzi kijiji cha mbali na mjini, kw wenyeji wa Shinyanga watakuwa wanaijua sehemu inaitwa Idukilo. Duh, njaa jamani isikieni tu, ndiyo maana ka Prof. Janabi hakana Siha njema utafikri kagonjwa ka ukimwi!
 
Sio yeye tu Kuna dr.mkumbo ndio nilifahamu hii kitu kwake NI Tina ya wenye uzito mkubwa na magonjwa ya homoni... Sukari na Mambo Kama hayo ulaji wa kupunguza sakari au kuuacha kabisa....umenisaidia mwaka 2016 kutoka kilo 86 mpaka kilo 75....huku unakula vyema nyama na mbogamboga...na Sasa hivi nimeanza Tena baada ya kujiachia na kuhisi suruali Zina nibana na kusikia maumivu hovyo...Kama una weza achana na mdhaha wa mtoa mada
 
Habari za leo wakuu

Mimi ni kijana wa makamo, wakati fulani nilikuwa nikimsikiliza sana Prof. Mohamed Janabi kuhusu ulaji na mtindo Bora wa maisha, awali nilikuwa nakula kutwa mara tatu sana sana vyakula vya mafuta na sukari nyingi ikiwemo ngano na ugali lakini baada ya kusikiliza ushauri wa huyu daktari bingwa nikabadili mtindo wangu wa ulaji, ikawa nikiamka asubuhi nakunywa maji tu then naenda kwenye shughuli zangu, mchana nakula ugali kidogo na mboga za majani na mtindi, jioni nakula matunda na mtindi tena, ratiba hii hubadilika lakini sitoki nje ya vyakula vya aina hiyo.

Wakuu leo asubuhi nimeamka vizuri kwenda kwenye shughuli zangu, kufika mahali fulani nikaanza kujihisi kizunguzungu nikakaa chini huku jasho linanitoka, njaa nayo ikawa inanikomoa kwelikweli utumbo wote unakata. Nikajikongoja mpaka hospitali fulani kupimwa naambiwa sukari imeshuka kutokana na ulaji duni nikashauriwa niache ubahili nile vya kutosha. Kwa sasa sijambo nipo nyumbani navuta nguvu wife kaniandalia supu ya kuku wa kienyeji, juice ya matunda kaniwekea sukari nyingi pamoja kachori, baadae ataniandalia chapati na mishikaki ya nundu.

Prof Janabi nakuita mara tatu
Sijapenda ulitaka kunitoa roho kwa ushauri wako wa hovyo.
Maamae utakuja kufa na tai shingoni 🤣🤣🤣
 
Back
Top Bottom