Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

asante mkuu nmefikiria kuondoka mimi sababu tunaishi nyumba ya kupanga kuna kiwanja nilinunua kwa ajili ya ujenzi ila nmeishia kumwaga tofali tu kwanza
bora wewe ata umeweza mwaga tofali sie wengine tunaishia kusafisha kiwanja tuu. hela zikifika million threesome inaondoka nazo 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Kuondoka sio solution mkuu. Cha msingi kaa nae umwambie kama mume kila mtu abaki na majukumu yake. Wewe kama mume utaendelea kuprovide matumizi na yeye kama mke aendelee na majukumu yake haijalishi unashinda nyumbani au vipi as long as matumizi unatoa.

Na inabidi usimame kama mume kipindi hiki maana ukitetereka kidogo tuu utaonja joto ya jiwe mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nijweli, Vijana tunatamiwa kabla ya kuoa inabidi mpenzi wako akuzoee ukiwa hauna pesa na akukute hauna kipato kizuri ili umjue tabia mapema

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Mimi issue yako ni kama yangu, yalinishinda nikaamua kumchana live arudi kwao. Aniache kwanza nijitafakari. Sawa sina kazi kwa sasa lakini nahudumia familia kwa kila kitu.

Dharau ni kitu sipendi kutoka kwa mwanamke. Bora nikae peke yangu kuliko kukaa na mtu anae kudharau ndani.

Sasa hvi yupo kwao pamoja na watoto na hvi ni likizo. huku mimi nipo naishi kibachela naendelea kujipanga upya namna ya kupambana na maisha. I believe nitatoboa tu.
 
Point noted, wadau Same na Dar kuna traako kubwa kubwaz.

Ila mwanamke ni mpokeaji tu sasa akianza kuwa mtoaji, jua atatoa hadi na matatizo pia.
 
Unawajua mabinti wa kichagga wewe?
 
Ngoja naye yakimpata umbadilikie atie akilini
 

Utapata shida sana:

  • Mwanamke atazaa kwa uchungu.
  • Mwanaume atakula kwa jasho.

Ingawa mke wako kazidi, lakini nataka ujue hakuna mwanamke atakaye mvumilia mwanaume anayeshinda home na kufanya kazi za House girl.
 
Kila siku tunasema humu, ajira haimfanyi mwanamke kua mke bora. Hapo nae tayar keshajiona ni mwanaume kisa analeta hela ya kula ndani.

Hapo anaitafuta 50/50 kwamba wee nae zamu yako unapaswa umpokee majukumu yake ya ndani.

Aisee hii ndo wanasema kua uyaone.
 
Ktk maisha hamna kipind kigumu mwanamue anapitia Kama kukosa Ela ya kulisha familia.

Na kibaya zaidi MKE ulienae ndani nae akubadilikie,

Aisee Utahs Moyo wako unapitishwa ktk tanuri kali la Moto[emoji26]
 
Kuna vitabia vya kivivu kaviona kwako vinamboa.hata kama huna kazi hamka saa 12 kapambane sio unalala mpaka saa tano ukiamka unashindia kwenye TV.All in all wanawake wengi wanadharau sana unapokosa kipato.
Hata Kama ni uvivu,
Sio mom kufikia kumnyima tendo na kumfulisha nguo. Hiyo Ni tabia ya kifeminism[emoji2955]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…