Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Kuna kitu kipo unaweza usiamini ila kuna hii ya kulinganisha ,Mkeo anapofanya kazi Kuna wanaume kibao hata wanaomzidi mshahara na hao ndo anakuwa anaokutana nao katika daily routine yake ni hatar sana kwa afya ndoa yako.

Sasa wewe hauna kazi na huko kazini anapigwa miruzi na hao jamaa anahitaji kuwa na moyo wa chuma sana kuchomoa.

Kaa mkao wa kula 😂😂
 
mashatiboyee Kaka fanya subra kidogo. Ni asili ya mwanamke kupenda kuwa na Mwanaume anayeweza kuleta chakula na kumlinda. Ni asili ya Mwanaume kutaka kuheshimiwa.

Kama hajakusaliti, haya mambo yanazungumzika. Kwa faida ya Familia (mtoto) kaa naye muongee. Hili swala litapita. Mtangulize uvumilivu mbele. Uzuri kipato sio kibaya na uwezo wa kuhimili hili mnao. Ongea naye. Fanya subra. Fanya subra. Fanya Subra.

Katika mazungumzo muweke maslahi ya mtoto mbele.
 
asante mkuu kwa ushauri, huu ni ukweli mchungu natakiwa kuumeza mimi bila kushauriwa na mtu kesho natoka hapa nyumbani nitakuwa natoa huduma za mtoto tuu ndoa imeshanishinda hii
Usikate tamaaa vitimbi vya wanawake ni vingi hakuna pasipo vuja tengeneza furaha yako chukulia vitu kimaskhara na fanya maamuzi sahihi kuachana nae sio suluhisho wanawake wote ni walewale.

Ukitaka alie Bora msubirie malaika au tengeneza wako.
 
Mkuu me niliwai yumba kimaisha mwanamke akawa analeta dharau nilikomaa kupambana mpaka akaondoka mwenyewe.

Mwaka wa nne huu napambana na sasa nimesimama tena kimaisha, mama yake mzazi na kaka zake wameanza kunipigia simu mimi kimya wala sijali zaidi ya kumuhudumia mtoto wangu tu niliyezaa nae japo sikuwa na ndoa nae na alikuwa mchaga wa mwika me mtu wa Arusha na hapa naona mwanamke mwingine yy apambane na hali yake.

Nakushauri ondoka hapo nyumbani nenda mbali kapambane, anzisha hata biashara ndogo pambana ukisimama tena atakutafuta mbona.
 
Tatizo ulilikaribisha mwenyewe ulipo oa mchaga wa Vunjo. Mimi huwa nawauliza Sana vijana.
Kwenu hakuna warembo mpaka mkaoe kwa watu?
Ukiwa msambaa, oa msambaa mwenzio hata mbondei, mdigo na mzigua usiguse.
Ukiwa mpare wa usangi, kaoe usangi achana na dada zetu wa Same.
Usioe kwa sababu ya tako. Oa asiye na yako lkn mwenye busara.
Wenye mijitako wako tele Dar. Unajipigia mwenye tako mchana jioni Benet na wife flat screen.
Oyaaa we jamaa ni fala [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji119][emoji119]
 
Nimejikuta nakuonea huruma mkuu kwa sababu kwa haraka unaonekana mtu mwema tu ila ni michongo tu haijakaa sawa.

Siamini kama ushauri wangu utakua mzuri sana ila unatakiwa uondoke hapo nyumbani and never go back. Kajichimbie mikoani huko na upambane na mishe yoyote halali bila kujali chochote

Huyo mkeo tayari ana watu wengine na utakuja kumuua bure ukafungwe jela.

Ondoka milele hapo
 
Habari za jioni wanajukwaa wa MMU, ikiwa mmetoka katika mihangaiko akili na mwili vimechoka nawaletea jambo jingine hili tupate kulijadili.

Mimi na mke wangu ni waajiliwa yeye ni mtumishi wa umma na mimi ni mtumishi wa sekta binafsi, ndoa yetu ina miaka mitatu sasa na tuna mtoto mmoja (asante sana MUNGU kwa hili).

Shida iliyonileta kwenu ni kuwa hapa karibuni nimepata matatizo ya kikazi sasa imenibidi niwe nashinda nyumbani kwa sababu mimi siyo mtu wa kukaa nje sana nahisi ndipo matatizo yalipoanzia. Tangu nipatwe na hii hali mke wangu amebadilika tabia sijui kama ni makusudi au lah.

Niwe muwazi kuwa mke wangu amenizidi mshahara lakini pamoja na hayo sijawahi kuona tabia hizi kwake hadi hapo nilipopatwa na hizo shida kazini.

Tabia zipo nyingi ila naleta tatu zilizonishitua;

~ Kwanza amekuwa hataki kushiriki nami tendo.

~ Pili sababu huwa nashinda na mtoto huwa napika kwa ajili yangu na mtoto ambapo ye akirudi anapika kwa ajili ya wote kwani anasema sijui kupika. Sasa hapo juzi kati alinambia itabidi nijifunze kupika kama nataka kuendelea kuwa naye.

~ Tatu ni kuwa tuna machine ya kufulia sasa imeharibika, nikamuomba kuwa nikipata hela tutafanya matengenezo akanijibu kama ni hivyo basi niwee namfulia nguo zikiwemo chupi zake daah.

Mimi nimefikiria uamuzi wa kuachana naye licha ya kuwa na mtoto naye, kwani sina mpango wa kumpiga na hiyo juzi ilibaki kidogo nipige arudi kwao Vunjo Mashariki na ulemavu wa uso alivyosema niwe namfulia.

Nauliza tu wanawake wa humu haya anayofanya mwenzenu ni halali kweli?

Polee sana brother, hili nenda nalo kwa busara huyo ni mke mkuu! Usikae om kusimama kazi haimaanishi hakuna kazi zingine!!!

Kama unaakiba kidogo fungua ata biashara jichanganye tafuta pesa, wewe ni baba kukaa apo om sio sawa, haya umuondoshe apo om mtoto atalelewa na nani?

Apo nikutafuta pesa tu mzee inaonekana hukuwa na muda wakukaa na familia nakumjua mwenzio yukoje....... biblia imetutaka tuishi nao kwaakili unajua kwann tuliambiwa tutumie akili kwa wanawake?

Brother toka tafuta mishe yoyote kifuatacho ni kibaya zaidi mkuu, utakuja kukuta siku ana mchepuko kabisa na atakuonyesha wazi wazi, kufukuza sio tatizo” naamini ukitoka atakuelewa au kama hukuwa na akina muazime uzungushe mtaa then utarudisha,

Ndoa na iheshimiwe na alicho kiunganisha mungu?!!! Tunaishi hapo kwenye maandiko, Dont give up brother
 
Jijengee kuanza kukabikiana na hali ya kuishi mwenyewe. Muda wowote anaweza akakuacha bila wewe kujijua.

Mwanamke akishaona umeyumba kiuchumi anakudharau na mwishowe anakuacha kabisa kama wewe utashindwa kumuacha.
 
nilimuuliza kesho yake tukiwa tumetulia na mimi nmpoa na hasira kuhusu hili swala akajiona yuko sawa still, leo nmeshinda nalo linanitafuna sana moyoni nmeamua kuja kulitema huku

Njia ni moja tu mkuu toka katafute pesa, sasa kama ajira ndo imesimama wewe utakaa apo om mpaka lini?

Maswala mengine jiulize na wewe kuwa nitakaa hapa mpaka lini? Kukaa na mwanamke kila saaa hautoki lazima ugombane, na wakati mwengine huwa sisi wanaume tunaisi tunakosewa kwasababu hatupati ile heshima tunayo stahili,

Hii yote ni kuwa jobless huwa tuna jistukia ivi kitu kidogo tunaona kikubwa, binafsi sikushauri umuwache au kupiga, chukua maneno yake kama changamoto yakujenge, yakupe ujasiri, ukajichanganye urudi na senti kidogo om, wewe unasema huwezi kujichanganya sasa itakuwaje?

Na kama ndo utakuwa apo om kila siku yatakuja makubwa hukuwai kuyaona, nashauri hivi mimi nimepitia unachopitia ilikuwa kama fursa kwangu nilijifunza mengi mno kupitia kile kipindi brother!!

Jifunze namna yakukabiliana na changamoto na sio kil jambo alianyalo ni baya, wakati mwengine wanaongea ivyo ili kutuchangamsha tutoke, tuchukue nafasi yetu kama baba, usimchukie muache akujenge brother!!! Hayo maneno yake ndo yatakujenga ila akicheka cheka utazoea vbaya! Siku moja utakuja kunshukuru uyo mkeo ndo anakupa energy ivyo yakutoka ukapambane mkuu
 
Mkuu me niliwai yumba kimaisha mwanamke akawa analeta dharau nilikomaa kupambana mpaka akaondoka mwenyewe mwaka wa nne huu napambana na sasa nimesimama tena kimaisha mama yake mzazi na kaka zake wameanza kunipigia simu mimi kimya wala sijali zaidi ya kumuhudumia mtoto wangu tu niliyezaa nae japo sikuwa na ndoa nae na alikuwa mchaga wa mwika me mtu wa Arusha na apa naona mwanamke mwingine yy apambane na hali yake.Nakushauri ondoka apo nyumbani nenda mbali kapambane anzisha ata biashara ndogo pambana ukisimama tena atakutafuta mbona

Umeshauri vizuri mkuu ila apo kwenye kuondoka om!! Anaondoka kwa sababu gani? Anamkimbia mkewe[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] na je mtoto wake nae anamkimbia? Apambane akiwa hapo hapo hakuna kukimbia majukumu yake sisi ni wanaume tangulini ukakimbia nyumba yako? Mzee akomae hapo hapo atafute hela usimlemaze huyu jamaa
 
Back
Top Bottom