Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Tangu nipatwe na Matatizo kazini, mke wangu amebadilika tabia

Kuna mwanamke alisema " ni rahisi mwanamke kupata mume bora WA kumuoa ingawa wanaume wako wachache kuliko Mwanaume kupata mke bora WA kuoa ingawa wanawake wako wengi".

Anyway MSIOE maana katika maisha lazima Kuna siku utayumba kidogo kimaisha na hapo ndio rangi zote Utaziona. Coz viumbe pekee wanaopendwa unconditionally ni MWANAMKE, MTOTO NA PAKA TU.

Siku utakayopoteza hiyo kazi inayokuingizia kipato utaletewa wanaume mpk mlangoni kwako. Usidanganywe na vile VIAPO vya pale kanisani.

Yale ni maneno tu ya kuwapa matumaini ila Hakuna mwanamke atakayekuvumilia wakati WA SHIDA. Wangefuta tu kile kipengele cha shida, waache cha raha tu.
 
Sikiliza utapigwa mimba za kutosha then unaachwa kama kawa ukiwa mpuuzi
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Bahati mbaya hujui unamuambia mtu wa aina gani upupu huu, nishavuka age ya kudate na watu hovyo hovyo.
Then punguza makasiriko Tafuta pesa timiza majukumu yako kama mwanaume.
Cha mwanamke hakitegemewi.
 
nme

nilifikiria hili ila mimi haiba yangu ni ngumu sana kujichanganya na watu na watu niaoweza kujichanganya nao wengi wanakuwa kazi zao mchana

Wewe una haiba gani mkuu? Toka jichanganye tafuta uzoefu mwingine kama una leseni kakae hata kwenye matipa utapata hata deiwaka, usikalie haiba ukweli wanawake wote ukishakua haoni upambanaji hawezi kukuheshimu ndio maana utamlisha miaka 30 , ukiyumba siku 7 tu inakua matangazo ukoo wote, tafuta angle unayojua utafit muda huu unafanya upambanaji mwingine.
 
Nawashangaaga sana wanaume wa hivyo.
Uoga wa majukumu unafanya wanaume wasiwe na sauti ya kiume sikuhizi wamebaki kama makondoo.
Binafsi nasema kabisa asije mtu kunioa akategemea nimsaidie maisha, aje afanye majukumu yake kama mume nitamzalia na watoto nitalea.
Pesa zangu ni zangu.
Ova.
Sikiliza utapigwa mimba za kutosha then unaachwa kama kawa ukiwa
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Bahati mbaya hujui unamuambia mtu wa aina gani upupu huu, nishavuka age ya kudate na watu hovyo hovyo.
Then punguza makasiriko Tafuta pesa timiza majukumu yako kama mwanaume.
Cha mwanamke hakitegemewi.
Kama ushavuka iyo age Basi acha kukata vitinguu maji .Uzuri 🤣 Medulla zenu azifanani Thanks God
 
Habari za jioni wanajukwaa wa MMU, ikiwa mmetoka katika mihangaiko akili na mwili vimechoka nawaletea jambo jingine hili tupate kulijadili.

Mimi na mke wangu ni waajiliwa yeye ni mtumishi wa umma na mimi ni mtumishi wa sekta binafsi, ndoa yetu ina miaka mitatu sasa na tuna mtoto mmoja (asante sana MUNGU kwa hili).

Shida iliyonileta kwenu ni kuwa hapa karibuni nimepata matatizo ya kikazi sasa imenibidi niwe nashinda nyumbani kwa sababu mimi siyo mtu wa kukaa nje sana nahisi ndipo matatizo yalipoanzia. Tangu nipatwe na hii hali mke wangu amebadilika tabia sijui kama ni makusudi au lah.

Niwe muwazi kuwa mke wangu amenizidi mshahara lakini pamoja na hayo sijawahi kuona tabia hizi kwake hadi hapo nilipopatwa na hizo shida kazini.

Tabia zipo nyingi ila naleta tatu zilizonishitua;

~ Kwanza amekuwa hataki kushiriki nami tendo.

~ Pili sababu huwa nashinda na mtoto huwa napika kwa ajili yangu na mtoto ambapo ye akirudi anapika kwa ajili ya wote kwani anasema sijui kupika. Sasa hapo juzi kati alinambia itabidi nijifunze kupika kama nataka kuendelea kuwa naye.

~ Tatu ni kuwa tuna machine ya kufulia sasa imeharibika, nikamuomba kuwa nikipata hela tutafanya matengenezo akanijibu kama ni hivyo basi niwee namfulia nguo zikiwemo chupi zake daah.

Mimi nimefikiria uamuzi wa kuachana naye licha ya kuwa na mtoto naye, kwani sina mpango wa kumpiga na hiyo juzi ilibaki kidogo nipige arudi kwao Vunjo Mashariki na ulemavu wa uso alivyosema niwe namfulia.

Nauliza tu wanawake wa humu haya anayofanya mwenzenu ni halali kweli?
Mkuu uamuzi ulifanya nahisi ni sahihi.
Mabinti wa kichaga 97% ukiishiwa huna lako.

Kuna binti ni mtu wa karibu alimuacha mzazi mwenzie kimasihara kwa kuachishwa kazi bank na akamwambia wazi nenda ukatafute ukipata uje. Ndio wakaachana kimasihara na eti ananisimulia bila woga, nilimwambia wazi kuwa hafai.
 
Mtoa mada tuliza kichwa. Unachopaswa kujua ni kwamba mwanaume ndio kichwa cha familia. Tayari kichwa umeyumba lazima vingine vitakosa mwelekeo.

Kuna ushauri mzuri wametoa huko juu kuwa ondoka hapo nenda mbali katafute shughuli ya kujikimu na ukikaa sawa ndio unaweza kufanya maamuzi sahihi

Kwa sasa ondoka tu hapo wala usijiangaishe na mtoto ondoka kata mawasiliano.

Wazee wa zamani walikuwa wanasepa hata miaka mitano ndio wanarudi mambo yakitengemaa. Usimwache wala nini huyo mke sepa kimya kimya badirisha namba asikupate kipindi haupo
 
Nawashangaaga sana wanaume wa hivyo.
Uoga wa majukumu unafanya wanaume wasiwe na sauti ya kiume sikuhizi wamebaki kama makondoo.
Binafsi nasema kabisa asije mtu kunioa akategemea nimsaidie maisha, aje afanye majukumu yake kama mume nitamzalia na watoto nitalea.
Pesa zangu ni zangu.
Ova.
Hapa ndo sielewi kabisa. Kwahiyo siku akikosa imekula kwake, akipata ndo mume. My dear tafuta wakuendana na wewe na uwe muwazi kabisa mwambie ukweli ajipange.
 
Kwanza kabisa ningependa kukufahamisha kuwa umeoa changudoa kwa maana changudoa pekee ndio huthamini watu kutokana na pesa kwa kuwa kwake kila kinachomhusu yeye ni biashara..........

VIjana wengi Siku hizi wanaoa makahaba wakidhania kuwa wamepata wake......na hao makahaba ndio wanaoitukanisha taasisi takatifu ya ndoa........

Misuko suko kwenye maisha ni vitu vya kawaida na mkeo alitakiwa kukutia moyo na kukufariji na sio kukubehi na kukudharau......mkeo alipaswa kukusitiri kwani wewe ndio mwandani wake.........kitendo alichokifanya mkeo ni kitendo cha kikatiri na sio Cha kibinadamu.......

Wahenga wanasema Mungu hamfichi mnafiki.....baada ya miaka mingi ya unafiki akijifanya anakupenda wewe kumbe anapenda kilichopo mfukoni mwako......Sasa huu mtihani mdogo tu umeshamuumbua na kuonesha rangi zake za asili.........

Kwa kifupi wewe hapo huna mke bali unaishi na shetani mwenye muonekano wa kike.........

Mungu amekusaidia kukuoneshea ushetani wa uliyekuwa unadhani ni mkeo Sasa uamuzi ni wako kuishi na huyo shetani uangamie au uachane nae ubakie salama..........

Kwa hali uliyokuwa na kero anazokupa mkeo ambaye ndiye angetakiwa kukufariji mimi nakushauri uachane naye ili upate utulivu wa mwili na akili
 
Kwan unapata shida gani kumfulia ama kujifunza kupika kwaajili ya umpendae? acha kusikiliza story za mtaani, ishi maisha halisia.

Kingine, hata km huna kazi, toka kajichanganye na wanaume wenzio huko nje, ukirudi njoo hata na mkate ama Embe hata km ni moja, acha ujinga mkuu
 
Hapa ndo sielewi kabisa... Kwahiyo siku akikosa imekula kwake,akipata ndo mume.... My dear tafuta wakuendana na wewe na uwe muwazi kabisa mwambie ukweli ajipange.
Mi nishakuwaga muwazi, nimemwambia kabisa mtu wangu mimi niko hivyo akiona hawezi Aende atafute mtu mwingine aoe sina cha kupoteza mimi.
 
Kwan unapata shida gani kumfulia ama kujifunza kupika kwaajili ya umpendae? acha kusikiliza story za mtaani, ishi maisha halisia.

Kingine, hata km huna kazi, toka kajichanganye na wanaume wenzio huko nje, ukirudi njoo hata na mkate ama Embe hata km ni moja, acha ujinga mkuu
Mume anatoa mahitaji yote ya familia kasoro matumizi binafsi ya mke, sasa hapo kosa la mume nini? Mwenyewe kaeleza kuwa hatoki lakini huwa anafanya kazi kupitia pc na analipwa, sasa kuzurura ndo ataonekana mume halisi?

Kufua sio shida lkn reaction ya mke kwa mumewe sio nzuri.
 
Mungu atuepushe mtu wa aina yako kwenye familia yetu, kwenye ukoo wetu hata kwenye kizazi changu.... Mtu asie kuwa na msaada kwa mumewe hapana kwakweli.
Mi nishakuwaga muwazi, nimemwambia kabisa mtu wangu mimi niko hivyo akiona hawezi Aende atafute mtu mwingine aoe sina cha kupoteza mimi.
 
Habari,
Hapa ndo panahitaji ujasiri. Mke ni wako na wewe ndo mmewe, na maisha ni yenu na familia yako.
Pata muda na mwenzako:

1: Orodhesha mabaya na mazuri ya mkeo kwako na familia yako/watoto.

2: Mke wako aje na mabaya na mazuri yako kwake na kwa familia.

3: Kaeni wawili bila mihemko na kujadili pande zote kwa kusikilizana.

4: Amueni kulinganana kilichowafanya kuwa pamoja tangu mwanzo, je mabaya yenu kati yenu yamezidi mazuri?

5: Je kwenye mabaya na mazuri ni yapi yanaweza kubadilishwa au kuendelezwa na je inawezekana?

6: Kwa yasiyoweza kubadilishwa je yanatosha kuganya maamuzi mengine zaidi ya yale yaliyowaweka pamoja?
usimsikilize uyu mwanamke akibadilika imetoka io
 
usimsikilize uyu mwanamke akibadilika imetoka io
Atampa hope za uongo mwisho atakufa kwa presha. Ajichange asepe. Mwanamke akishaanza hizo pigo jua Kuna mwana anakula mzigo. Asepe akaanze upya Mungu hatamtupa kamwe
 
Atampa hope za uongo mwisho atakufa kwa presha. Ajichange asepe. Mwanamke akishaanza hizo pigo jua Kuna mwana anakula mzigo. Asepe akaanze upya Mungu hatamtupa kamwe
hii ndio sababu naipenda jamii forums mm kuna jamaa alipata matatizo mke alianza visa aisee yaan mwanamke akichange ni balaa mm si niliingilia ugomv ili niweke mambo sawa alimanusura nimwagiwe mafuta ya moto aisee na familia naijua very close since then nilijifunza kitu mwanamke akitaka kukuacha akwambii yeye anakufanyia visa ww ndio ujiongeze
 
Mkuu kulinda heshima yako fanya haya
1. Kuwa jasiri usioneshe kumjali hata kidogo huyo mkeo

2. Anzisha mahusiano na mwanamke mwingine

3. Kama nyumba ni yako mwambie akapange humuhitaji tena

4. Weka mambo yako sawa ofisini au tafuta kazi au shughuli ya kufanya

Yakifanyika hayo atarud tena atakuomba na msamaha na atakupa haki zako zote kama mwanaume.
 
Mie nawashauri oa mtu ambaye babu wa babu yake anajulikana kwenu. Yaani huyo mchumba ama mke wako si ana babu take, Sasa huyo babu yake naye anaye babu awe anajulikana aliishije ama Tabia zake.

Oa mtu wa karibu. Hujiulizi mie wa Tarime nikitaka ubunge siwezi enda mtwara kuomba ubunge Bali naenda kwetu huko ama nakojulikana. So unaleta mtu kumpanda kwenu aote unaparamia kisa akasoma, anacho kipato
 
Back
Top Bottom