Tangu niwe na nyumba ndogo (mchepuko), ndoa yangu ina amani sasa

Miaka 15 ijayo binti yako nae atafanyiwa hivi Asante maana apandacho mtu ndicho atakachovuna
 
Hii code natembea nayo mkuu kuanzia 2025 september.
Mkuu usiingie mtegoni. Ukiona umeanzisha mahusiano ya kudumu ya kingono nje ya ndoa na rohoni huna Majuto basi imetoka hiyo ikirudi pancha.
 
Mchepuko si suluhisho la matatizo ya ndoa au uhusiano, bali ni chanzo kipya cha matatizo makubwa.Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia:

1. Kisaikolojia: Mchepuko huleta msongo wa mawazo, hofu ya kugundulika, hatia na wakati mwingine hupelekea magonjwa ya akili kutokana na migogoro isiyoisha (japo mwanzo,mwanzo utajihisi upo peponi wakati upo nae)

2. Kimaadili: Unapomchepukia mwenzi wako, unavunja maadili, uaminifu, na heshima ya familia. Ni rahisi kupoteza heshima yako mbele ya jamii na watoto wako.

3. Kiafya: Mchepuko huongeza uwezekano wa maambukizi ya magonjwa ya zinaa, hasa kama hakuna uaminifu wa kweli kati yenu.

4. Kiuchumi: Mchepuko ni gharama. Unahitaji pesa za matumizi, zawadi, outing, na mara nyingi pesa hiyo inatoka kwenye bajeti ya familia au malengo yako ya maendeleo. Mtu anaweza kupoteza kazi, ndoa au biashara kwa sababu ya mchepuko.( Kumbuka yeye anapenda Pesa zako na sio wewe)

5. Kihisia: Mchepuko huathiri moyo wa mtu. Unaishi kwa siri, kwa hofu, na kwa huzuni kwa sababu ya maisha ya uongo,
Ukweli ni kwamba hakuna faida ya kweli kwenye mchepuko. Mwisho wake ni majuto.
Kama una matatizo na mwenzi wako, suluhisho ni mazungumzo, ushauri nasaha au hatua za heshima si kusaliti.

Tafakari: ila ukikaidi ipo siku utakumbuka huu ujumbe!
 
Unatatizo la kisaikolojia.. Nenda katibiwe haraka sana.. Maana akiwa busy tena na jinsi unajipa moyo utarudi kule kule..
 
Ubarikiwe
 
Alooh hako katoto ka buku mbili sio kale kakwangu mkuu kembaba kafupi hivi keupe kamchepuko kangu ka kitambo hako siku hizi sikaelewi kananichuna balaa
 
Chai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…