Tangu nizaliwe, sijawahi kufika Dar es salaam. Naombeni ABC za jiji hilo kabla sijazamia

Tangu nizaliwe, sijawahi kufika Dar es salaam. Naombeni ABC za jiji hilo kabla sijazamia

Kila mtu yuko bize hata asiye na kazi, ni jiji ambalo mtu anaweza kukusalimia ukiwa stendi za daladala kwa tabasamu huku akipanga namna ya kukuuzia siti yake.

Wanawake ni wazuri, wanajua kupendeza na salammu zao ni tamu kuliko asali.!! lakini kumbuka upendo wa Dar unategemea sana unene wa pochi yako.!!

Balance ya akaunti zako ikisoma sifuri, hata salamu hutopata.!!
 
1. Mwonekano wa jiji 2. Watu ni wa aina gani 3. Biashara za mitumba zikoje 4. Hali ya hewa 5. Utapeli na wizi 6. Wanawake nk
Karibu , hapa ni Dari salama au vijana wanaita Bongo. Unaishi kwa urefu wa bongo yako.

MUONEKANO
Utakuta barabara zenye mashimo na wachina wengi wakichimba barabara na kufukia lakini hakuna kazi inafanyika.
Mji una foleni za magari mengi zaidi ya kilometa moja.
Halafu uje na mabuti, mvua ikinyesha to Dar maji mpaka magotini, ila halahala usije zama katika mitaro.

WATU
Utafika na kukuta watu wengi wanatembea tembea, bodaboda zikimbia huku na kule wakati mwingine bila sababu yoyote. Utakuta watu wamevaa kanzu vibargashia na makubazi wanaenda sokoni kununua mahitaji. Utakuta watu wamevaa masuti mazito mazito katika magari makubwa meusi watataka uwapishe mitaani, usipowapisha watakuwashia king'ora.

MITUMBA
Huku mitumba kama kawa, hata ofisi za serkali nje unakuta mzchinga kaning'iniza mitumba yake. Kuna nguo zote hata vichupi na sidiria za wanawake, ni wewe tu.

UTAPELI NA WIZI
Katika masuala hayo hapa ndio chuo kikuu.
Unaweza tapeliwa na mtoto mdogo hadi wazee, Tena utapeli ulioenda shule.
Unaweza kuuziwa msikiti kama unatoka Uskumani na unataka kiwanja.
Mtu anaweza kukujia na masuti ati yeye waziriwa utawala bora, na anataka mpango ili akusaidie uonane na mama. Umeliwa.
Kuibiwa ndo kabisaa!!!
WANAWAKE
Bongo kwa mabibi ndio kwao.

Unataka mswahili, mwarabu au mhindi hadi mzungu kwenye Casino, hela yako.
Ila tahadhari, ukimwi nje nje.
Ila uswahilini kambi ya fisi shillingi 2000/= tu unachukua mzigo.

KARIBU BONGO
 
Back
Top Bottom