Jesusie
JF-Expert Member
- Aug 29, 2021
- 1,466
- 766
==
Baada ya kutazama kipande hiki kifupi cha Video hii wacha sasa nitete na wale tuliosoma Shule za Msingi na Sekondari za Serikali ya Tanzania.
Naamini tutakubaliana kuwa "Tangu Tanzania iwe huru hatujawahi kuwa na shule za Serikali za Msingi na Sekondari zenye hadhi na mwonekano kama hizi zinazojengwa leo na Rais Samia Suluhu Hassan".
Mnaweza kukubaliana na mimi kuwa Rais Samia Suluhu Hassan amekuja na aina mpya kabisa ya utawala na anafanya mambo yake kitofauti sana.
Mtakumbuka Rais Samia Suluhu Hassan ametoa jumla ya madarasa kama haya elfu 18 yaani elfu 15 ya Sekondari na elfu 3 ya Shule za Msingi Shikizi.
Tunaamini, madarasa haya yataongeza hadhi ya wanafunzi na walimu lakini pia yataamsha ari na nguvu ya wanafunzi kupenda shule na madarasa yao.
Tuweni wakweli, hakuna kama Rais Samia Suluhu Hassan na huenda ikatuchukua miaka mingi kumpata mwingine mwenye upendo kama wake.