Tani Elfu 50 za sukari kuingizwa nchini kukabiliana na upungufu uliopo

Tani Elfu 50 za sukari kuingizwa nchini kukabiliana na upungufu uliopo

Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari nchini Tanzania Ndugu Kenneth amesema kuwa katika kukabiliana na upungufu wa sukari hapa nchini, inatarajiwa kuanzia mwezi huu wa januari kuingizwi kwa Tani Elfu Hamsini za Sukari kutoka nje ya Nchi.

Mkurugenzi huyo ameelezea pia sababu ya upungufu wa sukari uliopo hapa nchini na njia au mikakati ambayo inaendelea kufanyika ili kumaliza tatizo hilo.ambapo amesema ya kuwa upungufu huo unatokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini ambapo zinakwamisha shughuli za uvunaji wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

Kwa hiyo uagizwaji na uingizwaji wa Tani hizi za sukari kutoka nje ya nchini kuja hapa Nchini ni katika juhudi za kuongeza kiasi cha upatikanaji wa sukari hapa nchini na kuweza kuendana na mahitaji ya Sukari yanayohitajika.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Inabidi wajifunze kuwa proactive badala ya reactive. Wasiwe wanasubiri tatizo ndipo watafute suluhu wakati ni matatizo yanayojirudia kila mara.
 
Mdogo wangu umeelewa lakini sababu zilizotolewa za kupungua kwa uzalishaji wa sukari kwa kipindi hiki? Au wewe umekimbilia kutoa maoni yako tu yanayokujia kichwani mwako humo😀😀😀
Hizi sababu zipo kila mwaka yani sijui kwanini huwa wanaosimamia mambo hawajifunzi. Sio mara ya kwanza kutokea. Jambo likitokea mara kwa mara tunategemea watu wawe wamejifunza so siku nyingine wanaliwahi kabla ya kutokea. Lakini hapa kwetu kila siku mambo yanajirudia iwe mafuriko jangwani, sukari kuadimika, umeme kupungua. Inabidi tuwe proactive na sio reactive kwa amsuala yanayojirudia kila mara.
 
Kwamba kuagiza ndiyo tumeanza mwaka huu? uoni hata aibu kuandika hiyo taarifa yako?
Ni jambo la kawaida katika masuala ya kibiashara wakati ukiendelea kujiimarisha na kuongeza kiwango cha uzalishaji wako katika kukidhi mahitaji ya soko. Kumbuka ya kuwa matumizi ya sukari nchini yanaongezeka sana hapa nchini kutokana na mambo mengi yanayotumia na kuhitaji sukari yakiongezeka hapa nchini.angalia watu wanaooka maandazi na mikate,l mitaani waliofungua tuviwanda tudogo tudogo jinsi walivyowengi na kutapakaa kila sehemu ,ambapo kwao sukari ni lazima katika utengenezaji.bado viwandani ambapo viwanda vinaongezeka kila siku kutokana na sera nzuri za uwekezaji zilizopo hapa nchini zinazochochea na kuvutia wawekezaji
 
Hivi Azam si alipewa Mashamba alime Miwa na Magu Kule Bagamoyo?Hajafanikiwa kutatua changamoto ya sukari?

Sent from my SM-A107M using JamiiForums mobile app
Anaweza akalima na asikidhi mahitaji ya soko hapa nchini ,maana mahitaji ya sukari yanaongezeka sana hapa nchini.lakini pia hata kama naye angekuwa amelima bado asingeweza kuzalisha sukari ya kutosha wakati huu kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na hivyo kukwamisha uvunaji wa miwa kwa ajili ya kuzalisha sukari.
 
Usinifananishe mimi na Mheshimiwa Mama yetu mpendwa kipenzi cha watanzania Mama Samia Suluhu Hasssan chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia, simba wa nyika, komandoo wa vita,nuru ya wanyonge ,nyota ya matumaini anayefanya kazi na kuchapa kazi mpaka kazi zenyewe zinapiga salute kwake. Mama Samia Ni Mpango wa Mungu Mwenyewe
we bwana umelogwa au ndio mama sami mwenyewe ukiwa gheto na mumeo unaingia jf kujisifu upuuz we sami hata nikisema nikupambanishe kwa uelewa na mtoto wangu wa miaka 8 anakuzidi mara 8 kiufup kakatikie
 
Hizi sababu zipo kila mwaka yani sijui kwanini huwa wanaosimamia mambo hawajifunzi. Sio mara ya kwanza kutokea. Jambo likitokea mara kwa mara tunategemea watu wawe wamejifunza so siku nyingine wanaliwahi kabla ya kutokea. Lakini hapa kwetu kila siku mambo yanajirudia iwe mafuriko jangwani, sukari kuadimika, umeme kupungua. Inabidi tuwe proactive na sio ractive kwa amsuala yanayojirudia kila mara.
Asante kwa ushauri wako mzuri na wenye dhamira njema kwa serikali yetu kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
 
we bwana umelogwa au ndio mama sami mwenyewe ukiwa gheto na mumeo unaingia jf kujisifu upuuz we sami hata nikisema nikupambanishe kwa uelewa na mtoto wangu wa miaka 8 anakuzidi mara 8 kiufup kakatikie
Asante kwa mawazo yako. Mungu akubariki sana na kukujalia maisha marefu yenye heri na amani.
 
Ni jambo la kawaida katika masuala ya kibiashara wakati ukiendelea kujiimarisha na kuongeza kiwango cha uzalishaji wako katika kukidhi mahitaji ya soko. Kumbuka ya kuwa matumizi ya sukari nchini yanaongezeka sana hapa nchini kutokana na mambo mengi yanayotumia na kuhitaji sukari yakiongezeka hapa nchini.angalia watu wanaooka maandazi na mikate,l mitaani waliofungua tuviwanda tudogo tudogo jinsi walivyowengi na kutapakaa kila sehemu ,ambapo kwao sukari ni lazima katika utengenezaji.bado viwandani ambapo viwanda vinaongezeka kila siku kutokana na sera nzuri za uwekezaji zilizopo hapa nchini zinazochochea na kuvutia wawekezaji
Nonsense, kwamba matumizi ya sukari Tz yapo juu kuliko Marekani au Brazil? tuwe wa kweli hatupo serious na kilimo kwenye kuagiza sukari nje watu wanapiga dili zao, kwani tungeamua magereza pekee wazalishe sukari badala ya kuwakalisha ndani nini kingeshindikana? JKT wakazalisha pale Singida alzeti pekee? ni utawala mbovu, kwamba Brazil, Ukraine wao hawana changamoto ndiyo maana hawaagizi kutoka kwetu? sisi ni jambo gani ambalo limefanikiwa kwa hii miaka 63 ya uhuru zaidi ya uchawa? Lini umeona hata DC/RC/Waziri anafanya mdahalo wa kilimo? yamejazwa makada tupu kazi kusifia pekee badala ya kuwa wabunifu. Shame on you
 
Hizi sababu zipo kila mwaka yani sijui kwanini huwa wanaosimamia mambo hawajifunzi. Sio mara ya kwanza kutokea. Jambo likitokea mara kwa mara tunategemea watu wawe wamejifunza so siku nyingine wanaliwahi kabla ya kutokea. Lakini hapa kwetu kila siku mambo yanajirudia iwe mafuriko jangwani, sukari kuadimika, umeme kupungua. Inabidi tuwe proactive na sio reactive kwa amsuala yanayojirudia kila mara.
Kwanza ni sababu za kipumbavu na aibu kwa taifa lenye ardhi nzuri kama hili, shinda ni uongozi mbovu wa kujaza machawa kwenye nafasi nyeti kama hizi badala ya nafasi zitangazwe waombe watu wenye uwezo wamejaa makada na chawa.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari nchini Tanzania Ndugu Kenneth Bengesi amesema kuwa katika kukabiliana na upungufu wa sukari hapa nchini, inatarajiwa kuanzia mwezi huu wa januari kuingizwa kwa Tani Elfu Hamsini za Sukari kutoka nje ya Nchi.

Mkurugenzi huyo ameelezea pia sababu ya upungufu wa sukari uliopo hapa nchini na njia au mikakati ambayo inaendelea kufanyika ili kumaliza tatizo hilo.ambapo amesema ya kuwa upungufu huo unatokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini ambapo zinakwamisha shughuli za uvunaji wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

Kwa hiyo uagizwaji na uingizwaji wa Tani hizi za sukari kutoka nje ya nchini kuja hapa Nchini ni katika juhudi za kuongeza kiasi cha upatikanaji wa sukari hapa nchini na kuweza kuendana na mahitaji ya Sukari yanayohitajika.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Mnatarajia mhi
 
Back
Top Bottom