Tani Elfu 50 za sukari kuingizwa nchini kukabiliana na upungufu uliopo

Tani Elfu 50 za sukari kuingizwa nchini kukabiliana na upungufu uliopo

Huna akili.

Mvua imezuia uzalishaji sukari.

Mvua imesababisha upungufu uzalishaji umeme.::NCHI YA PWAGU NA PWAGUZI
Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo matusi. Ungeuliza ni vipi mvua imekwamisha uzalishaji wa sukari viwandani. Jibu ni kuwa uvunaji wa miwa umekuwa ni mgumu wakati huu wa mvua nyingi zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
 
Tstizo nyie hamuoni mbele hamjui kutathmini uzalishaji na ujazo wa sukari.
Habari ya mvua tuliambiwa miezi kadhaa na kama mnajua athari zake mlichukua hatua gani kuepusha kadhia hii?
Nyie mpo mpo tuu, bodi na wizara watendaji wanasubiri mishahara posho marupurupu na makandokando mengine na kuachia mambo yajiendee yenyewe
Halafu iweje tatizo hili hujorudia kila ikikaribia mfungo wa Ramadan no matter ukiwa December,June au hata January?😡
Acha lawama zisizo na msingi ndugu yangu.kwa hiyo ulitaka miwa ivunwe Kabya haijakomaa? Hujuwi kuwa kuna wakati wa kuvuna na huwezi ukavuna kabla kwa kuwa inakuwa bado haijakomaa?
 
Leo Supermarket za Mr Discount sukari mwisho kununua mfuko mmoja, juzi ilikuwa mifuko miwili.
 
Ndugu zangu Watanzania,

Mkurugenzi mkuu wa bodi ya Sukari nchini Tanzania Ndugu Kenneth Bengesi amesema kuwa katika kukabiliana na upungufu wa sukari hapa nchini, inatarajiwa kuanzia mwezi huu wa januari kuingizwa kwa Tani Elfu Hamsini za Sukari kutoka nje ya Nchi.

Mkurugenzi huyo ameelezea pia sababu ya upungufu wa sukari uliopo hapa nchini na njia au mikakati ambayo inaendelea kufanyika ili kumaliza tatizo hilo.ambapo amesema ya kuwa upungufu huo unatokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hapa nchini ambapo zinakwamisha shughuli za uvunaji wa miwa kwa ajili ya uzalishaji wa sukari.

Kwa hiyo uagizwaji na uingizwaji wa Tani hizi za sukari kutoka nje ya nchini kuja hapa Nchini ni katika juhudi za kuongeza kiasi cha upatikanaji wa sukari hapa nchini na kuweza kuendana na mahitaji ya Sukari yanayohitajika.

Kazi iendelee,Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
Deal za watu dhidi ya viwanda vya ndani
 
Tani 50elfu ni kidogo sana ukilinganisha matumizi ya nchi ,,kwanini nchi yetu inashindwa kujitosheleza na vitu vidogo kama sukari .

Aridhi ,watu,maji, tunavyo shida nini ??? Au kuna ubinfsi unakumbatiwa ??
 
Hoja hujibiwa kwa hoja na siyo matusi. Ungeuliza ni vipi mvua imekwamisha uzalishaji wa sukari viwandani. Jibu ni kuwa uvunaji wa miwa umekuwa ni mgumu wakati huu wa mvua nyingi zinazoendelea kunyesha hapa nchini.
na uzalishaji umeme tupe majibu ya tatizo lilipo
 
na uzalishaji umeme tupe majibu ya tatizo lilipo
Tatizo la umeme linakwenda kubaki historia katika vitabu vya historia.maana muda siyo mrefu mtambo wakwanza unakwenda kuwashwa katika bwawa la mwalimu Nyerere. ambapo megawati zake zitaunganishwa katika grid ya Taifa. Kwa sasa pia serikali inaendelea kuimarisha vyanzo vingine vya umeme ili hata kukitokea mabadiliko ya tabia nchi basi kusiathiri upatikanaji wa umeme.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Tani 50elfu ni kidogo sana ukilinganisha matumizi ya nchi ,,kwanini nchi yetu inashindwa kujitosheleza na vitu vidogo kama sukari .

Aridhi ,watu,maji, tunavyo shida nini ??? Au kuna ubinfsi unakumbatiwa ??
Tani za sukari zitaendelea kuingia mpaka zikidhi mahitaji yetu wakati nasi pia tukiendelea kuzalisha sukari ya ndani pale mvua zitakapo pungua na kuanza kutoa nafsi ya kuvuna miwa.
 
Tatizo la umeme linakwenda kubaki historia katika vitabu vya historia.maana muda siyo mrefu mtambo wakwanza unakwenda kuwashwa katika bwawa la mwalimu Nyerere. ambapo megawati zake zitaunganishwa katika grid ya Taifa. Kwa sasa pia serikali inaendelea kuimarisha vyanzo vingine vya umeme ili hata kukitokea mabadiliko ya tabia nchi basi kusiathiri upatikanaji wa umeme.
hata la sukari litaki historia ila nipe majibu kwanini hadi sasa hakuna umeme na mvua kedekede
 
Back
Top Bottom