Godman
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 423
- 650
Wakuu! Habari za muda huu, sijui ni nani anayewashauri hawa TANROAD wa Iringa, mwezi wa pili mwanzoni waliipa tenda ya kuziba viraka kwenye Barabara ya Iringa to Dodoma Kampuni iitwayo TS Solutions (T) Limited ya Kipunguni, Kizinga area Dar es salaam.
Kampuni hii imefanya kazi hiyo katika eneo la Mlima Nyang'oro hadi karibu na Kijiji Cha Migoli, hivi karibuni Kampuni hii iliishiwa baadhi ya "Material" na walikuwa wanasubiri yaletwe ili waendelee na kazi.
Cha ajabu wakati wanasubiri hayo "Material" Kuna Kampuni nyingine iitwayo Kings ya Madare Dar es salaam nayo imepewa tenda katika eneo ambalo Kampuni ya awali iliziba viraka siku chache nyuma,.
Hii sasa imepewa tenda ya kufumua lami yote takribani kilometa tatu eneo ambalo tayari lilishazibwa viraka na Kampuni ya awali, kwangu haya naona ni matumizi mabaya ya fedha za walipa Kodi.
Iweje kipande hicho hicho zipewe tenda Kampuni mbili tofauti ndani ya muda mfupi? Kwa nini sasa badala ya kuziba viraka siku chache nyuma, wangeamua kuifumua yote kama wanavyofanya sasa? Kama bajeti ilikuwa bado ya kufumua basi baada ya kupata hizo fedha kwa nini wasingeelekeza eneo lingine kuliko eneo hilo hilo kupewa tenda Kampuni mbili tofauti?