Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Morogoro wameendelea kuchukua hatua za haraka kuziba mashimo yaliyotokeza katika barabara kuu ya Morogoro – Iringa hasa eneo la hifadhi ya Taifa Mikumi kutokana na mvua kubwa zinazonyesha kwa wiki ya pili mfululizo Mkoani humo.
Hayo yameelezwa na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Mhandisi Alinanuswe L. Kyamba ambapo amesema eneo la mikumi kumejitokeza mashimo mengi, yaliyotokana na athari za mvua lakini TANROADS wamechukua hatua za kutatua changamoto hiyo kwa haraka kwa kuziba mashimo yote.
Ameeleza mvua nyingi zinaponyesha muda mrefu barabara inameza maji na kusababisha ifumuke na kwamba sehemu kubwa iliyoathiriwa kwenye barabara hiyo ni katikati ya Hifadhi ya Mikumi lakini TANROADS imeamua kuziba mashimo katika barabara yote kuanzia Msamvu - Mikumi - Iyovi hadi mpakani na Iringa.