TANROADS na TRC wekeni matuta kwenye makutano ya barabara na njia za treni; Alama na ishara hazitoshi maeneo hayo

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Ile kanuni ya treni kwamba huwa haigongi bali hugongwa haikuwa na maana hii kama inavyoelezwa na wengi!

Kama ni sheria au kanuni Basi waliopitisha hawakufikilia vizuri!

Treni haigongi porini lakini linapokuja suala la muingiliano wa njia za treni na barabara treni inaweza kugonga!

Kwasababu siyo watumiaji wote wa barabara wana macho au wanajua lugha!

Pia kuna wageni wa njia au pengine vibao vya alama kung'oka au kufunikwa na majani visiweze kuonekana kirahisi!

Hivyo kutokana na hatari iliyopo nashauri TANROADS na TRC wekeni matuta maeneo hayo!

Halafu Pia kuna zile njia za treni zilizokufa (ambazo hazitumiki) nashauri nazo muondoe yale mataaruma ya reli barabarani kwasababu yanaumiza pia huleta taharuki na usumbufu kwa madereva.

Tunalipia road license wajameni msitufanyie hivyo wateja wenu!
 
Kwasababu siyo watumiaji wote wa barabara wana macho au wanajua lugha!
Pia kuna wageni wa njia au pengine vibao vya alama kung'oka au kufunikwa na majani visiweze kuonekana kirahisi!

Hivyo kutokana na hatari iliyopo nashauri Tanroad na TRC wekeni matuta maeneo hayo!
Na leo asubuhi treni imegeuza gari chapati Morogoro, nashauri ziwekwe barrier za umeme zenye sensors
 
Alafu watu waje waibe hizo sensor au umeme umekatika sensor hazipigi kazi. ishu waweke matuta tu..lakini pia tuna madereva wapuuzi wanasikia treni inakuja ila wanaforce wapite..matuta yawekwe yale makubwa gari ikifika ipande kwa tabu..ila matuta yake rafiki ili hata wenye baby Walker tusikwaruze chini
 
Ile kanuni ya treni kwamba huwa haigongi Bali hugongwa haikuwa na maana hii kama inavyoelezwa na wengi!
Kama ni sheria au kanuni Basi waliopitisha hawakufikilia vizuri!

Treni haigongi porini lakini linapokuja swala la muingiliano wa njia za treni na barabara treni inaweza kugonga!

Kwasababu siyo watumiaji wote wa barabara wana macho au wanajua lugha!
Pia kuna wageni wa njia au pengine vibao vya alama kung'oka au kufunikwa na majani visiweze kuonekana kirahisi!

Hivyo kutokana na hatari iliyopo nashauri Tanroad na TRC wekeni matuta maeneo hayo!

Halafu Pia kuna zile njia za treni zilizokufa (ambazo hazitumiki) nashauri nazo muondoe yale mataaruma ya reli barabarani kwasababu yanaumiza pia huleta taharuki na usumbufu kwa madereva.

Tunalipia road license wajameni msitufanyie hivyo wateja wenu!
Inshu sio matuta, kwa dreva aliyepitia chuoni anafahamu kabisa kuwa unapoona reli imekatiza barabara lazima upunguze mwendo, na kuangalia, na kuna alama za zege kabisa kuonyesha uwepo wa kuviko cha treni.Ni mapuuzo tu ya sheria.
 
Hadi uione kumbuka unakuwa umepita au umefikia reli
 
Kuna uzembe mwingi unafanywa na Shirika la reli, baadhi ya maeneo kuna majani marefu kama msitu na ni ngumu kuona kama treni inakuja
Hapana sio kweli!!kwani malanyingi huwa zinakuwa sehemu iliyonyooka, ili kuweza kuiona hata kwa mbali, na ishara pia huwekwa
 
Madereva wa magari Wanaogongwa kwenye treni hupita na ndege kama matuta kote yapo?
 
Alafu watu waje waibe hizo sensor au umeme umekatika sensor hazipigi kazi. ishu waweke matuta tu..lakini pia tuna madereva wapuuzi wanasikia treni inakuja ila wanaforce wapite..matuta yawekwe yale makubwa gari ikifika ipande kwa tabu..ila matuta yake rafiki ili hata wenye baby Walker tusikwaruze chini
Unajua matuta yanaharibu magari????
 
Na leo asubuhi treni imegeuza gari chapati Morogoro, nashauri ziwekwe barrier za umeme zenye sensors
Umenikumbusha project yangu ya pale FoE, UDSM enzi hizo... Nilitengeneza protype ya hii kitu..!! LAKINI zile projects huwa zinaishia pale.

Na kuna vijana walitengeneza ya LUKU kwamba ukinunua luku kwa simu, wakala au TANESCO wenyewe, huna haja ya kuingiza zile namba kwenye mita au kirimoti chake, ukishanunua tu umeme unaingia straight kwenye mita yako
 
Kuna uzembe mwingi unafanywa na Shirika la reli, baadhi ya maeneo kuna majani marefu kama msitu na ni ngumu kuona kama treni inakuja
Siyo TRC peke yao kwenye hili, hata wanaoshughurika na barabara. Kuna blind corners nyingi sana karibu na vivuko vya treni, iwe kwa majani, milima etc
 
Umenikumbusha project yangu ya pale FoE, UDSM enzi hizo... Nilitengeneza protype ya hii kitu..!! LAKINI zile projects huwa zinaishia pale.

Na kuna vijana walitengeneza ya LUKU kwamba ukinunua luku kwa simu, wakala au TANESCO wenyewe, huna haja ya kuingiza zile namba kwenye mita au kirimoti chake, ukishanunua tu umeme unaingia straight kwenye mita yako
 
Umenikumbusha project yangu ya pale FoE, UDSM enzi hizo... Nilitengeneza protype ya hii kitu..!! LAKINI zile projects huwa zinaishia pale.

Na kuna vijana walitengeneza ya LUKU kwamba ukinunua luku kwa simu, wakala au TANESCO wenyewe, huna haja ya kuingiza zile namba kwenye mita au kirimoti chake, ukishanunua tu umeme unaingia straight kwenye mita yako
Angefanya mtoto wao ungesikia wakilishupalia Bungeni ila kwakuwa ulifanya mtu mwenye utashi unaojitegemea walikuona ni threat utachukua nafasi zao wakaizima
 
ishu waweke matuta tu..
Pale Morogoro karibu na Tanesco kuna crossway sign na matuta kila upande lakini panatafuna watu na magari kila mwaka kadhalika maeneo mengine mengi tu Tanga, Dar ni hivyo, wakiweka mifumo ya umeme ni salama, mbona wana vibanda vya walinzi mle kwenye crossway wanalinda nini zaidi ya kuvutia wanawake usiku mle
 
Back
Top Bottom