Tanzania 0-1 Uganda, kipigo kilikuwa ni haki yetu Watanzania, kwa sababu hizi....

Tanzania 0-1 Uganda, kipigo kilikuwa ni haki yetu Watanzania, kwa sababu hizi....

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Timu ya Tanzania imepoteza kwa bao 1-0 dhidi ya Uganga katika mchezo wa kuwania kufuzu CHA, leo Agosti 28, 2022

Japokuwa kuna mchezo wa marudio baina ya timu hiyo unaotarajiwa kuchezwa Septemba 3, 2022, lakini niwe mkweli ili kufanikiwa kufuzu basi kuna kitu kikubwa cha ziada kinatakiwa kifanyike, tofauti na hapo Uganda wapo mbali zaidi kuliko sisi.

Kuna mambo kadhaa ambayo yamechangia kupoteza mchezo huo:

WACHEZAJI HAWACHEZI KITIMU
Kuanzia kipindi cha kwanza hadi dakika 90 zinakamilika bila shaka ilionekana wazi ni kama hakukuwa na chemistry baina ya mchezaji mmoja na mwingine.

MENTALITY YA WACHEZAJI
Ukiangalia vizuri wachezaji wa Uganda walivyokuwa wakifanya baadhi ya vitu vidogovidogo kama kupoteza muda, kucheza na refa, kufanya vitu kadhaa ili wapoteze muda au wawatoe kwenye focus wapinzani wao, ni tofauti kabisa na ilivyokuwa kwa wachezaji wa Tanzania.

Wachezaji wa Tanzania ni kama walikuwa hawategui mitego ya wapinzani wao, na ndio maana nasema mentality ilikuwa tofauti na ilivyotakiwa kuwa.

HAKUNA PASSION
Hii hasa ni kwa wachezaji, asilimia kubwa au wote ni kama hawakuwa na passion ya kuichezea timu hiyo.

Watazame wachezaji walivyokuwa wakicheza, watazame na hao hao wakiwa ngazi ya klabu zao, ni tofauti kabisa, hata bao lilivyofungwa ni wazi kulionekana hakuna passion na focus ya mchezo ilikuwa chini.

KILA MCHEZAJI ANACHEZA KIBINAFSI
Tazama wachezaji wa Uganda walivyokuwa wakicheza ki strategy, kila move walikuwa wanajua inaenda wapi na kwa sababu gani. Nyota wa Tanzania kuuchukua mpira kupiga chenga, madoido ilikuwa kawaida na mengine hata hayakuwa na msingi kulingana na uhalisia uhitaji wa matokeo.

REFA YUPO KWETU LAKINI KAMA YUPO UGENINI
Mwamuzi wa kati hakuwa na presha kutoka kwa wachezaji wetu na ndio maana kuna amtukio yalioonekana wazi angeweza kuifikiria Tanzania, lakini kwa inavyoonekana ‘hawakujua kucheza naye’ matokeo yake katuminya.

ONE v ONE UGANDA WAPO VIZURI
Nguvu ya mchezaji mmoja mmoja wachezaji wa Tanzania wengi hawakuwa na nguvu ya kushindana na Waganda ndio maana mipira mingi ikawa inachukuliwa au kuanza kuguswa na Waganda.
 
Ile umbwa beki ya simba ya pembeni ndio imetoa boko mbwa yule!
 
Na tumetoka pale PTA ambapo timu yetu ya taifa ya netball ilikua ni vichekesho vitupu, eti tunafungwa na Eswatini!!,aibu na iwe mwisho kuwa na coach mwanajeshi hawezi hata kujieleza kwa kiswahili, shame!!
 
Mpira wa vilabu, hasa Simba na Yanga siku zote ndiyo unaharibu timu ya taifa. Tukiongelea siasa inaharibu mpira wetu huu ni mmoja wa uthibitisho.

Unachagua wachezaji ambao hata kwenye vilabu vyao hawana uhakika wa kucheza kisa ni anatoka timu hizi. Wakifika kule kama mtoa mada anavyosema, hawachezi kwa passion maana loyalty yao iko kwa club zao zaidi ya timu ya taifa.
 
Hata mechi ya marudiano huko Uganda sioni tumaini kabisa.
Hiyo mechi bora waite wale watoto kina tepsie Evans na wacheza wengine ambao team zao hazishiriki Caf champions league maana inaanza September 6 na mechi inachezwa September 3 hapo watacheza kwa tahadhari ili wasiumie waende wakacheze Caf kama leo Uganda wanakimbia Tanzania inatembea.
 
Haiwezekani kupatikana timu ya Taifa bila wachezaji wa Simba na Yanga?
Tusipo ondoka hapo hatutoboi.
 
Mwamnyeto kalala chini badala ya kukaba.
Alikula chenga kibwana. Lkn kosa lilianza kwa dogo Evance kupiga kona kimo kifupi ikadakwa, zimbwe akataka kuonesha umwamba, Mwamnyeto nae alkua kasogea mbele sana. Hata hivo speed ya recovery ni ndogo sana.
 
Ukweli timu ya Uganda imewekeza Kwa wachezaji vijana academy, ni mchezaji Gani wa Tanzania angeweza kuchukua mpira akawa na utulivu akapiga chenga na kufunga kama yule mganda mchawi ni uwekezaji wetu Kwa timu za vijana
 
Back
Top Bottom