Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Namjua mzee mmoja huko daslam ana nyumba 300 lakini anatembelea pikipiki,
Baada ya kuuliza sana nikaambiwa akihitaji gari anakodisha lakini hamiliki
Kumiliki nyumba pia ni indicator ya uwezo wa juu wa kiuchumi wa mtu.. Kuna mtu hawezi hata kukodi gari, yeye uwezo wake ni bodaboda au baiskeli. Lakini pia inategemea ni nyumba za aina gani? Za miti na juu nyasi? All in all indicators za kufanya wealth ranking mojawapo ni kumiliki nyumba...
 
Shida sio kujenga Viwanda bali ni kuweka mifumo endelevu na kuwekeza kwenye elimu ya watu,sasa hayo hayakufanyika..

Miaka 25 tulitegemea tuwe sehemu nzuri kidogo maana wewe unasema viwanda wakati hata malighafi yalikuwa ni yale wazungu waliacha..

Uchumi wa mkoloni ulikuwa mzuri kuliko wa Tanganyika..

Huu ni ukweli kwamba Misingi haikuwekwa vizuri ndio maana hata waliofuata kila mtu akawa anafanya lake.
Tulikuwa bize kuwasaidia wenzetu wajikomboe na kuwa nchi huru na kuwafukuza wakoloni [emoji23] [emoji23]
 
Hauelewi chochote kuhusu kodi kubwa wanazozisema wadau.
Kabisa, pia inategemea na umakini kwenye kununua kwa mtu, mimi gari ya kwanza nilinunua kwa mtu wa pili na niliitumia miaka 7 bila shida yoyote (ukiondoa minor services) mpaka nilipoiuza ili kununua nyingine..
 
Hivi shetani aliyepanga kodi ya kamkomeni namna hiyo bado hajafa?

Vyovyote iwevyo, kwanini wabunge wasi review kodi hii ya kinyang'au na kuipigia kelele mpaka kikaeleweka?
Wabunge hawawezi coz wao wanapewa milioni 200 mkopo wa gari na mengineyo... Wakijifanya kutetea sana wanaitwa kwenye kamati zao na kupigwa mkwara
 
Kwa ulimwengu wa SAsa ant dumping ni useless principal.sababu antidumping uja kumezwa na scrapping principal yaani kitu au gari likifika mwisho linaenda screpa kukatwa chuma chakavu then linarudi kiwandani kama raw materials ya kuzalisha tena gari.
Sahihi kabisa, hebu kwa mfano hapa Tanzania ni wapi huko utakuta migari chakavu imetupwa kama Ulaya? Mwezi uliopita nilikuwa Morogoro, Kihonda naelekea Veta. Kuna jamaa mmoja baada ya kupiga pombe sana pale Wallet Pub akatoka na gari yake mpya tuu Toyota Premio kama sikosei.. Alikuwa spidi hatari, akawa anaeakosa kosa watu njiani na bodaboda. Kufika maeneo ya shule ya msingi NOTO akamgonga boda boda aliyekuwa na abiria na kuwaumiza, na gari inaingia kwenye kimtaro. Dakika tuu bodaboda wskajaa na kumuweka kati na kwenye hizo purukushani gari ikawaka moto yoooteee na ikawa screpa.. Jamaa kwa kuchanganyikiwa akawa anarudi mjini kwa mguu. Asubuhi napita nikakuta ile screpa imeshanyofolewa kila kitu imebaki fremu tuu, na yenyewe after 3 days imebebwa... [emoji23] [emoji23]
 
Umesahau kwamba mpaka miaka ya karibuni piki piki na magari yalikua yana share number. Means kama ingekua kama sasa kwamba gari zisimame zenyewe inawezekana namba E ingesogea mpaka miaka 4 mbele, so piga hesabu upya.
Mkuu kwani zile za pikipiki hazikua replace na gari?

Basi kweli kama ndio hivyo namba D ingeweza kuja mwaka 2027, yaani tuangize gari 517k kwa miaka 13.

Hii nchi bado masikini sana. Maisha ni magumu sana.
 
Hata hayo 500000+ bado pikipiki nyingi zilichangia hiyo D kukimbia zaidi, maana hadi 2013 pikipiki zilikuwa zatumia D
 
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.

Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.

Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.

Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.

Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.

Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.

Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.

Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu😂. Aibu ya mwaka.

Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.
Na wengi Sasa eti wanasubir namba E ianze ndo waagize magar yao
 
Umesahau kwamba mpaka miaka ya karibuni piki piki na magari yalikua yana share number. Means kama ingekua kama sasa kwamba gari zisimame zenyewe inawezekana namba E ingesogea mpaka miaka 4 mbele, so piga hesabu upya.
Sijui waliogopa Nini?? Kwanza wanataka Txxx zikae mpaka lini. Wangeacha ziende pamoja, baada ya hpo wangeleta ubunifu mwingne wa namba
 
Hii ni kwasababu gari serikali imeifanya kama luxury commodity,kodi inakaribia nusu ya bei ya gari...gari inauzwa Japan/UK kiasi cha $3000 hadi ifike Dar port yaweza kua $3500 ila sasa kuitoa hapo uwenayo mkononi kodi inaweza kua hadi $2500 utashangaa ile gari utaipata kwa $6000 ....iyo kodi waipunguze kwa nusu ili watu waagize magari kwa wingi pesa watapata tu kupitia kuuza mafuta,vipuri,parking kwenye maeneo ya manispaa nk ...
Gari kwa sasa ni kama tu simu ,pikipiki sio usafiri rasmi mana risk yake ni kubwa sana na ndio imekua kama usafiri rasmi sasa

Gari zikiagizwa kwa wingi zitachochea pia biashara, KAZI na guess nyingine nyingine ambapo serikali itapata kodi kubwa zaidi.
 
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.

Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.

Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.

Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.

Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.

Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.

Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.

Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu😂. Aibu ya mwaka.

Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.
Msema kweli mpenzi wa Mungu
 
Back
Top Bottom