Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Kuna jamaa kasaidia watu kama wewe kuewa hapo juu. Kaandika hivi.

Moja ya kipimo cha umasikini au utajiri (poverty & wealth ranking) ni kuangalia mali mtu anazomiliki kwa mfano nyumba (ya miti & udongo, ya matofali, nyasi fulu suti etc), baiskeli, Pikipiki, gari etc... Mfano kama wewe humiliki hata bodaboda au baiskeli, huna nyumba hata ya matope na nyasi wewe tayari una indicators za umasikini...
Namjua mzee mmoja huko daslam ana nyumba 300 lakini anatembelea pikipiki,
Baada ya kuuliza sana nikaambiwa akihitaji gari anakodisha lakini hamiliki
 
Hayo ya 2010-2021 ni kwa matumizi ya serikali tu na mafisadi makubwa,serikali haijui kodi wao nikuleta na kutumia,halafu wakapaisha kodi badala ya kushusha na kuyapandisha kodi magari ya zamani.
 
Watu kwa ground wanauziana magari hum hum bongo, maelfu kwa maelf, kama huamn fuatilia utitili wa platform mbalimbal za madalali wanaopromote na kuuza magari ndipo utajua ukwel.

Kinachofanya watu wasiagize nje ni hiyo tabia ya kotoza kodi ndefu ambapo kihalali haikutakiwa iwe hivyo,so bora tuuziane humu humu
Yaani.. Kodi kubwa sana aisee... Unaweza kukuta gari inauzwa Milioni 3 huko Japan, ila ikija hapo bandarini unapigwa mil 8... Maninaaa!!!! Nchi hii ngumu sana...

Sent from my TECNO LA7 using JamiiForums mobile app
 
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.

Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.

Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.

Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.

Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.

Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.

Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.

Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu😂. Aibu ya mwaka.

Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.
Si bora magari unaweza sema kwa bongo ni anasa..

Baada ya miaka 60,installed capacity ya Umeme ni megawatt 1500 tuu na bado hatuzimalizi 😆😆.

Nadhani makosa yalifanyika kuanzia awamu ya kwanza kwa waliojenga msingi..

Kama mambo yatafangika na kutekelezwa Kwa namna mipango ilivyo sasa,naona Rais Samia atatuvusha kidogo ila kuna vitu vinatakiwa kubadilika.
 
Ni kweli lakini huko vijijini kuna barabara? Hebu jiulize barabara zilizopo kijijini kwenu ukiwa na gari litadumu??? Utaweza kuwa na gari la kawaida kijijini kwenu?

Nchi za wenzetu wana barabara zinazoopitika vizuri mpaka vijijini ndio maana magari wanayo.

Lakini pia vijiji vya tanzania wengi wanahali duni ambapo sidhani kama wanaweza kuhimili shs 3,400 ya lita moja ya mafuta. Kimsingi uchumi wa magari upo mijini, vijijini wakinayo wachache kusafirisha wengine inatosha maana wakulima na wafugaji wengi hawawezi kumudu gharama za kumiliki gari wacha tu manunuzi.
Hii ni hoja dhaifu sana na sijui kama umetembelea vijiji vingapi nchini. Kwanza nimekuambia magari ya wakulima na wafugaji ni pick up, Fuso, matrekta, piki piki za miguu mitatu, malori etc... Sijasema Vitz au IST au carina... Mwezi huu niko vijiji vya wilaya ya Tanganyika, mkoani Katavi na barabara za moram na za vumbi zimejaa magari kibao NOA, Brevis nk lakini kuna mafuso mpaka Tandam zinasomba mahindi na mpunga. Vijijini huku Sibwesa, Kamilala, Kapanga,Mwese, Katuma nk Hiace, pick up, matrekta nayaona. Nilikuwa Kigoma, Uvinza vijiji vya Koga, Rukoma nk kote huko magari yanaweza kufanya kazi. Ukienda Morogoro, Mvomero Noa, Hiace mpaka saloon zinaenda mpaka vijiji vya Dihinda, Msolokelo, Kanga, Mziha, Ndole.. Kwenye hoja ya eti wakulima ni masikini pia kumbuka si wote, kuna wenye uwezo mkubwa tuu... Ni dhana potovu sana kudhani eti magari sehemu yake ni mijini kwenye barabara za lami. Ukiangalia nchi zenye uzalishaji mkubwa wa mazao sababu kubwa ni kutumia mashine (mechanization kwenye kilimo) kama matrekta kulima, magari kubeba mazao, mashine za kupukuchulia mahindi nk
 
Si bora magari unaweza sema kwa bongo ni anasa..

Baada ya miaka 60,installed capacity ya Umeme ni megawatt 1500 tuu na bado hatuzimalizi 😆😆.

Nadhani makosa yalifanyika kuanzia awamu ya kwanza kwa waliojenga msingi..

Kama mambo yatafangika na kutekelezwa Kwa namna mipango ilivyo sasa,naona Rais Samia atatuvusha kidogo ila kuna vitu vinatakiwa kubadilika.
Mkuu awamu ya kwanza utawalaumu bure, kumbuka awamu ya kwanza walijenga viwanda karibu kila kona na watu walikua milioni 8. Leo tuko milioni 60.

Awamu ya kwanza walijenga reli, viwanja vya ndege na barabara kadhaa.

Tujiulize, kama awamu ya kwanza walifanya makosa, tumeshindwaje kuyarekebisha kwa miaka 38 toka awamu ya kwanza itoke.

Baada ya awamu ya kwanza zikaja awamu za rushwa, ufisadi, kuuza viwanda, kuuza kila kitu cha serikali.

Ni aibu nchi ya watu milioni 60 hatumalizi megawati 1500😂. Hii maana yake ni kwamba karibu 80% au zaidi ya watanzania wanaishi kwenye giza😂 wakitumia mikaa, kuni na mafuta ya taa, wakimulikia vijinga vya moto.

Hii nchi imenajisiwa vya kutosha na ccm.
 
Shida sio kujenga Viwanda bali ni kuweka mifumo endelevu na kuwekeza kwenye elimu ya watu,sasa hayo hayakufanyika..

Miaka 25 tulitegemea tuwe sehemu nzuri kidogo maana wewe unasema viwanda wakati hata malighafi yalikuwa ni yale wazungu waliacha..

Uchumi wa mkoloni ulikuwa mzuri kuliko wa Tanganyika..

Huu ni ukweli kwamba Misingi haikuwekwa vizuri ndio maana hata waliofuata kila mtu akawa anafanya lake.
 
Gari haitakiwi iwe na mmiliki zaidi ya wawili zaidi ya hapo inageuka ni chombo cha kuchafua mazingira inatakiwa ipelekwe screpa yadi ikakatwe katwe.
Ila sababu ya kodi kubwa unakuta gari imepita kwenye mikono kumi
Hauelewi chochote kuhusu kodi kubwa wanazozisema wadau.
 
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.

Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.

Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.

Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.

Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.

Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.

Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.

Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu😂. Aibu ya mwaka.

Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.
Tatizo pia ni Kodi! Mfano BMW X3 ya Mwaka 2006-12 Bei yake mpaka Bandali ya Dar es salaam ni kati ya Millioni 8 mpaka 15.Kodi yake ni kuanzia Million 11 na kuendele.
 
Hayo ya 2010-2021 ni kwa matumizi ya serikali tu na mafisadi makubwa,serikali haijui kodi wao nikuleta na kutumia,halafu wakapaisha kodi badala ya kushusha na kuyapandisha kodi magari ya zamani.
Ni anti-dumping,unalinda Pato la nchi kwa ku-frusrate matumizi hayo
 
Hili jambo huwa linanishangaza mnooo, kuna siku nilisikiliza clip ya Chris Lukosi, yule mhehe wa minada ya mtandaoni ya makanikia, akisema TZ kodi huwa inazidi mpaka pesa ya kununulia gari daah...
Hivi shetani aliyepanga kodi ya kamkomeni namna hiyo bado hajafa?

Vyovyote iwevyo, kwanini wabunge wasi review kodi hii ya kinyang'au na kuipigia kelele mpaka kikaeleweka?
 
Kodi za magari tanazania hii ndo inaleta kikwazo magari used lakini mpaka yafike kwa mtumiaji gharama zake bora uende kenya.
 
Inaitwa anti-dumping,unalinda forex zako
Kwa ulimwengu wa SAsa ant dumping ni useless principal.sababu antidumping uja kumezwa na scrapping principal yaani kitu au gari likifika mwisho linaenda screpa kukatwa chuma chakavu then linarudi kiwandani kama raw materials ya kuzalisha tena gari.
 
Back
Top Bottom