Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Tanzania bado nchi masikini sana, kwa miaka 8 watanzania wameagiza magari 561,875

Kwani magari ni utajili? Nani alikwambia Watanzania wakinunua magari wengi ndio ishara ya kuondokana na umasikini? Kwanza elezea umasikini upi ulikusudia maana Watanzania wengi ni maskini wa akili unakuta msomi PhD anagang'ana na siasa uyo ni masikini wa akili,
Kuna wasiojua Ccm inavyotafuna nchi kutwa kucheza iyena iyena ao nao ni maskini wa akili na wengine niwezi wa mali za Umma wanaiba mabilion ya kodi zetu wanaenda kuzificha ughaibuni wakifa zile fedha uchukuliwa na wazungu awa nao ni maskini wa akili.
Na wengi itakuwa wanakufa tu na pesa zinapotelea huko.
Umasikini wa Kwanza wa viongozi wa kibongoland ni kuwa na afya mbovu.
Hawa Jamaa wakipataga tu uongozi wanaanza kunenepa Ile mbaya wengi wao wanakuaga wa duara,yaani fat and shapeless,nadhani ndio hapo akili zao huanza kupata kutu, na hapo unakuta ni Prof.ana PhD zake kadhaa,lakini eti anashindwa ku practise maisha yenye afya wao kutwa kuchwa ni kunywaa mabiere wanashindwa kutambua kula na kunywa sana bila mpangilio ni mwanzo wa kuanza kufa mapema,japo wote tutakufa lakini kufa Kwa kuanza kuharibu afya Tena Kwa mtu msomi huo ni umasikini.
 
Pengine ungeweka ulinganishi na nchi nyingine kama kenya au afrika kusini ili uweze kuonyesha haya ni machache au mengi.
Kwa tanzania kodi ya magari bado ipo juu sana yaani 100% ya bei ya ununuzi , hiki nadhani ni kikwazo.

Lakini pia barabra zetu bado sio za kutosha magari mengi hasa miji mikubwa kama Dar, Arusha au Mwanza. Barabara zetu zinahitaji kuwa kubwa ili ziweze kuhimili magari mengi zaidi.
Lakini pia nadhani serikali inahitaji kuweka kizuizi cha uchakavu angalau miaka 10 ili nchi isiendelee kuwa jalala la magari mabovu. Wenzetu hapo Ke gari mwisho miaka 8 tu.

Usafiri ndo gharama
 
Mkuu herufi ni 24 na sio 25. Kumbuka herufi I na O zinarukwa. Rudia upya calculations zako
Mahesabu si ndio yatakuwa chini zaidi? Ujumbe umeeleweka.
 
Hata kama ni kodi, bado haiondoi hoja ya jamaa....
Wenzetu mbona wanannunua mapya, gari ist inauzwa usd 25,000...

Kwahiyo idadi ya mdau aliyotaja, kuna watu wanamiliki gari zaidi ya moja....

Kwa kukadiria, watanzania wenye magari hawazidi 300,000
Acha kutushika wewe .. hao laki Tatu si babati tu unawapata..
 
Watu kwa ground wanauziana magari hum hum bongo, maelfu kwa maelf, kama huamn fuatilia utitili wa platform mbalimbal za madalali wanaopromote na kuuza magari ndipo utajua ukwel.

Kinachofanya watu wasiagize nje ni hiyo tabia ya kotoza kodi ndefu ambapo kihalali haikutakiwa iwe hivyo,so bora tuuziane humu humu
 
Wakati namba D ikielekea kuisha tujikumbushe idadi ya magari yaliyoagizwa chini ya namba D.

Kwa mfano, Namba T100DAA, ili kubadilika na kua T100DAB inahitajika magari 899, herufi ziko 25 kutoa herufi I. Hivyo kubadili herufi moja inahitajika magari 899 mara herufi 25 unapata magari 22,475.

Kubadili kabisa herufi kutoka DAA kwenda EAA inahitaji magari 22,475x25 sawa ma magari 561,875. Kwa maana kwamba kwa namba D ambayo imeanza mwaka 2014 na inaisha mwaka 2022 ni miaka 8 Tanzania imeagiza magari 561,875.

Kwa maana kwamba kwa mwaka Tanzania wastani tunaagiza magari 70,234 ama magari 5,852 kwa mwezi sawa na magari 195 kwa siku.

Hii ina maana kwamba kwa wastani wa watu milioni 60, milioni 30 ikiwa ni nguvu kazi tunaagiza gari 5,852 kwa mwezi ni ishara ya umasikini mkubwa sana.

Mbaya zaidi magari hayo 95% ni second hand ya miaka mingi. Ukiangalia Watanzania wanaagiza magari ya mwaka 2000 hadi 2008. Hayo ni ya kutembelea, ya usafiri kama daladala ni ya kuanzia mwaka 1995 hadi 2000.

Magari ya kuanzia 2010 Tanzania ni ya kutafuta kwa tochi. Serikali pekee na watanzania wachache sana wanaagiza magari ya kuanzia 2018 na kuendelea.

Mimi mwenyewe kimkweche changu ni cha mwaka 1999 niko vidudu😂. Aibu ya mwaka.

Hii nchi miaka 62 ya uhuru bado ni maskini wa kutupwa. CCM imenajisi hii nchi kwa kiwango kisicho na mfano.
Badala ya kupima ukwasi wetu kwa exporting, wewe umetupima kwa importings.

Kweli ulienda shule kusomea ujinga
 
Hii ni kwasababu gari serikali imeifanya kama luxury commodity,kodi inakaribia nusu ya bei ya gari...gari inauzwa Japan/UK kiasi cha $3000 hadi ifike Dar port yaweza kua $3500 ila sasa kuitoa hapo uwenayo mkononi kodi inaweza kua hadi $2500 utashangaa ile gari utaipata kwa $6000 ....iyo kodi waipunguze kwa nusu ili watu waagize magari kwa wingi pesa watapata tu kupitia kuuza mafuta,vipuri,parking kwenye maeneo ya manispaa nk ...
Gari kwa sasa ni kama tu simu ,pikipiki sio usafiri rasmi mana risk yake ni kubwa sana na ndio imekua kama usafiri rasmi sasa
Kodi za kipuuzi kama hizi zinaua uchumi vibaya sana, na sio magari tuu huu ujinga ni kila kona na yule mporipori yuko busy kuongeza matozo kila siku, serikali inasafisha wananchi kuliko riba za mabenki
 
Magari mengi ndio utajiri?
Kuna jamaa kasaidia watu kama wewe kuewa hapo juu. Kaandika hivi.

expand...
Moja ya kipimo cha umasikini au utajiri (poverty & wealth ranking) ni kuangalia mali mtu anazomiliki kwa mfano nyumba (ya miti & udongo, ya matofali, nyasi fulu suti etc), baiskeli, Pikipiki, gari etc... Mfano kama wewe humiliki hata bodaboda au baiskeli, huna nyumba hata ya matope na nyasi wewe tayari una indicators za umasikini...
 
Badala ya kupima ukwasi wetu kwa exporting, wewe umetupima kwa importings.

Kweli ulienda shule kusomea ujinga
Nadhani umeandika ili uonekane unajua maana ya exports and imports ila havihusiani na hii mada kabisa.

Hii mada inahusu uwezo wa mtu mmoja mmoja kumiliki mali. Mojawapo ya mali anazopaswa kua nazo mtu ni pamoja na vyombo vya usafiri kama gari na gari hazitengenezwi nchini, lazima ziagizwe.

Exports/imports inaangalia uwezo wa nchi kuuza nje na kununua nje, nchi kama nchi sio individual.
 
Nadhani umeandika ili uonekane unajua maana ya exports and imports ila havihusiani na hii mada kabisa.

Hii mada inahusu uwezo wa mtu mmoja mmoja kumiliki mali. Mojawapo ya mali anazopaswa kua nazo mtu ni pamoja na vyombo vya usafiri kama gari na gari hazitengenezwi nchini, lazima ziagizwe.

Exports/imports inaangalia uwezo wa nchi kuuza nje na kununua nje, nchi kama nchi sio individual.
Kununua gari ndo dalili ya ukwasi wa mtu binafsi?
Shule umetoka lini?
 
Back
Top Bottom